Biashara ya Kutoa Mikopo (Microfinance): Hatua, Taratibu za Kufuata na Ushauri wa Uendeshaji

Biashara ya Kutoa Mikopo (Microfinance): Hatua, Taratibu za Kufuata na Ushauri wa Uendeshaji

mfumo wa kukopesha hususan kwa nchi zetu changamoto kubwa ni watu kutokulipa ukizingatia wahitaji wengi hawana collateral hence hata wakishindwa kulipa utawafanya nini (labda utumie ubabe na njia zisizo za kisheria)..., watu wanaofaidika na issue kama hizi bila tatizo ni kina SONGESHA..., wanakukopa pesa ikiingia wanachukua chao na ni vigumu mtu kukimbia deni sababu simu yako na namba yako ni asset muhimu sana
 
mfumo wa kukopesha hususan kwa nchi zetu changamoto kubwa ni watu kutokulipa ukizingatia wahitaji wengi hawana collateral hence hata wakishindwa kulipa utawafanya nini (labda utumie ubabe na njia zisizo za kisheria)..., watu wanaofaidika na issue kama hizi bila tatizo ni kina SONGESHA. Wanakukopa pesa ikiingia wanachukua chao na ni vigumu mtu kukimbia deni sababu simu yako na namba yako ni asset muhimu sana
Jambo kubwa katika biashara hii lipo katika utekelezaji. Ukiangalia msingi mkuu wa biashara hii ni SERA YA MIKOPO. Sera nyingi za mikopo hazikidhi vigezo vya uendeshaji wa hii biashara matokeo yake ndiyo hilo unalosema hapo juu.

Hii ina maana ya kwamba mchakato mzima kuanzia mteja kuomba mkopo, kukagua biashara au kazi anayofanya, vikao vya mkopo, uandikishaji wa dhamana, kiwango cha marejesho na hadi "recovery" iwapo mkopo haulipwi hazifuatwi. Kwa mantiki hy bhasi utaona mchakato mzima toka chini u akuwa umeshakosewa hvy tarajia changamoto kubwa ktk kulipwa laah uwe wasubiri uaminifu na uamuzi tu wa mdai kulipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fafanua swali lako mkuu ukiwa na maana hizi?
1. Umeandika tu neno Finance ktk jina la biashara lkn hautafanya biashara ya masula ya fedha? Au
2. Umeandika neno Finance lkn baadae utafanya biashara inahusisha fedha ila kwa sasa unafanya biashara nyinginezo lkn zimejumuishwa ktk biashara ulizochagua wakati wa usajili?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikua namaanisha kusajili jina la kampuni mfano badala ya kuandika MRX microfinance Ltd mm niandike MRX finance Ltd halafu nijihusishe na biashara ya kukopesha pesa je itaruhusiwa? Maana nimeona huo muongozo wako unajumuisha maneno matatu tu kama microfinance, financial service na microcredit ndo swali langu lililenga hapo? Au nn tofaut kati ya meneno hapo juu dhidi ya finance?
 
Habari za leo wanajukwaa,

UJUMBE MAHUSUSI: TUCHUKUE TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA, NI WAJIBU WETU SOTE KUKABILIANA NA JANGA HILI

Utangulizi
Rejea katika Makala yetu ya awali tuliyoiwasilisha mnamo tarehe 09 Agosti, 2018 ilikuwa bado suala la mabadiliko makubwa yaliyofanywa na serikali kurasimishwa:

MWONGOZO: Masharti na taratibu za kupata leseni ya kutoa mikopo kwa kutumia mtaji binafsi

Sasa kutokana na Mabadiliko hayo ya kisheria na pia rejea Notisi ya Benki Kuu ya Tanzania ya Desemba 2019 tumeona ni vema kuiboresha mada kwa kuileta kama sehemu ya pili ya maboresho ili wadau kujadili kwa upana wake na pia kuona faida na hasara zake kwa mkopeshaji na mkopaji.

