Biashara ya kuuza maziwa fresh na mgando kwa Dar es Salaam

Kama unataka kuuza reja reja....tafuta eneo la uswahilini kama Mbagala au kwingineko kwenye makazi yaliobanana...watu wanapuliana na kupakana jasho wakipishana.....kodi ka frame ka bei rahisi weka friza yako,nunua ndoo,vikombe,beseni,chujio,Tafuta machupa osha vizuri..

Nenda riverside stendi ya Mbagala,ulizia wanapouza maziwa kwa jumla,nenda hapo na ndoo zako chukua mzigo unapkutosha nenda kauze huko uswazi unaanza kupima kuanzia jero,buku,na kuendelea...usikose jiko la kuchemsha maziwa fresh kuna wadau wanapenda kunywa maziwa ya moto na vitafunwa kama maandazi,mikate,n.k hakikisha haukosi kila siku...

Cha kuzingatia uswazi watu wengi wanapenda maziwa ya mtindi(mgando) kwa sababu zao maalum ikiwa ni pamoja na kushibisha pia kuyatumia kama mboga hivyo utakuwa unapokea vibali,majagi,visufuria kwa ajili ya kuwapimia wateja wako wa mtindi.

Hapo Riverside wanauza maziwa kwa jumla na reja reja muda mzuri wa kuchukua mzigo ni asubuhi,changamoto wauzaji ni wezi wanapunguza maziwa na kuongeza maji ili wapate pesa ya kuondoka nayo nje ya mshahara hivyo unatakiwa uwe makini na Wachagga ndio wenye kazi.

Wanauza kwa lita hivyo ni pesa yako tu ndio itaamua uchukue kiasi gani..
Kama utahitaji misaada zaidi kuna jamaa yangu anaifanya hii biashara Mbagala yeye aliacha kuchukua mzigo hapo Riverside sasa hivi analetewa na wafugaji hapo hapo ofisini kwake...anaweza kukupa muongozo siku moja ukaenda kumtembelea uone anavyopiga kazi..
 
Cha kuzingatia uswazi watu wengi wanapenda maziwa ya mtindi(mgando) kwa sababu zao maalum ikiwa ni pamoja na kushibisha pia kuyatumia kama mboga hivyo utakuwa unapokea vibakuli,majagi,visufuria kwa ajili ya kuwapimia wateja wako wa mtindi.

Hapo Riverside wanauza maziwa kwa jumla na reja reja muda mzuri wa kuchukua mzigo ni asubuhi,changamoto wauzaji ni wezi wanapunguza maziwa na kuongeza maji ili wapate pesa ya kuondoka nayo nje ya mshahara hivyo unatakiwa uwe makini na Wachagga ndio wenye kazi..mzigo wao ni mzuri sana ukiupeleka popote inakubalika nilikuwa na namba za mdada anayeuza hapo Riverside sema zilipotea.

Wanauza kwa lita hivyo ni pesa yako tu ndio itaamua uchukue kiasi gani..
Kama utahitaji misaada zaidi kuna jamaa yangu anaifanya hii biashara Mbagala yeye aliacha kuchukua mzigo hapo Riverside sasa hivi analetewa na wafugaji hapo hapo ofisini kwake...anaweza kukupa muongozo siku moja ukaenda kumtembelea uone anavyopiga kazi....
 
Maziwa msimu wa kiangazi yanapungua (yanapatikana kwa shida)msimu wa mvua yanakuwa mengi.Nenda kwenye vituo vya ukusanyaji wa maziwa kama Kiluvya,Mlandizi,Vigwaza nk.Huko unaweza kupata,bei ni kuanzia 1600-2000 kwa Lita.
 
Nina jamaa yangu yeye anafanya biashara hiyo na inamuingizia vizuri tu faida,kwanza kabisa niende moja kwa moja kwa mfano wake.

