kipusy
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 639
- 323
By experience!
Nenda mikoa ya Iringa au Mbeya, nunua mahindi moja kwa moja kwa wakulima, sogeza mahindi kwenye mashine ya kusaga iliyo karibu ili kupunguza carriage cost!
NB: hapa uwe umeshaongea na watu wa mashine, ikiwezekana uwe unawaachia pumba ili gharama ya usagishaji iwe chini zaidi (chini ya 5000/= kwa gunia)
Mahindi yakifika kiasi unachotaka, anza kusaga na kupaki(kwa kuanza unaweza kuwa unatumia mashine ya kushonea ya kukodi na mifuko yenye nembo ya mtu mwingine (mtafute)!
Gharama ya mfuko tupu usio na nembo ni around 200-350 bei ya jumla na 400-600 wenye nembo)
Kipimo kiwe kilo 5, 10, 25 na 50 (gharama ya upakiaji kwa makuli ni around 700 kwa kila kilo 50!
Tafuta magari yanayosafirisha mizigo mikubwa, ongea nao wakuunganishie mzigo wako kwa wasafirishaji wengine (madalali are so good in this)!
Mzigo ukifika mkoa wako wa soko waombe wakushushie sehemu ambayo ni rahisi kwako!
Zambaza mzigo kwa wateja wako!
Nzuri ukiwa unasaga kwenye mashine zako ili kudhibiti viwango.