Biashara ya kuuza maziwa fresh na mgando kwa Dar es Salaam

Inategemea unataka kufanya kwa ukubwa gani.

1.Kuna wale wenye biashara ya miguu 2 wanapakia vidumu vya lita tano tano wanakuwa na kikombe cha nusu lita na robo lita wanapima.

2.Kuna wanaouza kwenye vituo vya mabus hawa wanakuwa wameshapaki kwenye chupa za lita moja au nusu(hizi chupa ni zilr zilizokuwa na maji ya kiwandani mfao hill,afya &uhai)

3.Kuna ambao wananunua vifungashio special wanapaki humo na kuweka label na kusambaza.

4.Kuna wanaofungua milk point/milk bar.

5.Kuna wanaofungua kiwanda kabisa kama dae fresh and like.

Upatikanaji wake zamani nilikuwa najua wanatoa mkoani yanashukia pale Kisutu unadamka alfajr unaenda kununua kuanzia lita 20.

Sijajua kama sasa hivi bado yanapatikana.
 
Upatikanaji wake zamani nilikuwa najua wanatoa mkoani yanashukia pale kisutu unadamka alfajr unaenda kununua kuanzia lita 20.
Sijajua kama sasa hivi bado yanapatikana.
Nahtaji kufungua milk point
 
Najazia tu maneno hii biashara nzur Sana Ila ningumu kupata taarifa zake hata mm natamani Sana kufanya hii biashara katika kufatilia kwangu nimegundua sido wanaweza kunisaidia A2Z ishu ni muda tu
 
Riverside hapa wanauza jumla lita tano kwa tsh 8,500
Mtindi na fresh
Hapo River Side unatakiwa uwe makini sana na wauzaji kwani maziwa yapo ya aina nyingi kwani hata Mahindi machanga, Ngano na Mihogo unaweza kupata maziwa pia zingatia harufu hasa kwa mtindi.
Ila kwa fresh vipimo vyake vipo ni umakini tu
 
Najazia tu maneno hii biashara nzur Sana Ila ningumu kupata taarifa zake hata mm natamani Sana kufanya hii biashara katika kufatilia kwangu nimegundua sido wanaweza kunisaidia A2Z ishu ni muda tu
Sido kulikuwa na Training Usindikaji na maziwa ikiwa ni sehemu ya iliyoisha mwezi wa nane kwani mm ni mmoja wapo niliyehudhuria.
Ila usindikaji wa maziwa ni Topic kamili kwani kuna haya yafuatayo-
Uandaji maziwa yenyewe kama mtindi, Jibini na Samli
Pia nakumbuka walitoa ahadi ya kuiandaa hiyo Training yake
 
Hii biashara ya maziwa sio mbaya ni moja biashara kama zilivyo biashara nyingine.

Ila tatizo linakuja ktk ukweli wa maziwa yenyewe kwani wauza maziwa wengi wanatenda sana dhambi na siku utaingia ktk hii biashara itaiona dhambi yenyewe japokuwa ni biashara yenye faida lakini bado wauzaji kuanzia anayeuza jumla na rejareja ni wenye tamaa na wasio wakweli.

Na hawa wajumla kasumba yao kubwa ni jeuri hasa kipindi hiki ambacho maziwa ni adimu kutokana na kiangazi.
Mm ni muuzaji wa rejareja na jumla sijafikia kiwango cha kujisifia yakuwa nauza jumla kwani pale ambapo nitakapoanza kuandaa mwenyewe ndo nitakuwa tayari kumwelekeza mtu vizuri zaidi.

Mm kwa sasa ni mchuruzi bado karibu ktk hii biashara lile ambalo.na uwezo nalo nitawaelekeza kwani mm ndo miaka miwili kwenye hii kazi
 
Inategemea unataka kufanya kwa ukubwa gani.

1.Kuna wale wenye biashara ya miguu 2 wanapakia vidumu vya lita tano tano wanakuwa na kikombe cha nusu lita na robo lita wanapima.

2.Kuna wanaouza kwenye vituo vya mabus hawa wanakuwa wameshapaki kwenye chupa za lita moja au nusu(hizi chupa ni zilr zilizokuwa na maji ya kiwandani mfao hill,afya &uhai)

3.Kuna ambao wananunua vifungashio special wanapaki humo na kuweka label na kusambaza.

4.Kuna wanaofungua milk point/milk bar.

5.Kuna wanaofungua kiwanda kabisa kama dae fresh and like.

Upatikanaji wake zamani nilikuwa najua wanatoa mkoani yanashukia pale Kisutu unadamka alfajr unaenda kununua kuanzia lita 20.

Sijajua kama sasa hivi bado yanapatikana.
Sasa hivi yanapatikana kwa uhakika na Kwa wingi Kiluvya madukani.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom