Biashara ya maharage frozen

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kutokana na maharage kuwa chakula na mboga pendwa pamoja na mapishi yake ya kuchukua muda mrefu kuiva na pia kutumia nishati nyingi. Biashara ya kuuza maharage yakiyochemshwa na kugandishwa katika ujazo wa 1/4, 1/2 na kilo moja.

Changamoto kubwa ni kuwa aina ipo ya maharage hupendwa zaidi. Kuna Serian, Meupe, ya njano, ..

Ninaomba uandike maharage unayopenda kula utakuwa umenisaidoa sana katika itafiti wangu.
 
Last edited:
wazo zuri sana. mie pia ntalifanyia kazi
Kama una freezer nunua container za plastic. Wateja lengwa ni wanafunzi wa chuo na vijana wanaoanza maisha. Hata watu wenye familia pia utawapata.
 
Kama una freezer nunua container za plastic. Wateja lengwa ni wanafunzi wa chuo na vijana wanaoanza maisha. Hata watu wenye familia pia utawapata.

Asante sana.. Hi kitu nataka niifanyie kazi. maana ninakijisehemu nataka kufungua min-supermarket
 
maharage yanayouza sana soko la congo ni kitenge au mix, na maharage ya njano yanaitwa kigoma.
Zanzibar ,tanga, mombasa, moroco ni maharage fulani yanaitwa rose coco ndio maarufu,
halafu kuna njano ndefu ya bukoba haya yanaiva haraka nayo hupendwa pia.
nipe dili niwe supplier wako wa maharage lakini uanzie tani 100 kupanda juu..
 
kuna njano fupi ile wanayotengenezea bia ya balimi hua inachelewa kuiva lakini wakenya ambao sio wa pwani wanaila sana.
 
kitenge au mix iko chini kwa bei lakini haipendwi sana kwani inaliwa sana magereza na mashuleni.
 
Shukran sana mkuu ngoja niangalie yanayotoka sana kwanza.
 
Maharage ya njano.
Ishu IPO mwenye utamaduni wetu,watu hawana mazoea ya kununua vyakula vya makopo,
Mi mwenye we nilitaka kuwaletea wanaume wa dar,frozen chips,nikaona zitanidodea.
Inabidi ufanye marketing ya nguvu sana,nyumba kwa nyumba
 
kuna njano fupi ile wanayotengenezea bia ya balimi hua inachelewa kuiva lakini wakenya ambao sio wa pwani wanaila sana.
Inategemea na mapishi, maharage ya curry beans haya taji will yai a mpaka yatoe rojo. Unatakiwa uyasikie ukiyatafuna
 
Maharage ya njano.
Ishu IPO mwenye utamaduni wetu,watu hawana mazoea ya kununua vyakula vya makopo,
Mi mwenye we nilitaka kuwaletea wanaume wa dar,frozen chips,nikaona zitanidodea.
Inabidi ufanye marketing ya nguvu sana,nyumba kwa nyumba
Niliuliza wanachuo wa UDSM kama kumi hivi na waliniambia nitakuwa nimewasaidia sana na watawaarifu wenzao.
 
Elungata uko sahihi ukijaribu kuangalia utamaduni wa shoping malls na super& minmarkets kwa sisi tanzania kiukweli bado sana wenzetu kenya na uganda hadi kijijini wanajua minmarket inatakiwa sisi tukiona hivo vitu tunajua huko bei ziko juu za bidhaa,
utakuta kwa Dar shopping ni buguruni na tandale na kkoo.
kwa mwanza ni kujazana igoma na buhongwa.
kwa kigoma ni nazareti na mwanga
yaani cjui tukoje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…