Kipi bora, kununua mchele ama mpunga? Sababu utajuaje mpunga unaonunua utatoa mchele mzuri unaotaka kwa ajili ya biashara Kipi bora kwa ajili ya biashara, mpunga au mchele?
Kadri ya jinsi nilivyoelewa maswali yako juu:
Ili kujua mpunga kama ni mzuri huwa tunachukua sample na kuumenya na kisha kutathmini ubora wake-mzuri hutoa punje zilizonyooka na nyeupe wakati mbaya hutoa mpunje zilizovunjikavunjika, ama nyekundu badala ya nyeupe.
Pia ubora wa punje/mchele huweza tegemeana na mashine uliyokobolea na technician anaeseti mashine-kuna mashine zenye wataalam wa kuseti mashine kulingana na mpunga unaokobolewa kwa wakati husika na mchele wote utokao kwenye mashine hizo ni "super" au ulionyooka tu.
-Ubora wa mchele hutathmini faida utakayopiga wakati wa kuuza mchele huo
Kwa mtaji mkubwa wa kuweza kununua tani hata 2 za mchele ni vyema ukauza mchele pale bei ya mchele inapokuwa juu zaidi sokoni wakati mashineni ukiuzwa kwa bei ya chini. Kwa mfano kama mashineni unauzwa kwa Tsh.800 kwa kilo na kuuzwa kwa Tsh. 1400 sokoni na wewe ukanunua tani 2 kwa Tsh. 1,600,000/- na kuuza kwa Tsh. 2,800,000/- wakati gharama ya usafiri ni kama 90,000/- kama utakuwa umetoa mzigo Shinyanga kuja Dar kwa mfano, hapo unakuwa umetengeneza faida ya 700,000/- kwa safari moja.
-Faida itaongezeka kutegemeana na safari unazofanya kwa wiki yaani safari moja, mbili au tatu; na hii inaonesha atakaepiga faida zaidi ni yule anaenunua mchele na kusafirisha moja kwa moja kuliko anaechukua mpunga na kupanga mstari mashineni ili akoboe ambapo anaweza koboa tani chache tu siku.
Kuna wakati pia kununua mpunga na kuuhifadhi kwa ajili ya kukoboa na kuuza baadae kunalipa sana, kwa mfano ikiwa leo gunia linauzwa kwa Tsh. 55,000/- na ukanunua na kulihifadhi hadi mwezi wa 12 (2016) au kwanza mwakani (2017) ambapo bei inaweza kuwa 85,000/- hadi 100,000/- kuna uwezokano wa kupiga faida isiyopungua 25,000/- kwa gunia kama utauza mpunga kama mpunga; ukikoboa na kuuza mchele unapiga zaidi ya hiyo (25,000/-)
Kwa ujumla ni vyema kipiga zote (mchele na mpunga) kulingana na kile kinachotoa faida zaidi kwa msimu husika, eneo unalofanyia biashara kama vyote vinapatikana kama mpunga haupatikana usione tabu kwenda maeneo ama mkoa wanakolima na nununua kisha hifadhi au koboa-ukiwa mfanyabiashara lazima uzungukie maeneo ya interest yako na utajua mikoa mingi na hata vijiji vingi nchini na umbali kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine hususani ukishakuwa na usafiri wako.