Biashara ya Kuuza Mkaa: Uzoefu, Vibali vya kuchoma, Changamoto na Ushauri

Achana na hiyo biashara ndugu yangu.Nimefanya utafiti,na majuzi tu nimetoka Handeni ofisi za maliasili.Kuna maushuru hayana kichwa wala miguu.Hapo juu umepewa mambo 4.Ngoja nikuongezee 2.Utahitajika pia kulipia 1.ushuru wa halmashauri unakotoa mkaa elfu 1 kwa kila gunia,2.Ushuru kwenye mfuko wa upandaji miti,5% ya ushuru wa serikali kuu (s/k).Mfano gunia 100 utalipia ushuru wa serikali kuu 14,400*100=1,444,000.Katika hiyo,ushuru wa mfuko wa upandaji miti ni 5% ya 1,444,000.Bado gharama za kununua mzigo,usafiri,upakiaji na ushushaji ni full usumbufu.Fikiria biashara nyingine ndugu.Ahsante.
 
Mkuu Mbunda @E asante kuboresha mahitaji ya biashara hii. Kweli kuna ushuru wa halmashauri (CES), hii 5% ya upandaji miti analipwa nani mkuu; halmashauri, s/kuu au kijiji?
Pamoja na gharama hizo mkuu, kama mzigo unapatikana kirahisi biashara hii inalipa hasa Dar ambapo sasa gunia moja sii chini ya Tsh 50,000/=. Ukitoa gharama zingine sii haba!
 
Last edited by a moderator:
Habari wanajamvi,mimi ni mama wa watoto wawili,tangu nimalize chuo mwaka 2011 sijafanikiwa kupata ajira.nimeamua nataka kufanya biashara ya mkaa wa jumla (kwa magunia) hapahapa nyumbani kwangu kwani nina nafasi itakayonitosha.shida yangu ni je mkaa mzuri unapatikana wapi?na wenye ujuzi na mkaa eti ni mkaa wa mti gani ni mzuri?pia wenye kujua soko la mkaa likoje tusaidiane mawazo asanteni
 
Habari zenu wapendwa, mimi ninaishi Dar, ningependa kujua mana nina mpango wa kuanzisha biashara ya kununua na kuuza mkaa hapa Dar ila cjajua soko lake liko vipi na mkaa wa jumla ni bei gani na huwa unatoka mkoa gani ili niwe nafata huko ulipo..Eneo pekee ambalo huwa najua ni Mkata ile barabara ya kuelekea Tanga ila cjajua inakuwaje..Kwa yeyote unayefahamu kuhusu biashara nzima ya mkaa, usisite kunishauri tafadhali kwani mawazo yako ni ya muhimu sana kwangu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Mkaa unalipa hasa kipindi hiki cha mvua gunia limefika hadi 70 elf na kwngne 80,mi si mjuzi sana ila kikubwa unatakiwa uwe na kibali cha serikali kuleta huo mkaa dar,na kuna usumbufu fulani hasa barabaran.
 
Unaweza ukafahamu huko wanakotolea mkaa wananunua kwa kiasi gani mpaka wanakuja kuuza Dar 70,000? na wanachukulia wapi??
 
kuna nyuzi nying humu zitakupa maelezo kuhusu hiyo biashara
 
ila mkaa kwa sasa mikoani unapatikana kwa shida sana halafu kuusafirisha mpaka hapa kuna ushuru kila kona nina ndugu yangu anafanya hiyo biashara
 
Ni biashara nzuri kutokana na utakavyoifanya
1.Tatizo liko kwenye usafirishaji hasa wakati huu wa mvua magari hata ya kukodi hayakubali kwenda porini yakihofia kukwama na kuharibika.
2. Unapaswa kukata kibali maliasili
3. Barabarani Maaskari wanakusumbua (hapa uandae fungu)
4. inabidi uwe na ujuzi uweze kuchagua mkaa mzuri usivunjika vunjika

ili kukwepa yote haya. kutegemea na kwamba unahitaji kiasi gani cha mkaa. tafuta mtu anayefahamiana na magari makubwa ya mizigo yanayoleta bidhaa mabli mbali pata mahali pa kununua kwa bei nzuri halafu safirisha mkaa wako kidogo kidogo. hapa maeneo ya river side kuna kijiwe cha kuuza mkaa wanasafirisha kwa njia hiyo wanaupokea pale na kuuza.
 