Ipo hivi ndugu yangu mmoja yeye ana frem ndani ya jiji hili la Dar es salaam,yeye alikuwa anachukuwa mzigo kutoka njia ya kusini,huko kusini aliweka kama ofisi kubwa ya wafugaji kumuuzia maziwa kila siku usiku na mchana,yeye anajua au anatumia kifaa ya kugundua ya kuwa maziwa yamewekwa maji au laah,akishachukua maziwa kutoka kwa wafugaji basi anaya chemsha na akimaliza ana ya hifadhi kwa fridge(friza) kwa ajili ya kuto kuharibika,baada ya hapo ana yasafirisha kuja kuuza huku dar.

Nilicho jifunza toka kwake,tafuta sehemu ambapo utakuwa na uhakika wa kuuza hata little 100 kwa siku,tafuta boma nje ya dar ambapo utanunua mzigo kutoka kwa wafugaji na ku yaandaa pia hakikisha fridge (friza) lipo la uhakika na umeme pia,pia hakikisha mzigo unao nunua basi ni wenyewe yani hauja chakachuliwa,pia pata vijana waaminifu ambao watakusaidia kuandaa mzigo vizuri.

Kama ntakuwa sijakuelewesha vizuri basi karibu PM
 
Kama unataka kuuza reja reja....tafuta eneo la uswahilini kama Mbagala au kwingineko kwenye makazi yaliobanana...watu wanapuliana na kupakana jasho wakipishana.....kodi ka frame ka bei rahisi weka friza yako,nunua ndoo,vikombe,beseni,chujio,Tafuta machupa osha vizuri..

Nenda riverside stendi ya Mbagala,ulizia wanapouza maziwa kwa jumla,nenda hapo na ndoo zako chukua mzigo unapkutosha nenda kauze huko uswazi unaanza kupima kuanzia jero,buku,na kuendelea...usikose jiko la kuchemsha maziwa fresh kuna wadau wanapenda kunywa maziwa ya moto na vitafunwa kama maandazi,mikate,n.k hakikisha haukosi kila siku...

Cha kuzingatia uswazi watu wengi wanapenda maziwa ya mtindi(mgando) kwa sababu zao maalum ikiwa ni pamoja na kushibisha pia kuyatumia kama mboga hivyo utakuwa unapokea vibali,majagi,visufuria kwa ajili ya kuwapimia wateja wako wa mtindi.

Hapo Riverside wanauza maziwa kwa jumla na reja reja muda mzuri wa kuchukua mzigo ni asubuhi,changamoto wauzaji ni wezi wanapunguza maziwa na kuongeza maji ili wapate pesa ya kuondoka nayo nje ya mshahara hivyo unatakiwa uwe makini na Wachagga ndio wenye kazi.

Wanauza kwa lita hivyo ni pesa yako tu ndio itaamua uchukue kiasi gani..
Kama utahitaji misaada zaidi kuna jamaa yangu anaifanya hii biashara Mbagala yeye aliacha kuchukua mzigo hapo Riverside sasa hivi analetewa na wafugaji hapo hapo ofisini kwake...anaweza kukupa muongozo siku moja ukaenda kumtembelea uone anavyopiga kazi..
Mku ww sio mkweli kwani pale River Side hakuna Wachaga pale kwani wauzaji jumla anayeongoza pale ni 1.Sam _Msukuma
2.Nyarandu au Manyonyo_Mkurya
3.Mama Maria labda huyu ndo nitakuwa Mchaga
4_Nuhu_Mgogo
5.Mchungaji_Mpare
Hawa wengine wote ni wachuruzi kwani kwani kuwa na frem river side sio sababu
Yaani mm river ndo maskani kwangu ila sijawa na ofisi bado kwani mm ni mchuruzi wa kawaida
 
Sawa mkuu naomba uelezea biashara ya hapo inavyokuwa,mfano hao kina Sam wanauza jumla/rejareja na wananunua au wanafuga ng'ombe,bei ya maziwa kwa lita nk.
 