Kwa Muhtasari
Biashara ya utoaji mikopo imezidi kushika kasi na kushamiri kwa kasi sana. Kundi hili linalojadiliwa hapa watoaji mikopo binafsi na makampuni binafsi yanayotoa mikopo kwa mitaji yao binafsi na hayaruhusiwi kuchukua na kuhifadhi pesa za wateja wao ie Non-Deposit taking ambazo zipo katika kundi no 2 (Tier 2)

Maboresho katika Usajili

Kwa mujibu wa sheria kampuni inayotaka kufanya biashara hii ya utoaji mikopo MEMART yake iwe na sifa hizi:
1. Jina la kampuni lazima liwe na neo “MICROCREDIT au MICROFINANCE au FINANCIAL SERVICES”
2. Biashara zitakazofanywa na kampuni hii lazima ziwe zenye mlengo (objects) wa biashara ya fedha tu na si kwa kuchanganya na aina nyingine za biashara
3. Mtaji wa kampuni ni lazima uwe kuanzia milioni 20

Pia kampuni hii inatakiwa kuwa na yafuatayo:
1. Ofisi ambapo wakaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania wanaweza kuja kukagua muda wowote ikiwa kabla au baada ya kupata leseni
2. Lazima uweke bango la kuonyesha ni kampuni ya mikopo
3. Uwe na mifumo ya wazi ya uendeshaji wa kampuni husika pamoja na mawasiliano
4. Wakurugenzi wa kampuni wawe na elimu ya ufahamu wa biashara hii hata kama sio wasimamizi wakuu
5. Lazima kampuni ielezee namna ilivyoupata huo mtaji ambao unatokana na mchango wa wanahisa ikiwa kila mmoja ataelezea alipata vipi katika zile hisa alizolipia
6. Kuwe na uongozi kamili ie bodi ya wakurugenzi, CEO et al

Kwa mtu binafsi anaetaka kufanya biashara hii nae atalazimika kufanya haya:
1. Kusajili jina la biashara ambalo litakuwa na sifa kama zilivyoonyeshwa hapo juu katika kapuni
2. Mtaji ni kuanzia milioni 20 ambao anapaswa kuuelezea wazi kaupataje mtaji huu
3. Atawasilisha ripoti ya madeni ie Credit Report from Credit Reference Bureau
4. Masuala ya kuwa na ofisi, mifumo rasmi ya uendeshaji biashara nk kama ilivyo katika kampuni nae atakuwa nayo pia isipokuwa uongozi ie Board of Directors hatakuwa na hii

