Biashara ya kuku wa mayai na nyama

Biashara ya kuku wa mayai na nyama

Anolway

Senior Member
Joined
Feb 6, 2021
Posts
158
Reaction score
590
Habari wakuu,,,
Naomba kuuliza wenye uzoefu na biashara za kuku, ni biashara ipi inalipa zaidi kati ya ufugaji wa kuku wa mayai au kuku wa nyama??

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Faida katika Biashara hizi zote mbili hutegemea mahali au uhitaji wa soko kuna mahali mayai trei yatauzwa 10000 na mahali pengine trei hio hio 4500.
 
Biashara yoyote inategemea masoko; kwahio huenda zote zisilipe (inabidi u-account kwa yafuatayo)

Chakula, Labour Cost na Muda..., gharama kubwa hapo ni chakula sasa kama ni kuku wa nyama imefika siku ya kuwauza ila unachukua wiki mbili kuwamaliza hapo ni wamekula chakula cha wiki mbili bure....

Kwenye mayai angalau utakuwa unatoa kidogo kidogo kulingana na soko kwahio huenda wasile bure..., ila je umeangalia mambo ya mortality (vifo, magonjwa n.k.) yaani risks involved ?

Na je muda wako ? (Muda unaoutumia hapo utakuwa na furaha - yaani unapenda unachokifanya) au utakuwa unanungunika hadi kupelekea magonjwa ya stress ?

In short kila kitu sio cha kila mtu, ushauri anza kidogo kidogo upate experience pili unaweza ukaanza kwa kuwa muuzaji (unachukua point A unauza B) all in all masoko ni muhimu sana tena sana....
 
Mkuu wapi trei inauzwa Tsh 4500???
 
Asantee, [emoji120] nitafanyia kazi...

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Faida katika Biashara hizi zote mbili hutegemea mahali au uhitaji wa soko kuna mahali mayai trei yatauzwa 10000 na mahali pengine trei hio hio 4500.
Ilala trey ni 6500,chini ya hapo nielekeze ulipo nami nikanunue
 
We anza kufuga wowote tu...changamoto zipo na zitakupa uzoefu...
 
Kama una mtaji mdogo fuga wa nyama, baada ya wiki nne unauza. Kuku wa mayai inabidi uwe na mtaji wa kuwalisha miezi minne hadi mitano ndio uanze kupata hela wakianza kutaga.
 
Back
Top Bottom