Nashukuru kwa maelezo yako mazuri, ngoja nitafute watu wa kunisaidia kwa hilo...
 
Huku tabora vijijini mkaa hadi elfu nne(4000) gunia tena mkaa mzuri,
 
Reactions: amu
Aksante kwa ufafanuzi mzuri ila hapo kwenye malipo ya 14400 kwa 90kg,hizi 90kg no gunia ngapi mana naona kama ni gunia moja au mbili.
 
Aksante kwa ufafanuzi mzuri ila hapo kwenye malipo ya 14400 kwa 90kg,hizi 90kg no gunia ngapi mana naona kama ni gunia moja au mbili.
Ushuru kwa 1kg ni Tsh 160/=. Utakadiriwa ukubwa wa gunia zako kwani hawatumii mzani!
 
Ushuru kwa 1kg ni Tsh 160/=. Utakadiriwa ukubwa wa gunia zako kwani hawatumii mzani!
.
Aksante. kwa hiyo hicho kibali cha kuuza mkaa wilayani mwako tunachukulia kwenye ofisi za manispaa mfano temeke pale uwanja wa mpira wa taifa au ofisi za maliasili wilaya?(mimi natarajia kufungua wilaya ya temeke)
 
Narudi kutoa shukrani kwako kwa ushirikiano....kuna sehemu nimesoma muda si mrefu kuwa ofisi za maliasili zipo changombe,naelekea huko sa hivi
 
TARATIBU ZA VIBALI KWA MAZAO YA MISITU-MKAA.


1,Hati ya usajili ambayo ni 261000 kwa mwaka hutolewa na ofisi ya misitu wilaya ambayo utafanyia biashara.
2,Hati ya kusafirisha mkaa ni 6500 kwa fuso na 13000 kwa semi ,hii ni kwa kila safari hii hutolewa kula unapochukulia mkaa(shambani).
3,Leseni ya kuvuna mkaa/ushuru wa serikali kuu ambayo ni 8700 kwa gunia la kawaida na 14700 kwa gunia lumbesa,hii ni sawa na 160 kwa kilo 1
4,Ushuru wa serikali ya mtaa ni kati ya 1000 hadi 2000 kwa gunia
5,Leseni ya biashara na tin
6,Uwe na daftari la mauzo kwa ajili ya ukaguzi ukitokea
7,Mwisho wa kusafirisha mkaa ni sa 12 jioni

NAWAKILISHA
 
Ukifungua ofisi tuwasilianee nina msitu nategemeea kuufyeka soon
msitu wako uko wapi,ili nikadirie gharama za usafirishaji na unaweza kuzalisha gunia ngapi(nitahitaji fuso kama bei yako ni poa,fuso inaingia gunia 170).Bei kwa gunia ni kiasi gani ushuru wa s/k ambao ni 8700 kwa gunia nitalipa mwenyewe
 
msitu wako uko wapi,ili nikadirie gharama za usafirishaji na unaweza kuzalisha gunia ngapi(nitahitaji fuso kama bei yako ni poa,fuso inaingia gunia 170).Bei kwa gunia ni kiasi gani ushuru wa s/k ambao ni 8700 kwa gunia nitalipa mwenyewe
Bado watu wanafanya hiyo biashara pamoja na changamoto zote hizo. Nakushauri waone wanaosafirisha mkaa wanafanyaje mpaka wanamudu kuendelea na hiyo biashara. Jiandae kutoa "kitu kidogo" hamna jinsi.
Mimi mwenyewe nina shamba rufiji nakusudia kuanza kuvuna mkaa September, kuna fedha naisubiri kwa ajili ya vifaa vya vita (chainsaw n.k). Sikusudii kusafirisha naona usumbufu nitauzia shambani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…