Biashara ya kununua korosho mwaka huu mnaionaje soko lake wadau.

Biashara ya kununua korosho mwaka huu mnaionaje soko lake wadau.

Profesa wa Maliasili

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2018
Posts
632
Reaction score
1,910
Baada ya mama kutuongezea chajuu kidogo kwenye salary nimeamua kujilipua benki nimevuta mkopo wa mulioni ishirini, milioni kumi nimefanyia finishing ya nyumba yangu ya kuishi na kumi zilizobaki nataka nifanye biashara ya kununua na kuuza korosho almaarufu kangomba.

Naomba mwenye uelewa anieleweshe kujua bei inaweza ikacheza vipi sokoni kuanzia mnada wa kwanza maana hadi sasa nina tani moja nimeshanunua kwa bei ya kilo1 @1500 kwa wakulima.

Nimeamua kusimama kwa muda ili nisome upepo kwanza nisije kuchukua mzigo mkubwa halafu bei ikawa chini ya niliochukulia mzigo.

Mwenye uelewa na hii bishara naomba Abc's tafadhali kwa mwaka huu mnaonaje soko lake.
 
Nunua tu kutokana na trend ya mvua duniani mwaka jana na mabadiliko ya tabia nchi mavuno ya korosho yako chini sana hivo kwa namna yoyote ile bei itakua juu maana uhitaji ni mkubwa
 
Nakushauri simama hapo kwanza..ila panga mipango yako vizuri..baada ya mnada wakwanza ndio kanunue.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kama una 10M, basi nunua mzigo wa milioni 7 au nane then hiyo inayobaki ndo itakuwa kujazia kama hasara itatokea. Ila kwa uzoefu wangu haiwezi kushuka zaidi ya buku jero. Zingatoa usafi wa mzigo wako. Mwaka jana kuna watu walikesha godown wakichambua mizigo yao.
 
Kwa uzoefu wako mkuu ukisoma upepo wa mwaka huu unaona bei inaweza kuanzia sh.ngapi kwa kilo?
 
Kama kuna mtu ana hela nzuri aje tukanunue korosho hata za milion 50 kama akitaka ,faida inagawanywa 40% kwa 60%

Uaminifu ni 100% hela unakuwa nayo mwenyewe unakuwa eneo la tulio ukitaka kwa muda wote wa manunuzi........

Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom