Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

Hapana sijawahi kutumia karasha za kawaida. Ila wanaotumia ndio nimewaskia kuwa wanapata tabu kdg mawe yakiwa na maji. Labda walio na experience nazo humu watatupa details
Mawe yakiwa na maji yanaanikwa juani au yanakaangwa/yanachomwa na moto kwenye kikaango, ambacho kinatengenezwa kwa kukata pipa na kulitengeneza mfano wa sahani ya pembe nne...
 

Wadau poleni na swaumu mulio katika mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Napenda kujulishwa kwa mwenye uzoefu biashara ya dhahabu inalipa vipi kwa mtaji wa million 5, tahadhali za kuchukua dhidi ya utapeli, vibali vya biashara na maeneo ambayo yako suitable kwa hiyo biashara.

Natanguliza shukrani.

WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU BIASHARA HII


MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI









Jinsi ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Madini​

1.0 Utangulizi

Uchimbaji wa madini ni kuyatoa madini kutoka ndani ya ardhi kuja nje na kuyapa dhamani kwa kukata (vito vya dhamani) au kusafisha (metali) kwa ajili ya matumizi ya binadamu. Uchimbaji wa madini inahusisha pia uchimbuaji wa mawe ya kujengea na dhamani zingine zilizoko ndani ya ardhi. Utaratibu au ustaharabu wa kuchimbua mawe kwa matumizi ya binadamu ulianza pale mwanadamu alipobuni na kuanza kutumia mawe (enzi za ujima) na baadaye metali ya chuma na metali zingine ili kurahisisha kazi . Pia uchimbaji wa madini unajumuisha uchimbuaji wa rasilimali zingine za ardhi kama maji, gesi na mafuta kwa matumizi ya binadamu.
Shughuli za uchimbaji wa madini ndio mojawapo ya shughuli inayoongoza katika kuharibu na kuchafua mazingira na kwa hiyo tathimini ya utunzaji wa mazingira ni muhimu kufanyika kabla ya kuanza kuchimba ili kuweka mpango, mkakati na mbinu za kuhifadhi na kutunza mazingira katika maeneo ya ndani na nje ya mgodi
Kwanza kuna mambo muhimu ni lazima uyafahamu kabla ya kuingia kwenye biashara hii

1.1 Ngazi za Uwekezaji Biashara ya Madini​

  1. Makampuni madogo ya uwekezaji, (Uwekezaji wa mtaji chini ya dola za kimarekani milioni 50)
  2. Makampuni ya kati ya uwekezaji (Uwekezaji wa mtaji kati ya dola milioni 50 na milioni 500)
  3. Makampuni makubwa (Uwekezaji wa mtaji wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 500)

a) Makampuni madogo ya uwekezaji – chini ya dola za kimarekani milioni 50​

Makampuni madogo ni yale ambazo kwa kiwango kikubwa zinawategemea wenye hisa kununua hisa ndipo zijiendeshe. Nyingi ya makampuni hizi ni za utafutaji wa madini na zinaweza kuwekeza mitaji midogo kwenye uchimbaji mdogo na hivyo kupata mapato yasiyozidi dola milioni 50 kwa mwaka

b) Makampuni ya kati ya uwekezaji dola milioni 50 hadi milioni 500​

Makampuni ya kati ni yale yenye mapato kwa mwaka kati ya dola za kimarekani milioni 50 mpaka milioni 500 na hazina uwezo wa kujenga miundo mbinu ya machimbo kama open pit au underground mining sites

c) Makampuni makubwa ya uwekezaji – zaidi ya dola milioni 500​

Makampuni yenye mapato ya mwaka ya dola Milioni 500 kwenda juu ndizo zinazohesabiwa kuwa ni makampuni makubwa. Pia ni lazima ziwe na uwezo wa kujenga miundo mbinu ya machimbo kama open pit au underground mining sites bila pesa za nje.
Tuchukulie wewe ni mchimbaji mdogo wa mtaji ulio chini ya milioni 50, sasa unatakiwa pia kujua aina za biashara za madini

