Biashara ya Kusafirisha Mazao Nje ya Nchi: Jifunze Utaratibu wa Kufuata, Changamoto, Faida na Uzoefu wa Wengine

Yaani ndio maana bongo kuendelea kazi ipo. Wewe si umsaidie mwenzako akupe mrejesho baada ya kuuza maana unataka cha juu utadhani dalali.
Sikuipata bure hiyo database mkuu. Si lazima kuishare mkuu. Nilifanya jitihada kupata. Simlazimishi yeyote. Siku njema
 
Badala ya kuwapatia mmoja mmoja ngoja nitengeneze portal kabisa. Nitawapa mrejesho wote ikikamilika.
 
Wana Jukwaa kwema? Hebu tusaidiane hapa jambo moja. Napenda sana hii biashara ya kusafirisha mazao nje ya nci, sijawahi kuifanya lakini naona kama vile ni field nzuri kwangu. Je ni zipi changamoto zake? Nimepata baadhi ya taarifa kwamba kuna baadhi ya nchi zinahitaji sana mazao ya Tanzania nchi kama Japan, China, India, Oman, South Africa na kwingineko.

Naona kuna fursa hapa, hebu tujadiliane tuone nini tunaweza kufanya kwa pamoja. Kumbuka Information is POWER.
 
Njioni mtupe elimu. Imekaa vizuri sana. Kenya wana export sana Maua, kahawa na Chai. Uganda ana export chai na kahawa pia ndizi za matoke anapeleka UK.

Jana nilienda kununua chai sehemu nikaona majani ya chai kutoka Rwanda. Sasa kumbe hadi Rwanda ana export kwenda duniani kwa nini na sisi tusifanye?
 
Jamaa wa nchi jirani wanafanya Export ya kufa mtu, why not Tanzania?
 

NI BIASHARA NZURI. FANYA UTAFITI WA UHITAJI WA MAZAO

Hakika ni biashara nzuri sana. Wengi wanashindwa kufikia matakwa ya Viwango yanayotakiwa katika masoko hayo.

Jambo la kwanza; fanya utafiti mdogo wa uhitaji wa mazao yanayotakiwa katika Nchi unayotaka kupeleka. Pamoja na kujua bei lakini mambo muhimu katika soko ni pamoja na; Viwango vya ubora vya nchi hiyo; mfano (tu) Japan wanataka ufuta wenye ubora (usio kuwa na taka taka) wa aslimia isiyopungua 95, endapo ufuta huo utatumika katika uokaji.

Viwango hivyo hutofautiana kulingana na aina mazao, soko/nchi, na matumizi ya bidhaa hizo kwa mlaji; Vivyo hivyo, wanaangalia viwango vya vimelea kama backteria, mabaki ya sumu za madawa yaliyotumika katika uzalishaji, na kuvu (fungus) nk. nk. katika mazao hayo.

Jambo hilo ni muhimu sana katika masoko ya Ulaya, Amerika na Japan. Nafuu kidogo inapatikana ukiuza katika nchi zingine kama za Uarabuni na Africa.

Hata hivyo, vitahitajika endapo mnunuzi katika nchi hizo nafuu, atataka auze Ulaya. Ni, kwa ufupi tu. Pamoja na maelezo yangu mafupi, yote hayo yanawezekana, na kuna watu wengi hapa kwetu wanafanya; kwa mazao ya chakula na viwanda. Pasi shaka, ukikaza nia utafanikiwa pia.
 
Aisee MUNGU akubariki, hio ya ufuta nasikia ni hot cake kwa Japan. Dah
 
CHANGAMOTO YAKE KUBWA NI URASIMU WA SERIKALI

Nilipata dili flani la kupeleka Mzigo Mwingi tu Comoro nikakusanya Nguvu za Jamaa zangu Kama wawili tukakusanya Mtaji wetu mdogo tu Kama 20 Million.

Tukashauriwa Tufuate Vibali halali

Tu kaanza kuelekezwa tuanze Board of External Trade, huko ikapigwa Danadana twende Chamber of Commerce kule wakatueleza kazi yao ni kutoa Vibali tu tukitaka kujua kitu gani kinaruhusiwa kipi hakiruhusiwi twende Wizara ya Mifugo au Kilimo ndio wenye orodha ya Mazao yanayoruhusiwa kusafirishwa nje ya nchi.

