Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Heshima kwenu wakuu!

Nimekuwa nikiwaza muda mrefu kuanza biashara ya kilimo. Ninaipenda sana japo sijawahi kuifanya. Nimetamani kuanza kununua mazao ama kwa kuyauza moja kwa moja au kwa kuyatunza katika ghala ili niwe nauza baadaye bei ikiwa nzuri.

Ninao mtaji kidogo kwa kuanzia lengo ni ili niweze kukua kidogo kidogo na sio kuweka pesa nyingi ambayo ninaweza kula hasara kipindi naanza biashara hii.

Sijachagua mazao maalum ya kuanza nayo na ndio maana nahitaji mawazo yenu.

Hivyo basi nipo hapa kuomba ushauri ni mazao gani ninaweza kuanza nayo, mtaji mdogo ambao unaweza kufaa kuanza nao ni kiasi gani, maeneo na masoko ya biashara ya mazao ndani na nje ya nchi ni yapi?.

Nitashukuru hata kwa ushauri wa ziada mtakaonipa.
 



NA mie pia ntasubiri jibu toka kwa wataalam wakija hapa
 
mimi ni mukulima mdogo mdogo niko huku morogoro wilaya ya mvomero maeneo ya manungu tulian, huku nimelima mpunga nina heka sita za mpunga na nategemea kuanzia wiki (jmos) ijayo nianze kuvuna, hivyo kama utakua unahitaji mpunga au mchele tunaweza kufanya biashara ndugu!
 
Ukivuna utauzaje mchele kg 1?
 

Ulishatoka kwenye ajira??
 

Heka 6 imegharimu Tshs ngapi?
 
Habari wadau,

Kwa sasa niko Mbeya mjini hivyo nimeona kuna fursa naweza ifanya nataka ninunue mchele Mbeya mjini then niutume Dar kwa ajili ya kwenda kuuzwa.

Hivyo wadau wenye uzoezi na biashara hii wanisaidie kunijuza yafuatayo:

1. Ni wapi naweza pata mchele kwa bei nafuu kwa hapa Mbeya mjini(nimeajiriwa hivyo kwenda nje ya hapa mjini itakuwa vigumu).

2. Njia ya usafiri (nafuu) nitakayotumia kuusafirisha kwenda Dar.

Ni hayo tu.
 
Wewe naona unataka kukosana na watu wako wa karibu.
 
Biashara za kusimamiwa na mtu mwingine zimeliza wengi, labda kama mtaji wako ni wa kupewa bure na atm Fulani!
 
Naomba msaada wa muhitaji wa bidha za mazao tunauwezo wa kukufuata mteja mpaka ulipo kwa bei nafuu bila kujari umbali dream, Morogoro, Iringa, Lindi, Mtwara nk bidhaa hizo nikama vile.
- Maindi
- Maharage ya rangi yoyote utakayo
- Viazi vya aina zote yaani mviringo (vya chip's) nk
- ndizi Nk
Kwa yeyote anae hitaji kuingia kwenye mfumo huu wa bihashara ya mazao ya aina mbali mbali
 
Gunia la viazi shilingi ngapi, na ni la ndoo ngapi?
 
Kama wewe u na deal na mazao Kwa kununua na kuuza tafadhali weka mahitaji yako hapa tukutanishe wanunuzi na wauzaji karibuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…