Biashara ya madini ni kichaa. Kaka yangu kapoteza milioni 120 mwezi huu nimemkuta ameshaanza kudata

Biashara ya madini ni kichaa. Kaka yangu kapoteza milioni 120 mwezi huu nimemkuta ameshaanza kudata

Wachimbaji wadogo wengi wanafanya kwa kubahatisha, hawafanyi utafiti.

Madini siyo maharage ambayo unapanda sehemu na kuyaona yanavyokua. Kwenye madini, unatafuta kitu ambacho hukuweka wewe wala rafiki yako. Hivyo hatua ya kwanza ni kufanya utafiti, siyo kuchimba. Unachimba baada ya kufanya utafiti, na kujua yako wapi,, kwa kiwango gani.
Nilishwahi kulizungumza hili humu JF lakini washirikina wale hawakunielewa.....huko chunya exploration shanta wametenga bajeti ya kutosha kufanya utafiti mashimo ya DD yanachimbwa ya kutosha kufanya utafiti na shimo moja linaweza kwenda mpka 150M halafu wewe na 120M yako uje upate mzigo kizembe.
 
Aisee naandika huu Uzi nikiwa nimekuja kumtembelea kaka yangu hospital hapa Mbeya, aisee hii biashara sio ya kuingilia kichwa kichwa.

Huwezi amini nipo hospitali maana broo kama akili zishaanza kuwehuka, vitu anavyoongea havieleweki aisee, haamini kama kafukia milioni 120.

Nawashauri ndugu zangu wana jamiiforums hii sio biashara ya kufanya, ni kama inauchawi fulani hivi!
Sio kama ina kauchawi. Kwenye madini kuna uchawi balaa, wapo watu wamepoteza pesa mpk maisha
 
Nitarudi!! Get well soon mpambanaji.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Kazi za wanaume hizo, kama alishaonja pesa ya madini atarudi tu. Kupoteza inatokea ila kupata ndio hua hesabu kuu.
 
Biashara yoyote ukiingia kichwa lazima likukute Jambo zito sana
 
Ndio nimefika Leo nilipigiwa simu jana kwamba kaka yangu kalazwa sababu ya kupoteza pesa machimboni Kwa kuendesha harakati za uchimbaji Sasa bado sijapata abc sababu ndio nimefika Leo mda huu
Poleni familia kwa hiyo changamoto
 
Back
Top Bottom