Niliwauliza wale watu wa Chamber of Commerce pale kwenye Barabara ya Morogoro na Samora (PPF House) kwanini hiyo orodha ya vitu vinavyoruhusiwa kwanini wasikae nayo pale kupunguza Urasimu Jibu wanatoa huo ndio utaratibu 'Mzee usilete Ujuaji fuata taratibu'

Tulipofika Wizara ya Kilimo ndio balaaa Urasimu mpaka tukaamua tusafirishe kienyeji.
 
Ndugu, ninakubaliana na wewe kwa asilimia zote. URASIMU. Mimi nilipata tenda ya kupeleka chakula cha mifugo hapa jirani tu, Kenya.

Kwa "ujinga" wangu nilitaka kurasimisha shughuli yangu kwa kufuata taratibu zote husika, wizara ya kilimo na mifugo aliyenipokea nadhani hajui hata kilichomuweka hapo, nikarushwa niende TFDA. Huko nako, wakaanza kunishangaa tu kama vile nimepotea njia. Hawajui kama wanahusika na biashara yangu. Nikarushwa niende TRA. Huko nako wakasema nipate kwanza kibali toka wizara ya kilimo na mifugo, pamoja na TFDA.

Nikaanza zoezi upya kupitia hizo office. Hakuna nilichoambulia, zaidi ya dharau kutoka kwa watumishi wa serikali.

Kwa vile mzigo ulikuwa tayari mteja ameshalipia na kutuma lori kwa ajili ya uchukuzi, tulipakia mzigo na kumwachia dereva afanye maalifa yake mzigo ufike. Hatukuwa na namna, maana mamlaka zote husika ni kama vile hawajui kwamba biashara ya nje kwa maana ya export inaleta pesa za kigeni kwa taifa.

Hapa bado kunatatizo kubwa sana! Sijui nani ataweza kutusaidia angalau kuwe na mamlaka moja inashughulika na biashara ya nje, ambapo unaweza kupata vibali na taratibu zote husika ukitaka kufanya hiyo biashara.
 

Eti Nchi ya Viwanda!

Board of External Trade kazi Yao ni kuleta Vipeperushi na kuvisambaza Sabasaba nothing more.

Utaratibu wa ku Export ni urasimu kuliko wa Ku Import wakati Exports ndio huchochea ukuaji wa Uchumi kuliko Import!
 
Uzi mzuri sana huu. Big up mleta mada kwa kuanzisha mjadala huu. Ku-export mazao, nchi hii ni urasimu tu ndicho kinachowakwamisha wengi. Ubabaishaji mwingi kwenye office za Serikali. Maofisa hawajuwi hata majukumu yao kama mdau alivyochangia hapo juu.

Nadhani kuna haja ya kulipigia kelele suala hili, kwamba kuwe na taasisi MOJA tu ambayo ihusike na utoaji wa vibali na clearance zote kwa mtu anayetaka kuexport bidhaa nje ya nchi.

Mie natafuta mzoefu wa biashara hii ya mazao awe 'mentor' wangu anipe A to Z jinsi ya kufanya & ku-excel kwenye biashara ya nafaka/mazao kwa soko la hapa hapa nchini.

-Kaveli-
 

Huu ndio urasimu tunaoongelea.

Ukiangalia Sharti no. 4 na namba 8 utajua kabisa si Sharti la Kibiashara!

Inaonekana Kibali kinachotolewa sio cha biashara ni cha kuvusha Mazao wao wanaita cha Biashara!

Nitaje aina ya Zao na kiwango ninachotaka kusafirishwa Ina maana nikishapata kibali cha Machungwa nikapewa taarifa kuwa soko la Machungwa lime change lete Mananasi maana yake nikaombe kibali upya? Tunaanda sera na taratibu kijamaa kwny soko huria

Ukitaka kupeleka Mzigo Mara ya pili unaandika report then unaomba Tena kibali [emoji12][emoji12][emoji12] hii sio Biashara BAKITA watohoe jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…