Biashara ya kuuza gesi za kupikia

Biashara ya kuuza gesi za kupikia

Madini yapo humu humu boss uliza maswali kuptia thread za kwenye jukwaa la biashara Utapata majibu stahiki utakayoshiba na akili yako.
Mimi nataka kufahamu,bei ya jumla na bei ya rejareja ili nijue faida Kwa Kila mtungi.
 
Asee una vitega uchumi halafu wife hakua na biashara unafeli wapi bwasheee,unakubalije bi mkubwa Kadi ya ATM ikose M kadhaaa,ukidondoka paaaa Hatoteseka yeye tu ila na wanao Pia.

Mfungulie Boss usiuweke tena fanya chap chap,hawa wake zetu waliotuletea viumbe ni wakuwawekea mazingira ya hela hadi wazizoeee wakitaka kwenda pelekea viben ten shauri zao,nachojua hawezi kubali mwanangu ateseke.
Umeongea pointi sana!
 
Mk

Mkuu CONTROLA Naomba kupatiwa Layout ya ndani ya Duka la Gas,yaan mpangilio wa mitungi,kabati,na shelves kama zipo...ili kuleta muonekano wa kisasa.
IMG_20230422_123510_062.jpg
 
Mkuu CONTROLA asante kwa kunirudia japo kwa kuchelewa sana. Hii biashara niliianza lakini kwa small scale,niliweka mitungi ya gas na uwakala wa fedha. Mitungi ya gas imekuwa na faida kidogo sana kiasi kwamba imebidi nifanye evolution ya biashara kwa kuongeza nguo za ndani za wadada khanga na vitenge. Kwa sasa pesa ya gas inatumika tu kupata chakula cha dada w dukani. Mtungi mmoja una faida kiduchu,kupata pesa ndefu ni mpaka uuze mitungi mingi sana. Biashara ipo Mlandizi kibaha.
Kitu kingine nilikuja gundua hii biashara gas haina bei,kila mtu anakutajia bei yake ya jumla.Ilifika hatua nilikuwa nafanya window shopping ya bei kwa mawakala naenda ja karatasi naandika,lakini siku ya kuagiza mzigo mtu ananiruka anasema "wewe hiyo bei umetoa wapi mimi siuzi hivyo"?
 
Mkuu CONTROLA asante kwa kunirudia japo kwa kuchelewa sana. Hii biashara niliianza lakini kwa small scale,niliweka mitungi ya gas na uwakala wa fedha. Mitungi ya gas imekuwa na faida kidogo sana kiasi kwamba imebidi nifanye evolution ya biashara kwa kuongeza nguo za ndani za wadada khanga na vitenge. Kwa sasa pesa ya gas inatumika tu kupata chakula cha dada w dukani. Mtungi mmoja una faida kiduchu,kupata pesa ndefu ni mpaka uuze mitungi mingi sana. Biashara ipo Mlandizi kibaha.
Kitu kingine nilikuja gundua hii biashara gas haina bei,kila mtu anakutajia bei yake ya jumla.Ilifika hatua nilikuwa nafanya window shopping ya bei kwa mawakala naenda ja karatasi naandika,lakini siku ya kuagiza mzigo mtu ananiruka anasema "wewe hiyo bei umetoa wapi mimi siuzi hivyo"?
Uko sahihi mkuu,Gas ni biashara yenye pesa lakini Kama tu utawekeza kwa Ukubwa sana.

Binafsi nimechanganya biashara ila nguvu nyingi nimeziangushia kwenye Gas, Ili ufurahie hii biashara lazima mtaji uwe umeeleweka.

Gas ni biashara watu wanajiamulia tu bei,shida inayopelekea kuathiriwa zaidi mtu kama wewe mwenye mtaji mdogo au wa kati.

Komaa na kinachotoka zaidi wala usihangaike kuchoma pesa sehemu inarudisha pesa kwa taratbu.

Ushauri wangu ni kwamba, Ukija kupata hela huko mbeleni Not Less of 50M rudi tena kwenye GAS ingia mzima mzima, Utanishukuru ukifika miaka 50-60 hv...

Ukijaga fikiria tu biashara ya kufanya ukizishika Rudi upya kwenye GAS,usiache mbachao mwa msala upitao.
 
Huwezi kwenda depo (kiwandani) kule wanaenda mawakala Wakuu TU.

Mtaji wa kuwa wakala Mkuu sio wa kuanza kudiscuss hapa, Fanya tu biashara ya gas kwa level hyo hyo uliyopo Mkuu.