1.2 Aina za Biashara za Madini​

  1. Utafutaji wa Madini (Mineral Exploration)
  2. Uchimbaji wa Madini (Mining)
  3. Kuchuuza (Brokering or Trading)
  4. Kutoa Huduma na Ushauri (Service and Consultancy)

a) Utafutaji wa madini au Mineral Exploration​

Utafutaji wa madini ni biashara nzuri kidogo kwa wale wanaoogopa vihatarishi na pia wanaridhika na faida za wastani. Uwekezaji wake ni mdogo na wa hatua mpaka upate prospect halafu unauza. Hatari yake kubwa iko kwenye kupata mkopo na prospect. Mpaka benki wakupe ni lazima uwe na track record nzuri sio tu ya kuchukua mikopo bali pia ya kuifanya hiyo biashara ya utafutaji kwa asilimia kubwa ya mafanikio.

b) Uchimbaji wa Madini au Mining​

Uchimbaji wa madini au mining ni kazi ngumu katika madini kwani kwanza uwekezaji wake ni mkubwa na pia unaweza ukakuta sivyo ndivyo au ndivyo sivyo kule ndani ya ardhi. Vifaa vyako vinaweza kukuonyesha kuna ngema ya kutosha lakini ukizama chini unakuta tofauti. Aidha unakuta ngema kubwa zaidi au unakuta kangema ambacho hata ngarama haiwezikurudisha. Na ndio maana utafiti wa hali ya juu na usio na haraka ni muhimu kabla hujafikia uamuzi wa kuchimba

c) Kuchuuza au trading

Hii ni hatua rahisi kuliko zote kwani hapa unahitaji vitu viwili tu
  1. Utaalamu wa madini unayotaka kuchuuza
  2. Mtaji wa kuanzia

d) Kutoa Huduma na Ushauri (Service and Consultancy)

Hii ni pale unapoamua kutumia ujuzi, uzoefu na vipawa vyako kwa kuwasaidia waliopo au wale wanaotaka kuingia kwenye biashara hiyo.
Huduma zinaweza kuwa ni
  1. Kufanya sorting
  2. Huduma za Umeme na maji
  3. Huduma za usafiri ndani na nje ya mgodi
  4. Huduma za chakula na
  5. Huduma za usafi
  6. Huduma za maduka
  7. Masoko na Kuuza
  8. Kuhudumia vifaa vya uchimbaji
  9. Kuwafundisha wataalamu /wafanyakazi wa migodi nk

2.0 Hatua 9 za Kufuata Ili Kuanzisha Biashara ya Madini​

  1. Kusajili Kampuni BRELA
  2. Kijiandikisha Mlipa Kodi
  3. Kuchukua Leseni
  4. Kuchukua Hati ya Usalama wa Mazingira
  5. Kuajiri wafanyakazi na wataalamu wengine
  6. Kununua na kuandaa vifaa mbalimbali
  7. Kutafuta masoko
  8. Kuanza uchimbaji wa majaribio
  9. Kuanza Uchimbaji Wenyewe
1. Kusajili Kampuni
Shirkisha mshauri wa biashara na mwanasheria wa upande wa makampuni ili wakusaidie kwa ushauri na utengenezajiwa MEMART ambayo ni muhimu katika kusajili kampuni

Unaweza kwenda mwenyewe BRELA kusajili au ukamtumia mhsauri mtaalamu wa mambo hayo. Nashauri umtumie mshauri mataalam ili kuokoa gharama za pesa na muda

2. Kijiandikisha Mlipa Kodi kwa kuchukua TIN TRA
Kujiandikisha TIN ni bure na inapatikana kwenye matawi yote ya TRA Tanzania

3. Kuchukua Leseni Wizara ya Nishati na Madini
Baada ya kukamilisha vigezo vya wizara unayo haki sasa ya kuomba leseni ya utafutaji au uchimbaji wa madini ambayo inatolewa na wizara ya Nishati na Madini

4. Kuchukua Hati ya Usalama wa Mazingira
Biashara ya madini ni mojawapo ya biashara inayoharibu mazingira kwa hali ya juu. Ni utaratinu wa mataifa yote duniani kutaka kuwa na uhakika wa utunzaji wa mazingira na hivyo bodi au mamlaka husika watahitaji kuingia mkataba na wewe ili wawe na uhakika kuwa mazingira yatakuwa salama wakati na baada ya uchimbaji.

