Asante KVM,
Nichangie kwa kuleta nyongeza za hapa na pale ili kujazia mjadala wetu. Maeneo ya kupanda miti yaliyosahaulika ni Kilolo, Mfindi,Mby vijijini, Makonde plateau.
Tumetaja sana pines, cyprus, teak,eucalyptus, tumesahau acrocarpus kwa ukanda wa baridi na Msederela kwa kanda za joto kiasi.
Hatujazungumzia mbegu, mbegu bora za Pines kwa sasa ni Tatizo sugu.Tangu mwaka jana kituo cha Iringa wameshindwa kuzalisha, kwa hiyo pines/cyprus zinaandaliwa kienyeji na vijana huko vijijini.Kwa sasa pines za uhakika zinapatikana Nairobi, ila bei imesimama.
Mwaka jana tulipata taabu sana ya tubes, ila mwaka huu walau zipo pale TFA Iringa, bei iko juu. Ukiwa na usafiri wako, ni bora kununua Dar ukasafirisha. Dar ni Tsh 5000/ kwa kilo na TFA Iringa ni 6500/ kwa kilo.
Ili kupunguza gharama za kitalu, watika miche mapema, miezi mitano kabla ya msimu wa kupanda haujafika.
Kama unataka ardhi kubwa,Makete usiende, ni kazi ngumu kupata eka 50 za pamoja zinazofikiwa na miundo mbinu. Utapanda milimani ambako utashindwa kuvuna. Na maeneo mazuri yaliyobaki bei iko juu. Ludewa/Wino/Lupembe/Mfindi kusini huko bei poa.Kilolo bei inaanza kupanda.
Kwa wale wanaonunua miti na ardhi, wawe waangalifu, vijijini unaweza kuta miti ni mtu mwingine na ardhi ni ya mtu mwingine.
Asante, tuendelee kukata issue.