Akikamilisha vielelezo hivi na vikiwa sahihi basi hatua ya pili itafuata

2. Kupata TIN na Cheti cha Ulipaji kodi ie Certificate of Tax Clearance
  • Hatua hii ya pili itafanywa upande wa Mamlaka ya Mapato ie TRA ambapo atalipa kodi stahiki zote kama vile kodi ya mapato, kodi ya zuio na ushuru wa stempu kwa mkataba wa pango. Kisha atapewa TIN ya kampuni au Mtu binafsi ambayo watakuwa wameongezea na jina la biashara na Cheti cha Mlipa kodi kitakuwa “addressed” kwenda BOT itategemea upo mkoa gani kwn zipo ofisi zao za kanda pia
3. Kuandaa Sera ya Mikopo na Wasifu wa kampuni na kujaza Questionnaires
  • Kampuni au mtu binafsi utaandaa sera ya mikopo inayokidhi vigezo vya uendeshaji wa biashara hii ya mikopo kwa kuweka mambo yote muhimu kama vile Muundo wa uongozi wa kampuni, aina za huduma za mikopo utoazo, riba, taratibu za kutoa mikopo, taratibu za urejeshaji mikopo, riba, vikao vya upirishaji mikopo, taratibu za kukusanya mikopo chefu chefu, risks, ufutaji wa mikopo chefu chefu nk nk. Hii ni muhimu sana kwa sbabu ndiyo dira na mwongozo mzima wa naman gani utafanya hii biashara
  • Vile vile kutatakiwa kuandaa wasifu wa kampuni, wakurugenzi na kila mtu ambae atahusika katika kampuni husika au kama mtu binafsi pia lazima uandae ikiwa pamoja na kuambatanisha vyeti vyako vya elimu na sifa nyingine za ziada
4. Maombi ya leseni (kibali) BOT
  • Baada ya kukamilisha vielelezo vyote kampuni au mtu binafsia
  • Ataandika barua ya kumchagua mtu maalum wa kufuatilia suala hili la leseni
  • Atalipa TZS. 500,000 kampuni au TZS. 300,000 ambayo ni pesa isiyorudihwa hata kama maombi yako yamekataliwa hairudi.
  • Ndani ya siku 60 utakuwa umejua mbivu au mbichi za kupoata leseni
5. Leseni ya biashara Wizara Ya Viwanda, Biashara Na Uwekezaji
  • Utaomba leseni online ktk website Tanzania National Business Portal
  • Ada yake TZS. 600,000
  • Ambatanisha vielelzo kama mwongozo ukuelekezavyo then unapata leseni kwa haraka na kwa wepesi kabisa
FAIDA ZA UTARATIBU HUU MPYA
  1. Unasaidia kulinda maslahi ya pande zote mbili kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za JMT za masuala ya biashara za mikopo
  2. Unatoa ajira kwa sababu hakutakuwa na ofisi za mifukoni kwani
  3. Zitasaidia kudhiti riba za juu sana ambazo kiuhalisia zinamuumiza sana mkopaji
  4. Kichocheo cha kupunguza umasikini katika jamii kwa mikopo wezeshi hii ya riba na fuu nay a muda mfupi mfupi
  5. Umeweka wazi kabisa masuala yote juu ya haki, wajibu na nafasi ya mkopaji na mkopeshaji N.k
HASARA ZA UTARATIBU HUU MPYA
  1. Mfumo una gharama kuanzia kufanya maombi hadi kupata leseni
  2. Wawekezaji wenye mitaji midogo chini ya mil 20 hawana nafasi
Kwa haya machache narudisha Mjadala huu uwanjani kwani naamini kuna members wajuzi na wenye uzoefu mkubwa zaidi katika biashara hii ya mikopo karibuni sana kwa mjadala mpana zaidi ikiwa katika msingi wa maswali, maoni na kuongezea au kurekebisha sehemu zenye mapungufu
Nauliza Je hiyo Million 20 inakuwa fixed deposit? Maana najiuliza si mnaweza mkachanga mkaweka then after some time ukishasajili unaweza ukaitoa?
 
Hapana sio fixed. Kuna ukaguzi wa mara kwa mara na tambua kwa sasa unatakiwa kuwa na mfumo wa uendeshaji wa biashara hii na sio kila kitu kinamalizikia ktk cm yako tu!
Nauliza Je hiyo Million 20 inakuwa fixed deposit? Maana najiuliza si mnaweza mkachanga mkaweka then after some time ukishasajili unaweza ukaitoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inakubalika kuweka mojawapo ya neno hili : finance, credit, microcredit, microfinance au financial services
Nilikua namaanisha kusajili jina la kampuni mfano badala ya kuandika MRX microfinance Ltd mm niandike MRX finance Ltd halafu nijihusishe na biashara ya kukopesha pesa je itaruhusiwa? Maana nimeona huo muongozo wako unajumuisha maneno matatu tu kama microfinance, financial service na microcredit ndo swali langu lililenga hapo? Au nn tofaut kati ya meneno hapo juu dhidi ya finance?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kama mkopaji hatarejesha mkopo wake sheria inaruhusu kushikiria na kupiga mnada dhamana zake?
Pia napenda kujua riba pendekezwa kwa ajiri ya hizi Microcredit?
 
Hapana sio fixed
Kuna ukaguzi wa mara kwa mara na tambua kwa sasa unatakiwa kuwa na mfumo wa uendeshaji wa biashara hii na sio kila kitu kinamalizikia ktk cm yako tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mteja aliyeshindwa kurejesha utartibu wa upndishwaji riba kwenye mkopo wake upoje? na hufanyika kwa muda gani kabla ya kumpeleka ktk vyombo stahiki? Je, ni sahihi kumpndishia riba kwa miezi nane mfurulizo? Tuendelee kuelimishaan
 
Vipi kama mkopaji hatarejesha mkopo wake sheria inaruhusu kushikiria na kupiga mnada dhamana zake?

