Biashara ya Kutoa Mikopo (Microfinance): Hatua, Taratibu za Kufuata na Ushauri wa Uendeshaji

mfumo wa kukopesha hususan kwa nchi zetu changamoto kubwa ni watu kutokulipa ukizingatia wahitaji wengi hawana collateral hence hata wakishindwa kulipa utawafanya nini (labda utumie ubabe na njia zisizo za kisheria)..., watu wanaofaidika na issue kama hizi bila tatizo ni kina SONGESHA..., wanakukopa pesa ikiingia wanachukua chao na ni vigumu mtu kukimbia deni sababu simu yako na namba yako ni asset muhimu sana
 
Jambo kubwa katika biashara hii lipo katika utekelezaji. Ukiangalia msingi mkuu wa biashara hii ni SERA YA MIKOPO. Sera nyingi za mikopo hazikidhi vigezo vya uendeshaji wa hii biashara matokeo yake ndiyo hilo unalosema hapo juu.

Hii ina maana ya kwamba mchakato mzima kuanzia mteja kuomba mkopo, kukagua biashara au kazi anayofanya, vikao vya mkopo, uandikishaji wa dhamana, kiwango cha marejesho na hadi "recovery" iwapo mkopo haulipwi hazifuatwi. Kwa mantiki hy bhasi utaona mchakato mzima toka chini u akuwa umeshakosewa hvy tarajia changamoto kubwa ktk kulipwa laah uwe wasubiri uaminifu na uamuzi tu wa mdai kulipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua namaanisha kusajili jina la kampuni mfano badala ya kuandika MRX microfinance Ltd mm niandike MRX finance Ltd halafu nijihusishe na biashara ya kukopesha pesa je itaruhusiwa? Maana nimeona huo muongozo wako unajumuisha maneno matatu tu kama microfinance, financial service na microcredit ndo swali langu lililenga hapo? Au nn tofaut kati ya meneno hapo juu dhidi ya finance?
 
Nauliza Je hiyo Million 20 inakuwa fixed deposit? Maana najiuliza si mnaweza mkachanga mkaweka then after some time ukishasajili unaweza ukaitoa?
 
Hapana sio fixed. Kuna ukaguzi wa mara kwa mara na tambua kwa sasa unatakiwa kuwa na mfumo wa uendeshaji wa biashara hii na sio kila kitu kinamalizikia ktk cm yako tu!
Nauliza Je hiyo Million 20 inakuwa fixed deposit? Maana najiuliza si mnaweza mkachanga mkaweka then after some time ukishasajili unaweza ukaitoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inakubalika kuweka mojawapo ya neno hili : finance, credit, microcredit, microfinance au financial services
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kama mkopaji hatarejesha mkopo wake sheria inaruhusu kushikiria na kupiga mnada dhamana zake?
Pia napenda kujua riba pendekezwa kwa ajiri ya hizi Microcredit?
 
Hapana sio fixed
Kuna ukaguzi wa mara kwa mara na tambua kwa sasa unatakiwa kuwa na mfumo wa uendeshaji wa biashara hii na sio kila kitu kinamalizikia ktk cm yako tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mteja aliyeshindwa kurejesha utartibu wa upndishwaji riba kwenye mkopo wake upoje? na hufanyika kwa muda gani kabla ya kumpeleka ktk vyombo stahiki? Je, ni sahihi kumpndishia riba kwa miezi nane mfurulizo? Tuendelee kuelimishaan
 
Vipi kama mkopaji hatarejesha mkopo wake sheria inaruhusu kushikiria na kupiga mnada dhamana zake?

Pia napenda kujua riba pendekezwa kwa ajiri ya hizi Microcredit?
Kwa kuzingatia sheria ya mikopo kifungu cha 51 sehemu ya 56 Ukusanyaji wa madeni (1), ( 2) ukijumuisha na sera ya mikopo kuna taratibu zimewekwa ktk kumdai mdeni wako. Miongoni mwa taratibu ni

i. Kumpa notisi ya siku 14 mdeni wako juu ya kulipa deni baada ya hapo taratibu za kukusanya deni zitachukua mkondo wake
ii. Usimtishe, mtukane, kumwambia maneno mabaya, lugha chafu et al hadi no ivi.

Sasa basi baada ya taratibu hizo kushindika utatakiwa kufuata sheria kukamata mali zake na ukifanikiwa ina maana utatangaza mnada wa hadhara juu ya uuzaji wa mali ambazo aliweka dhamana na sio kuziuza au kuchukua mwenyewe kinyemela

Riba ni ile iwe reasonable

(Wanasheria na debt collectors and auctioners twaomba waje kufafanua vema zaidi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa mteja aliyeshindwa kurejesha utartibu wa upndishwaji riba kwenye mkopo wake upoje? na hufanyika kwa muda gani kabla ya kumpeleka ktk vyombo stahiki? je ni sahihi kumpndishia riba kwa miezi nane mfurulizo? tuendelee kuelimishaan
Kwanza tukirejea ktk kifungu cha sheria ya ukusanyaji wa madeni kama nilivyonukuu hapo uzi wa juu sehemu ya 56 (3 na 4) imeweka wazi kuwa:

i. Kampuni ya mikopo haitaruhusiwa kukusanya riba, gharama yyt ya ziada ikiwa hakukuwa na makubaliano kati ya mkopaji na mkopeshaji wakati wa kuingia mkataba wa kukopana pesa.

ii. Kampuni ya mikopo itaihusisha kampn ya kukusany madeni iliyosajiliwa na yenye leseni mahususi ya ukusanyaji madeni ambao kampuni hii ya ukisanyaji madeni itafanya kazi hy kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za ukusanyaji madeni.

Kwa kifupi hakuna kutumia ubabe kudai madeni bali fuata sheria tu kupata haki yako

Nyongeza
Unaweza pitia The Microfinance act (cap. 407), Regulations, soma kurasa na 25 na 26 Debt collection or recovery section 56 (1) hadi (4)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii sheria imezungumziaje swala la riba. Taasisi inaweza ikajipangia na kumtoza mteja riba yoyote bila kubanwa na sheria hii?
 
hii sheria imezungumziaje swala la riba...taasisi inaweza ikajipangia na kumtoza mteja riba yoyote bila kubanwa na sheria hii?
Haijawa wazi sana ila kuna viwango vipo kwa kutegemea na asili ya huduma inayopata mkopo. Utaona ipo kati ya 10% hadi maximum 25% (substandard) kwa mwezi rejea pg 20 na 21 classification and provisions for loans, Regulations.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafasi ya Bank kuu ya kuregulate viwango vya riba kwa taasisi za kifedha inakuaje. Tunatambua bank kuu iko responsible nakupangilia viwango vya riba kwa bank zote za biashara. Kama sijakosea, miezi michache iliyopita bank kuu ilipunguza riba moka 17%.

Je, utararibu huu hauzihusu micro finances?
 
mkuu shukrsni kwa elimu hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…