Habari wanajamvi naomba kupewa muongozo kuhusu biashara ya kuuza maziwa fresh na mgando kwa mji wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na

*Vifaa vinavyohtajika
*Upatikanaji
*Gharama za manunuzi
*Na eneo zuri kwa biashara hii ni ipi though Nina targeting area tayar
Kitu ninachokuambia biashara ni ngumu Sana hasa mwanzoni haijalishi utapata taarifa sahihi kwa kiasi gani kutengeneza imani kwa wateja ni swala la muda cha msingi usikate tamaa
 
Sawa mkuu naomba uelezea biashara ya hapo inavyokuwa,mfano hao kina Sam wanauza jumla)rejareja na wananunua au wanafuga ng'ombe,bei ya maziwa kwa lita nk.
Sam,Nyalandu na Nuhu hawa wote hawafugi ila wanavituo wa kukusanya kwa wafugaji.
Mama Maria yy anapata pale Kiluvya kwani yy pale ni mfanyakazi.
Bei ya Fresh kwa baadhi yao ni Lita1500
na Mtindi ni Lita 1800 mpaka 1900.
 
Kitu ninachokuambia biashara ni ngumu Sana hasa mwanzoni haijalishi utapata taarifa sahihi kwa kiasi gani kutengeneza imani kwa wateja ni swala la muda cha msingi usikate tamaa
Kikubwa ktk biashara ni uvumilivu na kujikubali pamoja na kuibrand basi.
Usiwe mchoyo kuingia ktk masoko kwa ajili ya kuwaonjesha wateja Product yako kwani maziwa hayana hasara kwani utapata hasara pale utakapo yachanganya vitu vyako vingine mfano Maji kwa wale wenye tamaa.
Uza maziwa halisi kwani utatengeneza jina.
 
Sido kulikuwa na Training Usindikaji na maziwa ikiwa ni sehemu ya iliyoisha mwezi wa nane kwani mm ni mmoja wapo niliyehudhuria.
Ila usindikaji wa maziwa ni Topic kamili kwani kuna haya yafuatayo-
Uandaji maziwa yenyewe kama mtindi, Jibini na Samli
Pia nakumbuka walitoa ahadi ya kuiandaa hiyo Training yake
Vitabu vya mafunzo walitoa watu wa Sido
Ninashida na hiyo elimu kuandaa Jibini na samli.
 
Mku ww sio mkweli kwani pale River Side hakuna Wachaga pale kwani wauzaji jumla anayeongoza pale ni 1.Sam _Msukuma
2.Nyarandu au Manyonyo_Mkurya
3.Mama Maria labda huyu ndo nitakuwa Mchaga
4_Nuhu_Mgogo
5.Mchungaji_Mpare
Hawa wengine wote ni wachuruzi kwani kwani kuwa na frem river side sio sababu
Yaani mm river ndo maskani kwangu ila sijawa na ofisi bado kwani mm ni mchuruzi wa kawaida
Kuna frame ipo nyuma ya stendi ya Mbagala wauzaji mpaka boss wote ni Wachagga...kama unamfahamu Zena ndio muuzaji hapo nilikuwa nachukua Maziwa kwake,Nje ya hiyo frame kuna mgahawa upande wa kushoto kulia kuna mafundi wa milango madirisha ya aluminium.
 
Hii biashara ya maziwa sio mbaya ni moja biashara kama zilivyo biashara nyingine.

Ila tatizo linakuja ktk ukweli wa maziwa yenyewe kwani wauza maziwa wengi wanatenda sana dhambi na siku utaingia ktk hii biashara itaiona dhambi yenyewe japokuwa ni biashara yenye faida lakini bado wauzaji kuanzia anayeuza jumla na rejareja ni wenye tamaa na wasio wakweli.

Na hawa wajumla kasumba yao kubwa ni jeuri hasa kipindi hiki ambacho maziwa ni adimu kutokana na kiangazi.
Mm ni muuzaji wa rejareja na jumla sijafikia kiwango cha kujisifia yakuwa nauza jumla kwani pale ambapo nitakapoanza kuandaa mwenyewe ndo nitakuwa tayari kumwelekeza mtu vizuri zaidi.

Mm kwa sasa ni mchuruzi bado karibu ktk hii biashara lile ambalo.na uwezo nalo nitawaelekeza kwani mm ndo miaka miwili kwenye hii kazi
Kaka nakuomba ibox tutete Jambo
 
Back
Top Bottom