Kwa mtaji huo unaweza kuanza kibishi bishi na ukafanikiwa vyema tu
Gas zimepanda ila bado haisababishi ushindwe kuanza kufanya mtaji
ulio nao unatosha kuanza,ila achana na mambo za vibali mzee we komaa
BEI ZA GAS ZIKO KAMA IFUATAVYO
Mihan/Taifa
6KG 31,500 (gas + cylinder)
15KG 67,000 (gas + cylinder)
ORYX
6KG 40,000 (gas + cylinder)
15KG 85,000 (gas + cylinder)
MANJIS
6KG 38,000 (gas + cylinder)
15KG 65,000 (gas + cylinder)
O GAS
6KG 40,000 (gas + cylinder)
15KG 70,000 (gas + cylinder)
Hizo ndio gas ambazo zina mzunguko kwa wateja kwa sasa
kwa mtaji wako huo una weza ukaanza na Ndogo mbili kwa
kila kampuni utapata 219,000 na ukachukua 15KG 1 kwa kila kampuni
utapata 217,000 ukipga total hapo unapata 436,000 katika ile 500,000 yako
una balance ya 64,000 hii sasa kanunulie vifaaa vya gas kama Trivert na Burner
Vifaa bei Trivert 1 = 4000 Burner 1= 3000
Nunua Trivert 5 = 20,000
Nunua Burner 10 = 30,000
total 50,000, hapo chenchi imebaki 14,000 hiii 14k iliyobaki nadhani tunasema imebaki ki theory ila ki practical sidhan kama itakua imebaki maana nauli itakua humo,maji njiani,vocha kidogo.
so ki practical naona mfukoni utakua umebaki na jero au buku au sh 200 hv kama sio sh 100, Mtaji wako utakua umeishia hapo, kifuatacho ni wewe kupga biashara.
Najua sehemu ya biashara unayo mwanzo utakua unatoa na kuingiza hii ndio maana halisi ya mwanzo Mgumu.
Sijaweka bei za kubadlisha kwa wateja wa majumbani maana kila mtaa una bei zake,nadhani kuna kitu umepata mkuu MSHUKURU
Copa Cabana kwa kuni tag maana nisingeuona uzi wako.
Kwa mwanzo huu utatoboa, nikupe tu siri 1 mkuuu, Usikatshwe tamaa na boya yeyote GAS ni TAMUU nikikwambia TAMUU namaanisha Anza kuuza kwa ugumu na shida hvyo hvyo Baada ya miaka yako mi 5 kurudi home na faida 300k per day kwenye gas tu ni jambo la kawaida SANAAAAA tena huyo n mfanyabiashara mdogo.
Ukitunisha mtaji 500K PER DAY UNAGUSA TU gas tamu baba tamu sana anza na usikatshwe tamaa japo mwanzo huu wakati unaanza utapgwa pgwa sana bei na wauzaji gas maana sio waaminifu ila usijali hata sisi wenzako tuliumizwa hvyo hvyo mpk kufikia hatua ya kwenda fata Lori lako depo si safari ndogo,ilikua safari ya kupanda milima na mabonde.Komaaa utatusua.