Biashara ya kuuza kahawa

kitoto wa vitoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
375
Reaction score
410
Poleni na hongeren kwa ubize wa kutwa nzima ya Leo,

Ni matumaini yangu tunaebdelea vizuri tukiwa na afya njema, kwa wenye changamoto polen na mungu atawasaidia.

Ndugu zangu nimepata aidia moja ya biashara ya kuuza kahawa:

WAZO LANGU LIKO HIVI,
nifanye research kwenye bar kubwa zilizochangamka na zilizo kwenye standard nzuri na ambazoziko bize muda mwingine hasa weekend n haziuzi kahawa.

Niongee na uongozi wanipangishie sehemu ndogo ndani ya hiyo bar nifanyie marekebisho ninavyotaka Mimi nilete mashine ya kahawa (espresso machine).

Niiweke na vifaa vinginevyo
  • Niwe nauza kahawa aina zote, milkshake na ice cream, smoothie na juis fresh, hot drinks
  • Vifaa vikubwa ni ni espresso machine na friza ndogo,

Je mnaonaje wazo LANGU?

Naombeni mawazo, ushauri na maboresho kwenye wazo LANGU,
 
Location ya Bar ipo wapi mfano? Unajua kuna Kahawa, Gahawa, na Coffee.

We unataka kuuza Coffee.

Sasa ukibugi location utamuuzia nani? Sisi wakazi wa Temeke tunanunua zile za mia mia kikombe. Sasa wewe utaleta za buku 5?

Cheza na location.
 
Kunipeleka baa ndo umeharibu. Kwa nn usitafte nafS jNICC
 
Location ya Bar ipo wapi mfano? Unajua kuna Kahawa, Gahawa, na Coffee.

We unataka kuuza Coffee.

Sasa ukibugi location utamuuzia nani? Sisi wakazi wa Temeke tunanunua zile za mia mia kikombe. Sasa wewe utaleta za buku 5?

Cheza na location.
Ndio mkuu namaanisha coffee
Kuhusu locations nimelenga sehemu nyingi zilizo na movement angalau ya wageni /watalii na watu wa hadhi Fulani kama wanaofanya kwa ofisi kubwa na wafanyabiashara pia
 
Wazo zuri Wale local tu wanapiga hela kile kikombe kidogo kinauzwa tsh 100 alaf kahawa inanyweka masaa 24 hata wakati wa jua kali watu wanakunywa kuna wauza kahawa wamejenga kabisa
 
Ndio mkuu namaanisha coffee
Kuhusu locations nimelenga sehemu nyingi zilizo na movement angalau ya wageni /watalii na watu wa hadhi Fulani kama wanaofanya kwa ofisi kubwa na wafanyabiashara pia
Idea nzuri.

Coffee Shop + Wifi + Free Books & Magazine + TV zenye michezo ya kishua (F1 MotorGP Golf etc) + ...

Unaweza ongezea vitu kama iced tea, smoothies, juices, bites, etc
 
Wazo zuri Wale local tu wanapiga hela kile kikombe kidogo kinauzwa tsh 100 alaf kahawa inanyweka masaa 24 hata wakati wa jua kali watu wanakunywa kuna wauza kahawa wamejenga kabisa
Ni kweli na Wana maisha Safi sana
 
πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚ Dogo acha utani
Aise hata mimi awali nilivyosikia kuna wauza kahawa wamejenga nilikataa ila nilikuja kuthibitisha hiyo biashara inadharauliwa ila inafaida kubwa ukiwa vizuri maeneo ya mjini unauza hadi masaa 24, kikombe kinauza tsh 100 alaf ni kikombe kidogo sana pact 1 ya kahawa inachemsha sufuria kubwa kinoma
 
Wengi wanafamilia ,
 
Ni biashara nzuri. Kuna jamaa namfahamu, Rwanda lakini, alianza namna hii, na biashara yake iko city center Kigali. Sasa amefungua chain yake mwenyewe nadhani. Ila kule wanywaji kahawa ni wengi, I think, kuliko huku TZ. But biashara hii nzuri sana na ukiweza kupata location itakayowanasa foreigners nayo itakuwa poa zaidi. Places like Arusha yenye cool weather na lots of foreigners ni poa sana. Kuweka hii biashara hata kwenye big shopping malls pia poa au mahotelini Kila la kheri. Ila wazo zuri sana hili. Imenikumbusha Mug &Bean coffee house huko down South
 
Asante sana kwa ushauri kaka
 
Ushanipa wazo
Ushanipa wazo la biashara kesho kutwa utanikuta mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…