Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Kula MTU humu nimeona akiisifia biashara ya mchele....
Naomba kufahamishwa kuhusu uhakika wa soko tafadhali kwa maana ya kuwa natakiwa nikatafute mteja then aniambie kapasite yake ya kuchukua mzigo ndo nimpelekee au ni kwamba wateja hupatikana bila tatizo nikifika sokoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
najifunza mengi sana humu... nadhani siku si nyingi ntaazisha namm biashara yangu.. namba tu tusiacha kushauriana pindi tunapohitaji msaada wa ushauri kwa wale wazoefu..... Ahsanteniii
 
Bro kama hujawahi hustle na vi business vya kitaa huwezi nielewa au unaweza sema siko serious na life.

I’ve done pass all that..as i speak nina biz kubwa tu tena ya wholesale..

Biashara zina mambo mengi sana, Kwa mtu anayetaka kutoboa in a big way mimi kama
mimi binafsi nashauri atafute capital atleast isiyopungua 100+ million (Thats if mtu huyo ana plan kufanya any type of trading biz)

Kwa capital hyo any trading biz lazima utatoboa..ila sijui una 5M au 10 M utapata hela ndio ila ya kubadili mboga tu.

Ila kama nina elimu yangu nzuri average salary nipate between 1 M to 3M au mpaka 5M kwa mwezi nibora niajiriwe kwa atleast 3 years ni make hela then nizame kitaa na capital.

Maana yake kama hela huna possibly likely hata collateral mtu hana. Ya dig ??
Mkuu kwa mawazo hayo kufanikiwa basi kila mtu anajion kwa jicho lake..si kweli kuwa ukitaka kutoboa uwe na hiyo capital ya kuanzia 100m..ukiidharau 100 basi hata hyo 100m haitakusaidia kitu
 
Bei ya mahindi leo. Singida gunia la kilo 100 linauzwa 54000.

Arusha au manyara gunia hilo hilo linauzwa 100,000.

Nikichukua gunia 100 za mahindi singida nitatoa 5.4M. Usafirishaji kwa gunia moja ni 5000 hadi manyara. Kwa gunia 100 nitalipa 500,000 usafiri. Hapo sasa natakiwa kuwa na 5.9M

Nikienda kuuza gunia 100 manyara kwa bei ya 100,000 kila gunia nitapata jumla ya 10M. Nikitoa gharama za usafirishaji na hela ya mtaji nitabakiwa na jumla ya shilingi 4.1M.


Net profit hapa ni 4.1M.
Kazi hii naweza kuifanya ndani ya wiki moja kuanzia kukusanya magunia singida hadi kuyapeleka kuyauza manyara.
................................................................

Oya mwenye 5.9M ya haraka hapo aingie chimbo akapige hiyo hela. Faida ya milioni 4 ndani ya wiki moja sio hela kidogo. Hii ishu ni uhakika, hata kama hutapata hiyo 4M huwezi kukosa hata 2M.


Ngoja niendelee kujichanga kamtaji kakue nikapige hiyo hela.

Jioni njema.
Kamwe Singida mahindi hayawezi kuuzwa bei hiyo, unadanganya watu
 
Kamwe Singida mahindi hayawezi kuuzwa bei hiyo, unadanganya watu
Nilishangaa anaongelea mahindi gani. Yani Singida mahindi yawe cheap kuliko Manyara!

Manyara hii hii iliyoko kwenye production zone yani ndani ya zile big 5 regions zinazotegemewa kwa uzalishaji wa chakula hasa mahindi. Never..

Kwa mpaka Sasa hakuna sehemu yenye kuuza mahindi gunia kwa 54,000. Rukwa kwenyewe ambao ndio baba lao kwa uzalishaji wa mahindi Bei hivi Sasa Ni 85,000 mpaka 90,000 eti Singida wanakolima alizeti na vitungunguu yakawe 54,000??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu unaweza kuwa ni mwaka wa njaa.
Baada ya kuwepo kwa over supply ya mahindi mwaka jana hivyo kupelekea kuporomoka kwa bei, mwaka huu unaweza kuwa ni wa neema kwa wafanya biashara ya mahindi.
Kama una milioni kumi haina kazi, nunua mahindi sasa uyahifadhi. Unaweza ukaja kuyauza hata kwa milioni 20 mbele ya safari.
Huku kwenye Kangomba ya mahindi ni clean business. Mkono wa dola haufiki huku. Kazi kwenu wasaka fursa.
Unaweza - just like anything in life....,
Normally kwa mwaka wa kawaida mahindi huwa yanakuwaje katika hii biashara what's the profit margin
 
Huu unaweza kuwa ni mwaka wa njaa.
Baada ya kuwepo kwa over supply ya mahindi mwaka jana hivyo kupelekea kuporomoka kwa bei, mwaka huu unaweza kuwa ni wa neema kwa wafanya biashara ya mahindi.
Kama una milioni kumi haina kazi, nunua mahindi sasa uyahifadhi. Unaweza ukaja kuyauza hata kwa milioni 20 mbele ya safari.
Huku kwenye Kangomba ya mahindi ni clean business. Mkono wa dola haufiki huku. Kazi kwenu wasaka fursa.
Vipi mwaka huu? Kama msimu uliopita kulikuwa na upungufu kiasi wa mahindi, vipi mwaka huu?
 
Back
Top Bottom