5. Kuajiri wafanyakazi na wataalamu wengine
Biashara ya madini itahitaji wafanyakazi wa takriban nyanja zote kuanzia wahudumu, maofisa wataalamu na washauri. Hawa wote ni lazima uwaajiri au uwe na uhakika utawapata wapi kwa gharama muafaka

6. Kununua na kuandaa vifaa mbalimbali
Uchimbaji wa madini unatumia technolojia ambazo ndizo zitakazoamua kama wewe ufanikishe mradi au la. Teknolojia ya zamani ianweza kukupa hasara japo rahisi, teknolojia za kienyeji nazo zinaweza kukupa hasara. Teknolojia za kisasa zina faida japo ni ghali kununua. Unashauriwa kuwa na wataalamu washauri wa kukushauri tangu mwanzo namna ya kuamua juu ya teknolojia utakayotumia.
Kwa nini teknolojia za kienyeji au za zamani zina hasara?
  1. Nyingi ya hizo zinatumia muda mrefu kuleta matokeo
  2. Zina gharama kubwa za uendeshaji
  3. Zinaharibu mazingira
  4. Zinahitaji wafanyakazi wengi
  5. Nk
7. Kutafuta masoko
Kulingana na ukubwa wa uchimbaji au utafutaji, ni vyema kutafuta masoko ambayo utauza madini. Ikiwezekana uingie na mikataba ili uwe na uhakika wa kuuza punde utakapovuna.
8. Kuanza uchimbaji wa majaribio
Fanya uchimbaji wa majaribio angalau kwa miezi mitatu hadi sita kwa uchimbaji mkubwa kidogo unaweza kwenda hadi mwaka mmoja. Uchimbaji wa majaribio itakupa fursa ya kujua yafuatayo:
  1. Je vifaa vitafaa kwa malengo yako
  2. Je wafanyakazi uliowaajiri wanaweza kufanya uzalishaji wenye tija
  3. Je biashara nzima italeta tija iliyokusudiwa
9. Kuanza uchimbaji Halisi
Baada ya uchimbaji wa majaribio, sasa unaweza kwa ujasiri kabisa kuanza kuchima madini. Muhimu tu ni kwamba yafanyie kazi changamoto zote zilziojitokeza kwenye uchimbaji wa majaribio

Credits: Kivuyo.com
[emoji120]
 
Mzan tu inakimbilia 11m..mie namanisha jiko la dhahabu...sio ile ya kununua huku machimboni . Its above 80_100m..maana kwa siku unaweza nunua gram zaid100...ss piga hesabu sio chini ya 23m hapo...
Mrejesho wa upatikanaji wa dhahabu ya Malinyi Misegese tafadhali, mambo yakoje?
 
SHUGHULI ZA MGODINI KWA WASIO NA MTAJI

Kiukweli kule ujitoe tu ufahamu kama huna mtaji! Kazi zipo ila za kutumia nguvu especially kuosha unga, kuchenjua dhahabu (hapa lazima ujifunze kwwli kweli) na ni ngumu mtu kukupa tope lake umchenjulie, wanaiba sana hapa kwa kuchenjua.

Kazi nazoona wanafanya zaidi kina kaka wasio na .mtaji ni kupiga moko(kuzamaa huko chini kupiga mwamba) ni kazk ngumu kiukweli, ila ukibahatika ukatoka na kajiwe uongo! Mistake za kule ni zile zile kwasababu kazi ni ngumu bas mtu akipata hela anatumia hovyo sana!

Kuosha unga ni 2000@ mzunguko mmoja. Mzunguko mmoja unaweza chukua ndoo zile ndogo 5-8!inategemeana na ukubwa wa ile machine(crusher )na inaweza zidi pia kidogo. So unga ni mwingi kiukwel. Sasa vibarua ni hela ya kula tu..mayb uombe uoperator na mkubaliane mlipane mkishauza kifusi. Hapo makubaliano ni yenu wewe na mwajiri wako! Bt haizid 500k had kaz kufunga!

Mie nachoamini pia ni bahati! Kuna dogo ndugu yangu alifika kule mwaka 2017! Akitokea chuo, alifika hana kitu akaomba kwa mzee 200k! Leo hii kila miezi miwili ana faida ya kuanzia 6-8m!so alianza na , 200k akinunua mawe ya bei ya chini(fello) akapanda had kumiliki crusher! Means akianza leo 14th kazi anafunga 14 July anauza kifusi yy hana mpango na plant kbs.faida ndo hizo 6-8m! Ikigoma sana 4m. Kule naona wasomi kama wanatoka mapema eti! Mradi uwe serious na usmart fulani!

