GIRITA
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 4,432
- 5,864
Kama unataka kuuza reja reja....tafuta eneo la uswahilini kama Mbagala au kwingineko kwenye makazi yaliobanana...watu wanapuliana na kupakana jasho wakipishana.....kodi ka frame ka bei rahisi weka friza yako,nunua ndoo,vikombe,beseni,chujio,Tafuta machupa osha vizuri..
Nenda riverside stendi ya Mbagala,ulizia wanapouza maziwa kwa jumla,nenda hapo na ndoo zako chukua mzigo unapkutosha nenda kauze huko uswazi unaanza kupima kuanzia jero,buku,na kuendelea...usikose jiko la kuchemsha maziwa fresh kuna wadau wanapenda kunywa maziwa ya moto na vitafunwa kama maandazi,mikate,n.k hakikisha haukosi kila siku...
Cha kuzingatia uswazi watu wengi wanapenda maziwa ya mtindi(mgando) kwa sababu zao maalum ikiwa ni pamoja na kushibisha pia kuyatumia kama mboga hivyo utakuwa unapokea vibali,majagi,visufuria kwa ajili ya kuwapimia wateja wako wa mtindi.
Hapo Riverside wanauza maziwa kwa jumla na reja reja muda mzuri wa kuchukua mzigo ni asubuhi,changamoto wauzaji ni wezi wanapunguza maziwa na kuongeza maji ili wapate pesa ya kuondoka nayo nje ya mshahara hivyo unatakiwa uwe makini na Wachagga ndio wenye kazi.
Wanauza kwa lita hivyo ni pesa yako tu ndio itaamua uchukue kiasi gani..
Kama utahitaji misaada zaidi kuna jamaa yangu anaifanya hii biashara Mbagala yeye aliacha kuchukua mzigo hapo Riverside sasa hivi analetewa na wafugaji hapo hapo ofisini kwake...anaweza kukupa muongozo siku moja ukaenda kumtembelea uone anavyopiga kazi..