Biashara ya kuuza unga wa mahindi uliosagwa kutoka mikoani na kuleta Dar

Wengi wenye mashine Dar wanapack unga pitia mashine za mazense na kwengineko uone kwanza
 
Jiongeze tengeneza package nzuri na ufanye marketing ili uuze hadi nje ya mkoa wa ruvuma ikibidi hadi nje ya nchi. Nina shem wangu alitajirikia dodoma kwa biashara hiyo hiyo ya kusaga unga wa mahindi bila ya kusafirisha dar.
 
Itakulipa sana ukitafuta sehemu hapo dar kuna store nyingi zimegeuzwa magofu tafuta moja hata Tandika au Gomz tafuta mashine nunua mahindi kwa wakulima bei rahisi hata Morogoro au rufiji saga mwenyewe ongeza virutubisho print mifuko uza unga wako
 
Mimi ni mkazi wa Dar mkuu, rekebisha kauli yako.
 
Hawajui kwa mkoa kama ruvuma wakazi wengi ni wakulima wa mahindi hivyo swala la unga kwao sio tatizo na kingine mzunguko wa pesa au bishara ni mdogo sana songea , nashauri aende akajionee asifikiri watu wite wanaoongea hivi wapo mikoani
 
Inawezekana na wengi tu wanaleta unga toka mikoani kwa nembo ya Dar unasagia na kupaki huko huko ulipo kwa nembo ya plant ya Dar kisha unakuja uza Dar na si lazima uww na mashine unaaanza kusagia mashineni
 
Hawajui kwa mkoa kama ruvuma wakazi wengi ni wakulima wa mahindi hivyo swala la unga kwao sio tatizo na kingine mzunguko wa pesa au bishara ni mdogo sana songea , nashauri aende akajionee asifikiri watu wite wanaoongea hivi wapo mikoani
Unamaanisha biashara Songea ni mbaya
 
Hili jambo halina maaumuzi ya kudumu. Kuamua uzalishie mkoani au Dar inategemea na bei ya Mahindi ya Sehemu zote mbili, Bei ya Pumba ya sehemu zote mbili, Bei ya Unga kwa sehemu zote mbili na hali ya upatikanaji wa mahindi.

Weka excel itakayoruhusu mabadiliko ya hizo parameters na itakusaidia kujua ni wakati gani uzalishie mkoani na ni wakati gani uzalishie Dar.

Na ukiwa smart, huitaji kuhangaika na mahindi. Wekeza kwenye branding, promo, quality, tafuta virutubisho na uvifanye siri na then nunua unga, weka nembo yako na ongeza virutubisho. Segment soko lako na uhakikishe unafikia mahitaji ya walaji uliowachangua.
 
Dona inaweza kuongezwa virutubisho gani
 
Jiongeze tengeneza package nzuri na ufanye marketing ili uuze hadi nje ya mkoa wa ruvuma ikibidi hadi nje ya nchi. Nina shem wangu alitajirikia dodoma kwa biashara hiyo hiyo ya kusaga unga wa mahindi bila ya kusafirisha dar.
Kwann umetumia past tense mkuu? Utajiri uliondoka ?
 
Natamani kupata no yako
 
Sijafahamu mkuu lakini tunataka tutoe mkoani nyanda za juu kusini hasa Ruvuma kule kilo mahindi 540 tuyasagie kule ili tuje tuuzie huku Dar
Jaribu pia kucheki na mikoa ya kusini, maana unga unatokaga dar unaenda huko. Kila la kheri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…