Hakika ni biashara nzuri sana. Wengi wanashindwa kufikia matakwa ya Viwango yanayotakiwa katika masoko hayo.
Jambo la kwanza; fanya utafiti mdogo wa uhitaji wa mazao yanayotakiwa katika Nchi unayotaka kupeleka. Pamoja na kujua bei lakini mambo muhimu katika soko ni pamoja na; Viwango vya ubora vya nchi hiyo; mfano (tu) Japan wanataka ufuta wenye ubora (usio kuwa na taka taka) wa aslimia isiyopungua 95, endapo ufuta huo utatumika katika uokaji.
Viwango hivyo hutofautiana kulingana na aina mazao, soko/nchi, na matumizi ya bidhaa hizo kwa mlaji; Vivyo hivyo, wanaangalia viwango vya vimelea kama backteria, mabaki ya sumu za madawa yaliyotumika katika uzalishaji, na kuvu (fungus) nk. nk. katika mazao hayo.
Jambo hilo ni muhimu sana katika masoko ya Ulaya, Amerika na Japan. Nafuu kidogo inapatikana ukiuza katika nchi zingine kama za Uarabuni na Africa.
Hata hivyo, vitahitajika endapo mnunuzi katika nchi hizo nafuu, atataka auze Ulaya. Ni, kwa ufupi tu. Pamoja na maelezo yangu mafupi, yote hayo yanawezekana, na kuna watu wengi hapa kwetu wanafanya; kwa mazao ya chakula na viwanda. Pasi shaka, ukikaza nia utafanikiwa pia.