Mimi nafanya hii biashara pia Kinondoni duka lipo Mkwajuni mtaa wa Moscow nauza maji ya kampuni ya Uhai na Hill. Kwa Uhai unaanza na carton 1,000 baada ya hapo unaruhusiwa kuchukua order ya carton minimum 500. Ila kwa hill unachukua carton kuanzia 300, ndio unauziwa kwa bei ya kiwandani, ambapo wanakuletea hadi dukani kwako.
Faida ni 200 kwa kila carton, hivyo inahitaji uwe mahali penye mzunguko mkubwa ili uweze kuona faida.
Pia, japokuwa kwa sasa nauza maji tuu ila nilichobaini unatakiwa kuwa na bidhaa nyingine kama juice na soda kwa kuwa soko lako kuu ni wateja wanaouza maduka ya retail. Hivyo mara nyingi wanapoweka order ya mzigo huwa wanahitaji supplier ambaye ataweza kuwapa vinywaji vyote. Ukidepend kwenye maji peke yake kuna wakati mauzo yanakuwa magumu.
So naendelea kujipanga Mungu akijaalia fedha baada ya miezi michache nitaongeza vinywaji hasa kutoka kampuni ya Sayona & Mo.