Biashara ya kuuza unga wa mahindi uliosagwa kutoka mikoani na kuleta Dar

Biashara ya kuuza unga wa mahindi uliosagwa kutoka mikoani na kuleta Dar

Wengi wenye mashine Dar wanapack unga pitia mashine za mazense na kwengineko uone kwanza
 
Mkuu kama umetembea mikoa mingi ya Tanzania utakubaliana hakuna Mkoa hata mmoja unafikia Dar hata kwa asililimia 60 kwa kila kitu.

Dar is far the most developed and fast growing Region in Tz.

Ukiongelea biashara ya mahindi kwa mfano....Ruvuma kuuza kilo za Unga 100kwa siku inweza kuwa ndoto wakati Dar utauza siku moja au siku mbili tu.

Ruvuma unaweza ukawa unauza kilo 5 hadi 10 tu kwa siku. Sasa Tani Moja utaimaliza lini.
Jiongeze tengeneza package nzuri na ufanye marketing ili uuze hadi nje ya mkoa wa ruvuma ikibidi hadi nje ya nchi. Nina shem wangu alitajirikia dodoma kwa biashara hiyo hiyo ya kusaga unga wa mahindi bila ya kusafirisha dar.
 
Habarini wakuu

Kwa muda mrefu nimekuwa na wazo la kufungua biashara ya uuzaji wa unga wa mahindi ambapo unga utakuwa unasagwa mkoani na kuletwa huku Dar

Kutokana na ugeni katika nyanja hii imenipasa kutafuta taarifa muhimu ambazo zinaweza kunisaidia kufanya hii biashara.

Kwahiyo kama kuna mtu ana uzoefu na biashara hii kwa huku Dar kama ni potential au lah naomba aniambie na kama ikiwa ni ngumu pia nikipata ushauri namna ya kuikuza ikawa yenye manufaa zaidi naomba aniambie

Asanteni
Itakulipa sana ukitafuta sehemu hapo dar kuna store nyingi zimegeuzwa magofu tafuta moja hata Tandika au Gomz tafuta mashine nunua mahindi kwa wakulima bei rahisi hata Morogoro au rufiji saga mwenyewe ongeza virutubisho print mifuko uza unga wako
 
Watu wa mikoani wana ushamba sana wa dar! Yaani kila siku wanawaza wafanyeje ili wawe na acces ya kufika dar mara mara. Mtu kama mleta mada anaweza kukomaa huko huko nyanda za kusini na akatoboa huko huko coz soko bado ni kubwa ila unaweza kuta yeye mwenyewe haamini anaweza kutoboa bila kuja Dar

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mimi ni mkazi wa Dar mkuu, rekebisha kauli yako.
 
Mkuu kama umetembea mikoa mingi ya Tanzania utakubaliana hakuna Mkoa hata mmoja unafikia Dar hata kwa asililimia 60 kwa kila kitu.

Dar is far the most developed and fast growing Region in Tz.

Ukiongelea biashara ya mahindi kwa mfano....Ruvuma kuuza kilo za Unga 100kwa siku inweza kuwa ndoto wakati Dar utauza siku moja au siku mbili tu.

Ruvuma unaweza ukawa unauza kilo 5 hadi 10 tu kwa siku. Sasa Tani Moja utaimaliza lini.
Hawajui kwa mkoa kama ruvuma wakazi wengi ni wakulima wa mahindi hivyo swala la unga kwao sio tatizo na kingine mzunguko wa pesa au bishara ni mdogo sana songea , nashauri aende akajionee asifikiri watu wite wanaoongea hivi wapo mikoani
 
Inawezekana na wengi tu wanaleta unga toka mikoani kwa nembo ya Dar unasagia na kupaki huko huko ulipo kwa nembo ya plant ya Dar kisha unakuja uza Dar na si lazima uww na mashine unaaanza kusagia mashineni
 
Hawajui kwa mkoa kama ruvuma wakazi wengi ni wakulima wa mahindi hivyo swala la unga kwao sio tatizo na kingine mzunguko wa pesa au bishara ni mdogo sana songea , nashauri aende akajionee asifikiri watu wite wanaoongea hivi wapo mikoani
Unamaanisha biashara Songea ni mbaya
 
Hili jambo halina maaumuzi ya kudumu. Kuamua uzalishie mkoani au Dar inategemea na bei ya Mahindi ya Sehemu zote mbili, Bei ya Pumba ya sehemu zote mbili, Bei ya Unga kwa sehemu zote mbili na hali ya upatikanaji wa mahindi.

Weka excel itakayoruhusu mabadiliko ya hizo parameters na itakusaidia kujua ni wakati gani uzalishie mkoani na ni wakati gani uzalishie Dar.

Na ukiwa smart, huitaji kuhangaika na mahindi. Wekeza kwenye branding, promo, quality, tafuta virutubisho na uvifanye siri na then nunua unga, weka nembo yako na ongeza virutubisho. Segment soko lako na uhakikishe unafikia mahitaji ya walaji uliowachangua.
 
Na ukiwa smart, huitaji kuhangaika na mahindi. Wekeza kwenye branding, promo, quality, tafuta virutubisho na uvifanye siri na then nunua unga, weka nembo yako na ongeza virutubisho. Segment soko lako na uhakikishe unafikia mahitaji ya walaji uliowachangua
Dona inaweza kuongezwa virutubisho gani
 
Jiongeze tengeneza package nzuri na ufanye marketing ili uuze hadi nje ya mkoa wa ruvuma ikibidi hadi nje ya nchi. Nina shem wangu alitajirikia dodoma kwa biashara hiyo hiyo ya kusaga unga wa mahindi bila ya kusafirisha dar.
Kwann umetumia past tense mkuu? Utajiri uliondoka ?
 
Hii ni biashara nzuri Sana Mkuu Cha kufanya hapa tafuta wakala wa hapa DSM akutafutie wateja itakuwa vizuri Zaid uki deal na wafanyabiashara wa jumla. Yaani ukiweza kupack fresh na ukipata usafiri wa uhakika ni biashara inayolipa Sana.

Pack kuanzia kg 5,10,25

Ukikwama niambie nikutafutie wateja
Natamani kupata no yako
 
Sijafahamu mkuu lakini tunataka tutoe mkoani nyanda za juu kusini hasa Ruvuma kule kilo mahindi 540 tuyasagie kule ili tuje tuuzie huku Dar
Jaribu pia kucheki na mikoa ya kusini, maana unga unatokaga dar unaenda huko. Kila la kheri
 
Back
Top Bottom