Pia napenda kujua riba pendekezwa kwa ajiri ya hizi Microcredit?
Kwa kuzingatia sheria ya mikopo kifungu cha 51 sehemu ya 56 Ukusanyaji wa madeni (1), ( 2) ukijumuisha na sera ya mikopo kuna taratibu zimewekwa ktk kumdai mdeni wako. Miongoni mwa taratibu ni

i. Kumpa notisi ya siku 14 mdeni wako juu ya kulipa deni baada ya hapo taratibu za kukusanya deni zitachukua mkondo wake
ii. Usimtishe, mtukane, kumwambia maneno mabaya, lugha chafu et al hadi no ivi.

Sasa basi baada ya taratibu hizo kushindika utatakiwa kufuata sheria kukamata mali zake na ukifanikiwa ina maana utatangaza mnada wa hadhara juu ya uuzaji wa mali ambazo aliweka dhamana na sio kuziuza au kuchukua mwenyewe kinyemela

Riba ni ile iwe reasonable

(Wanasheria na debt collectors and auctioners twaomba waje kufafanua vema zaidi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa mteja aliyeshindwa kurejesha utartibu wa upndishwaji riba kwenye mkopo wake upoje? na hufanyika kwa muda gani kabla ya kumpeleka ktk vyombo stahiki? je ni sahihi kumpndishia riba kwa miezi nane mfurulizo? tuendelee kuelimishaan
Kwanza tukirejea ktk kifungu cha sheria ya ukusanyaji wa madeni kama nilivyonukuu hapo uzi wa juu sehemu ya 56 (3 na 4) imeweka wazi kuwa:

i. Kampuni ya mikopo haitaruhusiwa kukusanya riba, gharama yyt ya ziada ikiwa hakukuwa na makubaliano kati ya mkopaji na mkopeshaji wakati wa kuingia mkataba wa kukopana pesa.

ii. Kampuni ya mikopo itaihusisha kampn ya kukusany madeni iliyosajiliwa na yenye leseni mahususi ya ukusanyaji madeni ambao kampuni hii ya ukisanyaji madeni itafanya kazi hy kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za ukusanyaji madeni.

Kwa kifupi hakuna kutumia ubabe kudai madeni bali fuata sheria tu kupata haki yako

Nyongeza
Unaweza pitia The Microfinance act (cap. 407), Regulations, soma kurasa na 25 na 26 Debt collection or recovery section 56 (1) hadi (4)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hii sheria imezungumziaje swala la riba...taasisi inaweza ikajipangia na kumtoza mteja riba yoyote bila kubanwa na sheria hii?
Haijawa wazi sana ila kuna viwango vipo kwa kutegemea na asili ya huduma inayopata mkopo. Utaona ipo kati ya 10% hadi maximum 25% (substandard) kwa mwezi rejea pg 20 na 21 classification and provisions for loans, Regulations.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafasi ya Bank kuu ya kuregulate viwango vya riba kwa taasisi za kifedha inakuaje. Tunatambua bank kuu iko responsible nakupangilia viwango vya riba kwa bank zote za biashara. Kama sijakosea, miezi michache iliyopita bank kuu ilipunguza riba moka 17%.

Je, utararibu huu hauzihusu micro finances?
 
Kwanza tukirejea ktk kifungu cha sheria ya ukusanyaji wa madeni kama nilivyonukuu hapo uzi wa juu sehemu ya 56 (3 na 4) imeweka wazi kuwa:

i. Kampn ya mikopo haitaruhusiwa kukusanya riba, gharama yyt ya ziada ikiwa hakukuwa na makubaliano kati ya mkopaji na mkopeshaji wakati wa kuingia mkataba wa kukopana pesa.

ii. Kampuni ya mikopo itaihusisha kampn ya kukusany madeni iliyosajiliwa na yenye leseni mahususi ya ukusanyaji madeni ambao kampuni hii ya ukisanyaji madeni itafanya kazi hy kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za ukusanyaji madeni.

Kwa kifupi hakuna kutumia ubabe kudai madeni bali fuata sheria tu kupata haki yako

Nyongeza
Unaweza pitia The Microfinance act (cap. 407), Regulations, soma kurasa na 25 na 26 Debt collection or recovery section 56 (1) hadi (4)

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu shukrsni kwa elimu hii
 
Back
Top Bottom