Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake

Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake

Pamoja na ushauri mzuri uliotolewa, nashauri aende kwenye kutengenza vyakula vya mifugo haswa kuku na ng'ombe. hiyo itamlipa vizuri kama ni hapa Dar.

Maana hawa akina Azam na Azania itakuwa vigumu kushindana nao na wanaendelea kuwekeza tu.

Naona kwenye mifugo ushindani sio mkubwa! Biashara ukae mwenyewe, ukimweka ndugu yako au shemeji umeshashindwa kabla hujaanza!

Asante sana wana JF nazidi kupata mawazo mazuri sana la kampuni ni lamaana sana,kwa hiyo nitaweza kuwa na packaging zenye nembo ya kampuni yangu na kusambaza sehemu mbalimbali mjini,hapo nimekupata.Suala la kutafuta masoko kwenye taasisi na mavyuo nalikubali na kushukuru kwa ushauri mzuri sana ntaufanyia kazi.

Kulima shamba usipate taabu sana maana risk ni kwa upana katika biashara. Ila ukifanikiwa kuwa na chanzo chako mwenyewe unaweza tengeneza faida kubwa.

Hilo ni kwa baadaye, na ukiamua kuanza na ununuzi toka kwa wakulima ni vema maana unapata nafasi ya kujipanga vizuri, kwani subira yavuta kheri na kila penye nia pana njia.

Asante sana wana JF nazidi kupata mawazo mazuri sana la kampuni ni lamaana sana,kwa hiyo nitaweza kuwa na packaging zenye nembo ya kampuni yangu na kusambaza sehemu mbalimbali mjini,hapo nimekupata.Suala la kutafuta masoko kwenye taasisi na mavyuo nalikubali na kushukuru kwa ushauri mzuri sana ntaufanyia kazi.

Kuna mmoja hapa amedokeza utengenezajiwa wa vyakula vya mifugo, hilo jambo zuri sana, kwani pumba zitokanazo na mafaka unazifanyia recycle kwa kutengeneza vyakula vya mifugo, hapo unapiga ndege wawili kwa jiwe moja. Kaza kamba yakhe kwani njia ipo wazi.

Pamoja na ushauri mzuri uliotolewa, nashauri aende kwenye kutengenza vyakula vya mifugo haswa kuku na ng'ombe. hiyo itamlipa vizuri kama ni hapa Dar. Maana hawa akina Azam na Azania itakuwa vigumu kushindana nao na wanaendelea kuwekeza tu. Naona kwenye mifugo ushindani sio mkubwa! Biashara ukae mwenyewe, ukimweka ndugu yako au shemeji umeshashindwa kabla hujaanza!

Ni kweli hawa wakina Azam wamekubuhu hiyo ni challenge kubwa,kuhusu kutengeneza vyakula vya mifugo nimekupata,licha ya kuuza itanisaidia na mimi pia manake ndio nimeanza ufugaji wa kuku kwa hiyo kwa upande wa vyakula itakua hainipi tabu.

Nafikiri fanya research ya kutosha kabla ya kujiingiza kwenye biashara hii ikiwa ni pmj kuangalia eneo ambalo unahitaji kuinvest,upatikanaji wa raw material(mahindi), wateja,idadi ya washidani kama wapo, bei yao,uwezo wa wateja(economic base) sifa ya mjasiriamal ni kutake risk ,usiogope hasara la sivyo utakufa presha bure once unapopata hasara.mkuu ubarikiwe sönga mbele.

Kweli nitajaribu kufanya reseach ya kutosha kabla ya kuanza,kuhusu hasara kweli ipo lakini inachosha sana pale unapoingiza milioni kadhaa kwenye biashara halafu inazama kama ilivyo bila return,halafu fedha yenyewe ukute umekopa kwenye taasisi za fedha na unahitajika ulipe.

