Biashara ya kuuza sigara na vocha

Emma M Bai

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
223
Reaction score
126
Naomba kufahamu kama biashara ya sigara za rejareja na vocha maeneo kama stend hivi inalipa?

Wataalam naomba ufafanuzi au tujadili kwa mapana kidogo.

Nina mtaji wa shilingi laki 2 utafaa kuanzia na kama hii biashara inalpa niongeze na nini kinachoendana na biashara tajwa

Naomba kuwasilisha

NB: Kama kuna mtu mwingine anaushauri mzuri zaidi tukiachana na hiyo sigara na vocha ambayo itafaa Kwa mtaji huo nipo tayari kupokea ushauri.

Ushauri kutoka Kwa Mdau niongeze na pombe kali
°cuca
°kitoko
°Double kick
°K-vant
°vodka
°Rizla za kuhesabu

Na vitu vingine vingi ambavyo muda wote vina nunulika
 
Tafuta ujuzi upige sambusa za nyama utembeze
Nataka biashara ambayo kama nawekeza pesa yangu ili ispotee uzoefu wangu biashara ya maduka ya vyakula


Sambusa mkuu pesa yenyewe si naipoteza sasa hapo bado vitendea kazi
 
Lakin mzunguko mkubwa kama upo haina shida kama unauza labda Kwa siku vocha za laki na upo sehem hulip kodi za eneo me naoma kama ndo Fursa peke yake
fanya biashara ya matunda

yaani unakatakat then unapack kwenye vi-contena ni biashara inayolipa kutokana na mtaji wako. unaweza kunitajia mkoa unaotoka ili nikuelekeze sehemu zilizo nzuri kwa biashara hii
 
Lengo langu hii pesa sitaki ipotee nataka nifanye kama naiwekeza saw a na mtu anaenunua ardhi

Nikiweka na sigara zote biashara itaenda binadamu lazima avute naweka na Tigo rusha


Karibuni Kwa mtu ambae ana biashara tofauti na hii lakin sitaki iwe na risk sana ambayo haiwez kupoteza pesa hii nataka ambayo ni ndogo ndogo kama hivyo lakin iwe muda with inatoka

Na nitajitahidi iwe masaa 24 huduma ziwepo lazima

Naomba wadau mawazo yoyote ambayo yatakuwa hayalengi kupoteza hii pesa
 
Ukumbuke kwamba siku hizi watu wengi hawanunui vocha za kukwangua.

Sana sana ni kupitia huduma za fedha kama MPesa, Airtel Money nk.
Sawa lakin ila bado kundi kubwa la watu wa hali ya chini halitumii hizo linatumia za kukwangua naiangalia zaidi hali ya maisha kulingana na sehemu biashara husika
 
hiyo je☝☝☝☝
 
fanya biashara ya matunda

yaani unakatakat then unapack kwenye vi-contena ni biashara inayolipa kutokana na mtaji wako. unaweza kunitajia mkoa unaotoka ili nikuelekeze sehemu zilizo nzuri kwa biashara hii
Ya Matunda brother hii labda niifanyie research kwanza
 
Vipi mkuu funguka nipo ovyo mawazo yako yanaweza kunisaidia
fatilia hii ya kutengeneza matunda iko vizuri alafu pia taja mkoa uelekezwe aina ya biashara kulingana na mazingira husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…