Salute, mwezi wa pili nataka nijaribu kufanya biashara ya mayai ya kienyeji kutoka Singida hivyo kwa wazoefu wa hizi mambo kule Singida vijijini bei za tray za mayai zinauzwaje na changamoto zipi nijiandae nazo asanteni.
Yaani uhalisia wa mawazo na kufanya huwa tofauti kabisa, wengi wanawaza lakini naona bora kufanya tu...... Hapa Mara aje mtu aseme amna faida nani anajua wateja wanatokeaga wapi na siku gani kwenye utachojaribu kufanya.
Mayai ya kienyeji yana faida shida yake moja ymtu yanaharibika fasta so useme utoe singida uje uuze dar ni haiwezekani pambana ufuhe kuku hadi watage ukiweza pata matetea 50 hadi 70 hukosi hela ya kula