Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake

Unga unashida gani kwenye kuuza ndg yangu?nilishawahi kuwa agent wa kiwanda fulani kilichokuwepo maandazi road karibu na veta nakumbuka nilikuwa nauuza kweli kweli
Msosi in general hauwezi kukosa soko. Ishu kubwa ni sehemu ya kuweka bidhaa husika
 
Mkuu, mashine yako ya packaging bado ipo? ni model gani? Nami nahitaji sana ili kufikia mwisho wa mwaka huu nianze kazi.
 
Hii biashara inaonekana ni kimeo, watu wakishaanza wanapotea kimya kimya.
Mkuu, unaposikia neno biashara, jua biashara ni kazi kama kazi zingine na inahitaji dedication na knowledge (kwa kusoma au uzoefu) kama zilivyo biashara zingine.

Biashara yoyote ukiingia kichwa kichwa kwa kusikia story za watu bila kuwa na taarifa sahihi pamoja na self drive/passion inakula kwako.
 
Na feedback inaleta matunda sana kwa sisi ambao tuna ndoto za baadae
 
Nimefanya hii biashara kwa miaka kadhaa.Ni biashara nzuri sana.Kinacho 'matter' zaidi ni location.Ukipata location nzuri kwa siku moja unaweza kwenda mpaka units 60,70 na zaidi.Kwa wastani unit moja ni Sh 1350.Uzuri wa hii biashara ni kwamba sio pasua kichwa.Haina usumbufu mwingi wa maintenance.Zaidi sana labda kubadili chekeche,oil na mikanda tena inaweza kuwa mara moja tu kwa mwaka.
 
Mkuu, unaposema unit, unamaanisha ni unit za umeme?
 
Biashara nzuri sana hiyo,jamaa yangu kaacha kazi serikalini,anakomaa kuuza unga,anasaga halafu anapaki,aisee anapata hela sana.
 
Kiongozi, umewahi kufanya biashara na taasisi za kibongo? Unawauzia huduma yako leo, wanakulipa baada ya mwaka mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…