Mkuu,
Kabla sijatoa ushauri wangu kwako kwanza nianze kwa kukupongeza kwa WAZO ulilolipata.
Lakini pia kwa maswali ulioainisha hapo juu, kwa mtu aliyemakini tayari una majibu kwa maswali yote maana umesema tayari una jamaa zako wa karibu wanaofanya biashara hiyo na tayari wameonyesha nia ya kukubeba yaani wapo tayari kukuonyesha njia. Nitashangaa sana kwa mtu ambaye tayari anafanya biashara hiyo then hawezi kukupa majibu ya maswali uliyouliza hapo juu.
USHAURI: Mtaji ulonao ni Pesa sawa lakini kwa biashara ya mazao hiyo haitoshi na kwakuwa unayo hiyo tu nikisema nikutajie kiasi ambacho unaweza kuanza nacho na ukajisikia inafanya kazi nitakuwa kama nakukatisha tamaa hivi.
Sasa basi huo mtaji ulonao (1mil) itakulazimu ujiunge na mmoja wa hao jamaa zako ulowataja ili akubebe tu hapa nina maana kwamba mwende naye huko vijijini ambapo yeye anapata mzigo mnunue kwa maana kwamba atajulikana kwa wauzaji kuwa anayenunua ni yeye (mwenyeji wao) kumbe ndani ya mzigo kuna vigunia vyako 4-5, mkija kwenye masoko anapouza huyo jamaa yako mwachie auze yeye na baadaye anakutolea pesa yako, hapo utaona mtaji na faida yako.
Ninakupa wazo hili kutokana na ufinyu wa mtaji wako.
Kwa kufanya hivyo, utakuwa unatunisha mtaji wako, lakini pia utakuwa unapata uzoefu ktk Kazi hiyo.
Baada ya muda mtaji wako utakuwa umeongezeka, lakini pia utakuwa mzoefu ili baadaye uweze kupeperuka kwa mbawa zako.