Biashara ya kuuza gesi za kupikia

Madini yapo humu humu boss uliza maswali kuptia thread za kwenye jukwaa la biashara Utapata majibu stahiki utakayoshiba na akili yako.
Mimi nataka kufahamu,bei ya jumla na bei ya rejareja ili nijue faida Kwa Kila mtungi.
 
Umeongea pointi sana!
 
Mkuu CONTROLA asante kwa kunirudia japo kwa kuchelewa sana. Hii biashara niliianza lakini kwa small scale,niliweka mitungi ya gas na uwakala wa fedha. Mitungi ya gas imekuwa na faida kidogo sana kiasi kwamba imebidi nifanye evolution ya biashara kwa kuongeza nguo za ndani za wadada khanga na vitenge. Kwa sasa pesa ya gas inatumika tu kupata chakula cha dada w dukani. Mtungi mmoja una faida kiduchu,kupata pesa ndefu ni mpaka uuze mitungi mingi sana. Biashara ipo Mlandizi kibaha.
Kitu kingine nilikuja gundua hii biashara gas haina bei,kila mtu anakutajia bei yake ya jumla.Ilifika hatua nilikuwa nafanya window shopping ya bei kwa mawakala naenda ja karatasi naandika,lakini siku ya kuagiza mzigo mtu ananiruka anasema "wewe hiyo bei umetoa wapi mimi siuzi hivyo"?
 
Uko sahihi mkuu,Gas ni biashara yenye pesa lakini Kama tu utawekeza kwa Ukubwa sana.

Binafsi nimechanganya biashara ila nguvu nyingi nimeziangushia kwenye Gas, Ili ufurahie hii biashara lazima mtaji uwe umeeleweka.

Gas ni biashara watu wanajiamulia tu bei,shida inayopelekea kuathiriwa zaidi mtu kama wewe mwenye mtaji mdogo au wa kati.

Komaa na kinachotoka zaidi wala usihangaike kuchoma pesa sehemu inarudisha pesa kwa taratbu.

Ushauri wangu ni kwamba, Ukija kupata hela huko mbeleni Not Less of 50M rudi tena kwenye GAS ingia mzima mzima, Utanishukuru ukifika miaka 50-60 hv...

Ukijaga fikiria tu biashara ya kufanya ukizishika Rudi upya kwenye GAS,usiache mbachao mwa msala upitao.
 
Kuwa wakala mkuu mtaji kiasi gani?
 
Kuwa wakala mkuu mtaji kiasi gani?
Unaweza ukawa na Pesa 1B na usipewe uwakala.

Sio pesa tu huangaliwa unapotaka kuomba au kupewa uwakala mkuu.

Wakala mkuu maana yake unapewa eneo flani ulihudumie, mfano hapa DAR kuna Wilaya ya UBUNGO,TEMEKE,ILALA nk.

Ukiwa wakala mkuu unaomba halafu wao wanakupa WILAYA uihudumie.

Sasa kuhudumia wilaya nzima ni lazima uwe na vithibitisho vinavyoonekana not papers.

Uwe na MAGARI ya kusambaza mzigo wilaya nzima ambapo si chini ya GARI 10.

Uwe na GARI la kufatia Mzigo Kiwandani/Depo ambalo ni lako na wamelisajili maana ni hilo tu litaruhusiwa ingia ndani.

Gari la Kubeba Mzigo wa Gas Sio chini ya 500 ujue hapa tunaongelea FUSO.

Ukishakua na vitendea kazi MAGARI + WATU (kampuni) sasa unaweza onyesha SALIO lako bank ambapo 1B sio mbaya kuwa impress wakupe not Less. utawaonyesha Live wataona watajiridhisha taarifa zako za PESA.

UWAKALA mkuu si lelemama ukisikia mtu ni wakala Mkuu, Huyo sio mwenzako.

Hapo unaongea na mtu mwenye capital isiyopungua hata 3B na ana channel nyingine kibaooo.

So jibu ni kwamba hata uwe na 5B kama huna vitendea kazi hupewi uwakala mkuu.
 
Hii comment ni ya mwaka 2022, Mimi nafahidikia nayo Leo kwa kuipitia hapa na kuvuna maarifa. Thank You brother
 
mkuu nimejifunza jambo kutoka kwako,mimi nataka kuanza kwa mtaji wa milioni 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…