Na ukitaka kufanikiwa mapema nenda kwenye mgodi ulolipuka. Sio mgodi uliodormant!
Mkuu hapo kwenye kununua mawe ya bei ya chini pamenivuta. Kwa hyo jamaa alikuwa anakusanya mawe mpka kinafika kifusi anauza?
 
Mkuu hapo kwenye kununua mawe ya bei ya chini pamenivuta. Kwa hyo jamaa alikuwa anakusanya mawe mpka kinafika kifusi anauza?
Kifusi ni udongo ulitolewa dhahabu, ila hicho kifusi kinanuliwa na watu kwa ajili ya kupeleka plant ili kuozeshwa na makemikali kwa ajili ya kupata dhahabu zaidi.
 
Kifusi ni udongo ulitolewa dhahabu, ila hicho kifusi kinanuliwa na watu kwa ajili ya kupeleka plant ili kuozeshwa na makemikali kwa ajili ya kupata dhahabu zaidi.
Well basi sijamuelewa, kama umepata point ya alichokizungumza, naomba nieleweshe mkuu!
 
Afadhali huyu ameomba ushauri hapa jukwaani. Mwaka 2016 nilifuatwa inbox na jamaa mmoja baada ya kuchangia kwenye uzi humu jf. Yule jamaa mpaka leo nashindwa kuelewa lengo lake. Alinisumbua sana mpaka nikaanza kumpa ushirikiano.

Mara nina mtaji wa 20m USD nahitaji kuwekeza, tafuta eneo tununue, fuatilia vibali na mambo meeeeengi. Na wakati huo nilikuwa hovyo nikawa nahangaika nikijua hapa mambo si muda yatajipa.

Baada ya kuhangaika nae mwisho nilianza kuwa na mashaka naye. Mpaka leo siwezi kumsaidia mtu inbox mpaka nione kuna umuhimu. Kwanza nimejifunza ukitoa elimu jukwaani unawasaidia wengi.

Shukurani sana kwa Wangari Maathai kwa elimu unayoitoa hapa.
Nakutana na watu wa hivi wengi sana inbox, wengi wengi wengi

nimeanza ka utaratbu kagumu kdg huko inbox wanaonifata wanaelewa

mpaka nitoe muda wangu kwa mtu inbox hadi nijiridhishe nae aseee not otherwise
 
Afadhali huyu ameomba ushauri hapa jukwaani. Mwaka 2016 nilifuatwa inbox na jamaa mmoja baada ya kuchangia kwenye uzi humu jf. Yule jamaa mpaka leo nashindwa kuelewa lengo lake. Alinisumbua sana mpaka nikaanza kumpa ushirikiano.

Mara nina mtaji wa 20m USD nahitaji kuwekeza, tafuta eneo tununue, fuatilia vibali na mambo meeeeengi. Na wakati huo nilikuwa hovyo nikawa nahangaika nikijua hapa mambo si muda yatajipa.

Baada ya kuhangaika nae mwisho nilianza kuwa na mashaka naye. Mpaka leo siwezi kumsaidia mtu inbox mpaka nione kuna umuhimu. Kwanza nimejifunza ukitoa elimu jukwaani unawasaidia wengi.

Shukurani sana kwa Wangari Maathai kwa elimu unayoitoa hapa.
Huyo alinifuata hata Mimi inbox aliniambia Yuko German ila ni Raia wa kenya. Alinihangaisha saaana ofisi za TANZANIA INVESTMENT CENTER
 
Huyo alinifuata hata Mimi inbox aliniambia Yuko German ila ni Raia wa kenya. Alinihangaisha saaana ofisi za TANZANIA INVESTMENT CENTER
[emoji4][emoji4][emoji4] pole sana. Jamaa ni mjinga sana
 
Nakutana na watu wa hivi wengi sana inbox, wengi wengi wengi

nimeanza ka utaratbu kagumu kdg huko inbox wanaonifata wanaelewa

mpaka nitoe muda wangu kwa mtu inbox hadi nijiridhishe nae aseee not otherwise
Wanafanya hata muhitaji ahisi members wenzie wanajivuna.
 
Back
Top Bottom