Achana na hiyo biashara ndugu yangu.Nimefanya utafiti,na majuzi tu nimetoka Handeni ofisi za maliasili.Kuna maushuru hayana kichwa wala miguu.Hapo juu umepewa mambo 4.Ngoja nikuongezee 2.Utahitajika pia kulipia 1.ushuru wa halmashauri unakotoa mkaa elfu 1 kwa kila gunia,2.Ushuru kwenye mfuko wa upandaji miti,5% ya ushuru wa serikali kuu (s/k).Mfano gunia 100 utalipia ushuru wa serikali kuu 14,400*100=1,444,000.Katika hiyo,ushuru wa mfuko wa upandaji miti ni 5% ya 1,444,000.Bado gharama za kununua mzigo,usafiri,upakiaji na ushushaji ni full usumbufu.Fikiria biashara nyingine ndugu.Ahsante.