Ni kweli hawa wakina Azam wamekubuhu hiyo ni challenge kubwa,kuhusu kutengeneza vyakula vya mifugo nimekupata,licha ya kuuza itanisaidia na mimi pia manake ndio nimeanza ufugaji wa kuku kwa hiyo kwa upande wa vyakula itakua hainipi tabu.

mkuu hawa kina azam ni wafanyabiashara wakubwa nadhani dhana hii iondoke tunacho aim hapa ni kuwa na kuanzisha viwanda vidogo vidogo kama mradi wako huu wa kusaga mahindi na ku pack unga. viwanda hivi vita weza kupata wateja into a specific location.

let say umelocate goba hivyo basi ukifanya uzalishaji wako na unga ukawa ni bora hutakuwa na cost kubwa za usambazaji pale goba hivyo bei yako yaweza kuwa chini kuliko azam ambaye analeta ungo toka buguruni

pia jaribu kuwa na packs zenye ujazo tofauti. kwenye commerce kunakitu wanaita double coincidence of wants. hii inamaana unaweza anza kuuza hata maharage

Ninauhakika utafanikiwa

Bei ya mashine za SIDO moshi ni kama ifuatavyol;
- Mashine ya kusaga namba 75 ni Tshs.2,500.000/=
- Mashine ya kukoboa rola tatu ni Tshs. 2,500,000/=
Mashine hizo zinakuwa zimewekewa Mota ya 25 Horse powe, Stata ya 25HP pamoja na frame zake.

Wasiliana na Maneja wa Karakana kwa simu namba 0754-399922. Mashine zao ni nzuri sana na imara kabisa.mimi nazitumia kwa sasa. Bei ni negotiable.

Purchase them you will never regret. Sipendi kuharibu biashara za watu lakini uzoefu wangu unaonyesha kuwa mashine toka china na ambazo zinauzwa na auto sokoni bei yake ni rahisi sana lakini sio imara na milling na hulling (usagaji na ukoboaji) capacity yake ni ndogo sana. Ni ushauri tu mkuu.

Wengi tumeelimika na eimu hii mliyoitoa, nimekopi posti zote nyeti katika hii thread ili zinisaidie kupanga vema biashara hii. Asanteni sana kwa ushauri huo mwanana.

mkuu shida kubwa ni kwenye masoko wateja wengi wasembe ni watu wanaohitaji mzigo kwa kukopeshwa na waswahili bado hatuna utamaduni wakulipa kwa wakati wenye maduka ya jumla wanapenda kukopa hawalipe cash inabidi uwe na mtaj mkubwa kidogo kg ya mahindi ni sh 570/= kwa gunia moja ni sh 60000/=

Wana JF wataalamu wa biashara na wale walioshawahi kuifanya biashara ya mashine ya kusaga naomba mnijuze inalipa?au itakua ni kupaka hewa rangi?na mashine ya kusaga na kukoboa zinapatikana wapi na bei yake ni shilingi ngapi?Na umeme wake ni wa phase ngapi?
Nina kasehemu kangu Goba nimejenga fremu za biashara kwa mbele nataka niweke mashine ya kusaga nyuma,naomba mnijuze kwa mwenye experience au idea.Natanguliza thanks.

mmmnh,,,,,,,hapo kwenye bluuuuu.......nifafanulie

TANESCO watakufungia mita mpya ambayo readings zake ni kule HQ yao, hivyo you will get the bills from HQ no kuchakachua, ni kama LUKU. Ongea na TANESCO!!!!!!!!!

kudadadeki,,,,,lakini bado wanaibiwa kupitia DOWANS

Wengi tumeelimika na eimu hii mliyoitoa, nimekopi posti zote nyeti katika hii thread ili zinisaidie kupanga vema biashara hii. Asanteni sana kwa ushauri huo mwanana.

binafsi nimejifunza meeeeengi,ntaipeleka hii biashara somewhere

Wana JF wataalamu wa biashara na wale walioshawahi kuifanya biashara ya mashine ya kusaga naomba mnijuze inalipa?au itakua ni kupaka hewa rangi?na mashine ya kusaga na kukoboa zinapatikana wapi na bei yake ni shilingi ngapi?Na umeme wake ni wa phase ngapi?
Nina kasehemu kangu Goba nimejenga fremu za biashara kwa mbele nataka niweke mashine ya kusaga nyuma,naomba mnijuze kwa mwenye experience au idea.Natanguliza thanks.