Bado faida utaiona vyema wala hutopata stress,Komaa anza na ulichonacho.

Cha muhimu Kuwa makini,wauza gas namaanisha wasambazaji madereva wanaosambaza gas kwa wateja Huwa wanaongeza sana vi buku buku na vijero jero...

Usije ukatajiwa bei yakununua ni 19,000 ukaona ndogo ukawa unatoa hela, wakat huo wenzio mahali wananunua kwa 17,000...

Gas ni biashara hutakiwi kuagiza kwa mtu 1 unatakiwa akili iwe inafanya utafiti kila iitwapo leo, Maana ina madalali wengi sanaa kuanzia kwenye gas yenyewe mpk kwenye Vifaa vyake.

ili uone faida vyema zuia upoteaji wa vile vijero jero na vibuku buku wanavyokuongezea wauzaji wasambazaji.

Ukiuza Gas 22,000

Jirani ako akiuza gas 21,500 nakuhakikishia wewe utamlaumu sana Mungu kwann wateja hawakuoni...

Ofa INAENDELEA upande huu HUKU

View attachment 2176534
Kuwa wakala mkuu mtaji kiasi gani?
 
Kuwa wakala mkuu mtaji kiasi gani?
Unaweza ukawa na Pesa 1B na usipewe uwakala.

Sio pesa tu huangaliwa unapotaka kuomba au kupewa uwakala mkuu.

Wakala mkuu maana yake unapewa eneo flani ulihudumie, mfano hapa DAR kuna Wilaya ya UBUNGO,TEMEKE,ILALA nk.

Ukiwa wakala mkuu unaomba halafu wao wanakupa WILAYA uihudumie.

Sasa kuhudumia wilaya nzima ni lazima uwe na vithibitisho vinavyoonekana not papers.

Uwe na MAGARI ya kusambaza mzigo wilaya nzima ambapo si chini ya GARI 10.

Uwe na GARI la kufatia Mzigo Kiwandani/Depo ambalo ni lako na wamelisajili maana ni hilo tu litaruhusiwa ingia ndani.

Gari la Kubeba Mzigo wa Gas Sio chini ya 500 ujue hapa tunaongelea FUSO.

Ukishakua na vitendea kazi MAGARI + WATU (kampuni) sasa unaweza onyesha SALIO lako bank ambapo 1B sio mbaya kuwa impress wakupe not Less. utawaonyesha Live wataona watajiridhisha taarifa zako za PESA.

UWAKALA mkuu si lelemama ukisikia mtu ni wakala Mkuu, Huyo sio mwenzako.

Hapo unaongea na mtu mwenye capital isiyopungua hata 3B na ana channel nyingine kibaooo.

So jibu ni kwamba hata uwe na 5B kama huna vitendea kazi hupewi uwakala mkuu.
 
Amen Kubwa ndugu yangu kiboboso nautamani sana utajiri, naamini kwa baraka hizo alie Juu atanipa tu maana ndio shauku yangu siku 1 kuketi na wafalme wa Dunia hii.

Kusaidia wengi na wanaopta ktk mazingira magumu,najua This word is a better place for everyone, and i will make it real.

if not everyone but atleast anyone around me, To Put a smile kwenye kila sura ya kiumbe kitakachonifahamu CONTROLA .
Hii comment ni ya mwaka 2022, Mimi nafahidikia nayo Leo kwa kuipitia hapa na kuvuna maarifa. Thank You brother
 
Biashara ikikubali kakate kibali cha fire 45,000 tu japo vibali vinatoka kwa sqm so idadi ya mitungi yako ndio ita determine wewe kibali chako kiwe cha sh ngapi.

Mwanzo nilifanyaga mafekeche nikawa nimekata kbali kdg tu ila mitungi kibaooo,baadae roho ikanisuta nikaona nikija kuotewa ntaumia basi nimekubali ongeza dau kibali bei ya juu kdg,ila wewe cha 45k ndio size yako.

Kingine Fire extinguisher kwisha habari ukshapata certificate ya fire na hyo fire extinguisher umemaliza Hao fire inpectors wakipta eneo la ofisi yako watapta kwa mbaliii kama hawakuoni.

Kupata Kibali cha Fire ni LAZIMA uwe na leseni ya biashara plus TIN number,imeisha hiyo mkuu.Kapambane.
mkuu nimejifunza jambo kutoka kwako,mimi nataka kuanza kwa mtaji wa milioni 1
 
Back
Top Bottom