Habari za leo wanajukwaa,
UJUMBE MAHUSUSI: TUCHUKUE TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA, NI WAJIBU WETU SOTE KUKABILIANA NA JANGA HILI
Utangulizi
Rejea katika Makala yetu ya awali tuliyoiwasilisha mnamo tarehe 09 Agosti, 2018 ilikuwa bado suala la mabadiliko makubwa yaliyofanywa na serikali kurasimishwa:
MWONGOZO: Masharti na taratibu za kupata leseni ya kutoa mikopo kwa kutumia mtaji binafsi
Sasa kutokana na Mabadiliko hayo ya kisheria na pia rejea Notisi ya Benki Kuu ya Tanzania ya Desemba 2019 tumeona ni vema kuiboresha mada kwa kuileta kama sehemu ya pili ya maboresho ili wadau kujadili kwa upana wake na pia kuona faida na hasara zake kwa mkopeshaji na mkopaji.
Kwa Muhtasari
Biashara ya utoaji mikopo imezidi kushika kasi na kushamiri kwa kasi sana. Kundi hili linalojadiliwa hapa watoaji mikopo binafsi na makampuni binafsi yanayotoa mikopo kwa mitaji yao binafsi na hayaruhusiwi kuchukua na kuhifadhi pesa za wateja wao ie
Non-Deposit taking ambazo zipo katika
kundi no 2 (Tier 2)
Maboresho katika Usajili
Kwa mujibu wa sheria kampuni inayotaka kufanya biashara hii ya utoaji mikopo
MEMART yake iwe na sifa hizi:
1. Jina la kampuni lazima liwe na neo
“MICROCREDIT au MICROFINANCE au FINANCIAL SERVICES”
2. Biashara zitakazofanywa na kampuni hii lazima ziwe zenye mlengo
(objects) wa biashara ya fedha tu na si kwa kuchanganya na aina nyingine za biashara
3. Mtaji wa kampuni ni lazima uwe kuanzia milioni 20
Pia kampuni hii inatakiwa kuwa na yafuatayo:
1. Ofisi ambapo wakaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania wanaweza kuja kukagua muda wowote ikiwa kabla au baada ya kupata leseni
2. Lazima uweke bango la kuonyesha ni kampuni ya mikopo
3. Uwe na mifumo ya wazi ya uendeshaji wa kampuni husika pamoja na mawasiliano
4. Wakurugenzi wa kampuni wawe na elimu ya ufahamu wa biashara hii hata kama sio wasimamizi wakuu
5. Lazima kampuni ielezee namna ilivyoupata huo mtaji ambao unatokana na mchango wa wanahisa ikiwa kila mmoja ataelezea alipata vipi katika zile hisa alizolipia
6. Kuwe na uongozi kamili ie bodi ya wakurugenzi, CEO et al
Kwa mtu binafsi anaetaka kufanya biashara hii nae atalazimika kufanya haya:
1. Kusajili jina la biashara ambalo litakuwa na sifa kama zilivyoonyeshwa hapo juu katika kapuni
2. Mtaji ni kuanzia milioni 20 ambao anapaswa kuuelezea wazi kaupataje mtaji huu
3. Atawasilisha ripoti ya madeni
ie Credit Report from Credit Reference Bureau
4. Masuala ya kuwa na ofisi, mifumo rasmi ya uendeshaji biashara nk kama ilivyo katika kampuni nae atakuwa nayo pia isipokuwa uongozi
ie Board of Directors hatakuwa na hii
Akikamilisha vielelezo hivi na vikiwa sahihi basi hatua ya pili itafuata
2. Kupata TIN na Cheti cha Ulipaji kodi ie Certificate of Tax Clearance
- Hatua hii ya pili itafanywa upande wa Mamlaka ya Mapato ie TRA ambapo atalipa kodi stahiki zote kama vile kodi ya mapato, kodi ya zuio na ushuru wa stempu kwa mkataba wa pango. Kisha atapewa TIN ya kampuni au Mtu binafsi ambayo watakuwa wameongezea na jina la biashara na Cheti cha Mlipa kodi kitakuwa “addressed” kwenda BOT itategemea upo mkoa gani kwn zipo ofisi zao za kanda pia
3. Kuandaa Sera ya Mikopo na Wasifu wa kampuni na kujaza Questionnaires
- Kampuni au mtu binafsi utaandaa sera ya mikopo inayokidhi vigezo vya uendeshaji wa biashara hii ya mikopo kwa kuweka mambo yote muhimu kama vile Muundo wa uongozi wa kampuni, aina za huduma za mikopo utoazo, riba, taratibu za kutoa mikopo, taratibu za urejeshaji mikopo, riba, vikao vya upirishaji mikopo, taratibu za kukusanya mikopo chefu chefu, risks, ufutaji wa mikopo chefu chefu nk nk. Hii ni muhimu sana kwa sbabu ndiyo dira na mwongozo mzima wa naman gani utafanya hii biashara
- Vile vile kutatakiwa kuandaa wasifu wa kampuni, wakurugenzi na kila mtu ambae atahusika katika kampuni husika au kama mtu binafsi pia lazima uandae ikiwa pamoja na kuambatanisha vyeti vyako vya elimu na sifa nyingine za ziada
4. Maombi ya leseni (kibali) BOT
- Baada ya kukamilisha vielelezo vyote kampuni au mtu binafsia
- Ataandika barua ya kumchagua mtu maalum wa kufuatilia suala hili la leseni
- Atalipa TZS. 500,000 kampuni au TZS. 300,000 ambayo ni pesa isiyorudihwa hata kama maombi yako yamekataliwa hairudi.
- Ndani ya siku 60 utakuwa umejua mbivu au mbichi za kupoata leseni
5. Leseni ya biashara Wizara Ya Viwanda, Biashara Na Uwekezaji
- Utaomba leseni online ktk website Tanzania National Business Portal
- Ada yake TZS. 600,000
- Ambatanisha vielelzo kama mwongozo ukuelekezavyo then unapata leseni kwa haraka na kwa wepesi kabisa
FAIDA ZA UTARATIBU HUU MPYA
- Unasaidia kulinda maslahi ya pande zote mbili kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za JMT za masuala ya biashara za mikopo
- Unatoa ajira kwa sababu hakutakuwa na ofisi za mifukoni kwani
- Zitasaidia kudhiti riba za juu sana ambazo kiuhalisia zinamuumiza sana mkopaji
- Kichocheo cha kupunguza umasikini katika jamii kwa mikopo wezeshi hii ya riba na fuu nay a muda mfupi mfupi
- Umeweka wazi kabisa masuala yote juu ya haki, wajibu na nafasi ya mkopaji na mkopeshaji N.k
HASARA ZA UTARATIBU HUU MPYA
- Mfumo una gharama kuanzia kufanya maombi hadi kupata leseni
- Wawekezaji wenye mitaji midogo chini ya mil 20 hawana nafasi
Kwa haya machache narudisha Mjadala huu uwanjani kwani naamini kuna members wajuzi na wenye uzoefu mkubwa zaidi katika biashara hii ya mikopo karibuni sana kwa mjadala mpana zaidi ikiwa katika msingi wa maswali, maoni na kuongezea au kurekebisha sehemu zenye mapungufu