URENI, nimependa sana wazo lako ni michango ya wana JF kwa ujumla. Ni wazo zuri sana, maana naona CApital yake ni ya kawaida, ukilinganisha na RETURN (KIPATO) inayopatikana. Ningependa pia kujua FEEDBACK yake katika mambo yafuatayo, ili na mimi nione uwezekano wa kuondoa UMASKINI kupitia dirisha hilo, maana eneo ninalo;-

1. nisaidie kujua gharama halisi za MOTA 25 - 30 HP kwa sasa na wapi zinapatikana na niza nchi gani ambazo ni nzuri.

2. Gharama za kununua kinu cha Kusaga namba 75 - 100 ni Tsh, Ngapi?

3. Gharama za kinu cha kukoboa cha Rola 3 ni Tsh, ngapi?

4. KAMA kuna gharama nyingine ambazo naweza kukutana nazo wakati wa kuaznisha mradi pia nijulishe ili niweze kuzielewa.

Katika maelezo yangu, Nimeunganisha michango ya wadau mbalimbali wa JF.

Nasubifi toka kwako.

Wengi tumeelimika na eimu hii mliyoitoa, nimekopi posti zote nyeti katika hii thread ili zinisaidie kupanga vema biashara hii. Asanteni sana kwa ushauri huo mwanana.

Shukrani sana kwa aliyeanzisha post hii,mbarikiwe wote mliochangia na kusoma kupata njia ya ujasiliamali

Habari wapendwa,
Naombeni mnisaidie mwongozo nataka kuanzisha mradi wa mashine ya kusaga nakukoboa nafaka, gharama zake nizipi? uendeshaji wake?

Je, biashara hii inaweza kunitoa kimaisha? nimetenga chumba kimoja nyumbani kwangu ndo nitawekeza humo mradi huo, natanguliza shukrani wapendwa

1. Mashine ya kusaga unga wako wewe ili uweke kwenye mifuko uuze au unasagia watu wanalipia huduma hiyo?!!

2. Angalia soko na wanunuzi endelevu au hapo unapoiweka tabia ya watu unaoishi nao je, ni wa kipato cha kati au vipi, watu wengi kwa sasa wananunua unga dukani kuliko kubeba mahindi kwenda kusaga, angalia sehemu unayokaa na wateja unaowalenga.

3. Kukutoa au kutokukutoa inategemea na malengo yako, mtaji, mipango kazi, uelewa wako wa soko, timu yako utayofanya nayo kazi, aina za mashine utazotumia, usimamizi wako n.k. . . .Biashara inataka nidhamu ya hali ya juu sana nabkubadilika kutokana na soko na washindani wako.

4. Umeamua kuweka chumba katika nyumba hiyo hiyo au unapoishi umejenga vhumba pembeni maalum kwa kazi hiyo??!!. Kusaga ni kazi ya vumbi na ina kelele, sio salama sana kuweka katika nyumba hiyohiyo. . nadhani hata maandalizi ya msingi wa mashine ni tofauti na nyumba ya kuishi

Kila la kheri. . . .

mkuu siku nyingine, kabla y kuweka uzi, jaribu kutafuta kwanza nyuz za nyuma, utapata watu wameshajadili hayo mambo. so usiwe na akiri kama za ccm

mkuu siku nyingine, kabla y kuweka uzi, jaribu kutafuta kwanza nyuz za nyuma, utapata watu wameshajadili hayo mambo. so usiwe na akiri kama za ccm
Kama hauna msaada wa kumpa mtoa mada ungesepa tu badala ya kumkashifu! Sasa wewe nyumbu ndiyo una akili kuliko ccm?

Back
Top Bottom