Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake


Malila unaweza nijuza mbagala na aroma maeneo gani yenye miche ya mitiki, nataka ninunue kama mia mbili hivi.
 
Malila unaweza nijuza mbagala na aroma maeneo gani yenye miche ya mitiki,nataka ninunue kama mia mbili hivi.

Ukifika Tabata Aroma, iko pembeni kulia kwako kama umetoka mjini kwenda Segerea. Miche yao mingine ipo Kinyerezi mwisho wa lami.Bei ni Tsh 1000/ ni miche yenye ubora ukilinganisha na Mbagala.

Ukifika Mbagala inapoishia dabo ROAD mpya, unaanza mtelemko kwenda Kongowe, kabla hujavuka daraja, unaingia mkono wa kulia, mita kama mia hivi ndani, acha maua yaliyopo barabarani, fuata hicho kinjia.Bei ni Tsh 500/ ila ubora wake kama shamba halina unyevu wa kutosha ni mdogo.
 

Ok nitaenda huko! Thanx.
 
Vipi kuhusu soko la mbao dar? Nachotaka kujua ni kuhusu soko kama ni kubwa.
 
Ahsante kwa kutumotivate. Nitakutafuta kwa msaada zaidi.
 
Mkuu malila nilikuwa naomba kujiunga na umoja wenu wakibihashara hasa wakupanda miti je nitafanyaje!
Tafadhali naomba unijibu!
 
Mkuu malila nilikuwa naomba kujiunga na umoja wenu wakibihashara hasa wakupanda miti je nitafanyaje!
Tafadhali naomba unijibu!

Karibu sana,
Hakuna kiingilio kabisa, cha umuhimu ni uaminifu wako tu, nipe mail yako kupitia pm ili tuanze mawasiliano ya moja kwa moja.
 

Mkuu huu ushauri wako na ulichokifanya nimekipenda na ntatekeleza kwa kukuiga ili kudumisha ushauri wako
 
Vipi kuhusu soko la mbao dar ? Nachotaka kujua ni kuhusu soko kama ni kubwa

Kwa kweli soko la mbao ni kubwa sana hapa hapa nchini na nje ya nchi. Kwa sasa mbao za Tanzania zinauzwa Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini, Somalia hadi uarabuni. Ukitaka kujua ukubwa wa soko hili nenda Morogoro uhesabu malori yanayoleta mbao kutoka nyanda za juu kusini. Mbao nyingine zinatoka mpaka Malawi.

Kwa maoni yangu soko la mbao litazidi kupanuka ingawaje uzalishaji kwa miaka kadhaa ijayo utakuwa chini kutokana na kuisha kwa miti hasa huko vijijini. Hivyo bei itazidi kupanda na siyo kushuka. Mahitaji ya mbao yatazidi kwenda juu kwani wengi siku hizi wanajitahidi kujenga nyumba bora, mpaka huko vijijini. Mbao za asili kama mninga, mvule, n.k haziwezi tena kutumika kwenye kazi za kuezekea majumba kutokana na bei zake kuwa kubwa mno.
 

Mkuu mninga unachukua muda gani mpaka kuuvuna? Mimi huwa naiona vijijini lakini nikiuliza una umri gani huwa sipati majibu yenye uhakika. Mninga ni utajiri.

Pia niliona kwenye maonesho ya kilimo mwaka fulani. Kuna gereza moja huko kilimanjaro wanatengeneza furniture (nyeupe) nzuri sana kwa kutumia muarobaini.
 

Mninga/Mvule ili uvunwe unahitaji miaka isiyopungua sabini. Kwa hiyo ukipanda wewe atavuna mjukuu wako.
 
Jamani maeneo ya chalinze -- lugoba ni miti gani inastawi vizuri.

Maeneo yale ni makame sana, miarobaini inaweza kustawi ila jamii nyingine ni ngumu sana kukua kibiashara. Kama unaingia Chalinze ukitokea huku Dar, kuna mitiki upande wa kushoto, ipo na haiongezeki kimo wala unene. Sijui Msederela kama unaweza kumea na kukua kibiashara.
 

Hivi miarobaini inafaa kwa mbao? Mbona kama vile huwa haikui sana kwenda juu?
 
Hivi miarobaini inafaa kwa mbao? Mbona kama vile huwa haikui sana kwenda juu?

Miarobaini inatoa mbao nzuri sana. Sasa kama mnazi unachongwa mbao, itakuwa muarobaini. Waulize mafundi fenicha mjini Dar wakuambie miguu ya makochi na vitanda iliyobora kabisa wanachonga mti gani.
 


Wenger...!!! Nadhani wewe tunaweza kwenda pamoja jamaa yangu, Ebana unaweza kunidokeza kidogo acre moja maeneo ya huko inauzwaje...???/

 
Mninga/Mvule ili uvunwe unahitaji miaka isiyopungua sabini.Kwa hiyo ukipanda wewe atavuna mjukuu wako.

miaka 70! sipo tayari kwa hili. Ngoja niendelee kufanya utaratibu wa kumiliki ardhi kisheria maana hizi projects za muda mrefu ni lazima uwashirikishe watu wa ardhi kikamilifu kabla ya kuanza kupanda miti. Tuliangalie kwa umakini hili swala, watu wengi wamepoteza ardhi kwa kutofuata taratibu za umiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…