Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usije ukadanganyika kufanya hiyo biashara bila kuchukua dhamana kutoka kwa mkopaji.Wakuu heshima yenu,
Nimeanza biashara ya kukopesha!! Nimeandaa daftar la kuandikishana Ila kuna watu wengi tunashindana kwa sababu kila wakija nawambia waniachie kitu ndo nimpe pesa wengine wanakataa kwan kungine hawaletewi masharti ya hivo!!
Nilkua naomba ushauri TOFAUTI NA KUANDIKISHANA NIFANYE NINI ILI NISIZURUMIKE ???
Ni Vitu gani unaweza ukachukua kama unataka kumkopesha MTU? (10000-100 000)
Kwa ushauri
Wataalam na wenye uzoefu tafadhari
Mi SAA iz sina hamu usiwaamini watu kwa maneno yao!! Mi mwenyewe nimelizwa Mara kibao!! Sina hamu yaan!!! Ila kwenye hela hata awe mchungaji usimuaminiwolf5100 mkuu nimekuelewa sana somo lako. Nimeshalia sana, na kupoteza marafiki kwa mambo kama haya.
Tena bahati mbaya nilikua nawaazima watu kwa lengo la kuwasaidia bila riba, binadamu hatufanani na kulipa madeni ni kipaji.
Ahsante kwa somo.
Tena watumishi wa serekali ndo wateja wakubwa,kwakweli watu wanataabikaKwa kipindi hiki cha uncle Mzee baba, hii biashara naona imeshika kasi sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Mtaji ni sh ngap mkuuHuwezi kusajili microfinince company wakati una mtaji wa milioni 2
kweli maarifa n muhmumimi pia ninafanya iyo biashara.sijaisajili bado kwa sababu ninabiashara nyingine naifanya inanikeep bize sana.sijapata muda hasa.
-utaratibu wangu unaacha dhamana kiwanja,hati ya kiwanja au nyumba,kadi ya gari na gari lenyewe,laptop,smart phone kwa kampuni za apple samsung sony htc,au hisa kwenye kampuni flani.
-dhamana unayoiacha ni lazima ivuke 87% ya pesa unayotaka.na huwa ninatoa 60% hadi 80% ya thamani ya dhamana.kulingana na dhamana yenyewe.
-cha muhimu ww kama c.e.o uwe na mwanasheria unayemwamini,uwe na proffesional surveyor kwa ajili ya evaluations,viwanja na nyumba.kingine uwe na watu 5 professional&mixer ambao watakuwa washauri wako.
-malipo ya mkopo wangu ni 17% kila mwezi kwa muda wa miezi 8 au 4.+ amount uliyochukua. yaani 17% kivyake na amount uliyochukua kivyake.wafanyabiashara wengi wamjini wanakopesha kwa 35% interest+ amount ulioichukua/utakayoichukua.
-loan processing fee yangu ni 9% inalipwa kabla au up on loan delivery.
-Ila kwa sasa nakopesha wafanyabiashara wa mazao,wakulima,wafanyabiashara wenzangu wa madini na wanaohitaji kuingia kwenye madini au kilimo/mazao.biashara nyingine ninayokopesha ni jumla na rejareja.Nakopesha wanaotaka kuingia kwenye biashara,cha muhimu dhamana.
-Pia mkopaji anasign transfer documents kwa mwanasheria wa hiyo dhamana yake kuja kwa jina langu.akishindwa kulipa ndani ya siku 90 kisheria namfilisi bila kusuburi sekunde.
-Biashara hii inautajiri wa haraka sana,kuna mbinu na ubunifu.
+255627575354