Biashara ya mbuzi

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
23,265
Reaction score
17,120
Wadau,

Niko katika utafiti awali wa biashara hii(huswa mbuzi) na hivyo naomba wenye mawazo nayo wanisaidie tafadhali hususani katika nyanja hizi:

  1. Aina za mbuzi wanaofaa
  2. Risks
  3. Ushindani na fitina za biashara hii
  4. Taratibu za kisheria
  5. Usafirishaji
  6. Masoko
Shukrani
=========



Ili kufanya biashara ya viembe hai ikiwemo mbuzi mfanyabiashara anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
  • 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 62,000/-
  • 2.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA kinatolewa bila malipo
  • 3.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA
Mfanyabiashara mwenye viambatisho husika atapewa Leseni ya kufanya biashara ya Mifugo ndani ya Mkoa husika. Leseni inatolewa na Ofisi ya Biashara ya Halmashauri kwa malipo ya kuanzia shilingi 80,000 na kuendelea kulingana na ada iliyopangwa na Halmashauri Husika.

Biashara ya mifugo ndani ya nchi

Mfanyabiashara anayefanya biashara ya mifugo ndani ya nchi yaani katika minada ya awali, upili na mipakani anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
  • 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 62,000/-
  • 2.Mkataba wa kupanga ofisi
  • 3.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA ambacho kinatolewa bila malipo
  • 4.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA
Mfanyabiashara mwenye viambatisho husika atapewa Leseni ya kufanya biashara ya Mifugo ndani ya nchi kutoka BRELA kwa malipo ya shilingi 200,000.

Endapo atahitaji huduma nyingine BRELA kama vile
  • 1.Kusajili jina la biashara atalipa kiasi cha shilingi 22,000
  • 2.Kusajili Kampuni malipo yatategemea na kiwango cha mtaji wa biashara ambayo yanaanzia shilingi 160,000 hadi 720,000
Biashara ya mifugo kutoka nje ya nchi

Mfanyabiashara anayefanya biashara ya mifugo nje ya nchi yaani kutoka minada ya mipakani kwenda nje ya nchi anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
  • 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 152,000/-
  • 2.Mkataba wa kupanga ofisi
  • 3.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA kinachotolewa bila malipo
  • 4.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA
Mfanyabiashara mwenye viambatisho husika atapewa Leseni ya kufanya biashara ya Mifugo nje ya nchi kutoka BRELA kwa malipo ya shilingi 300,000.

Endapo atahitaji huduma nyingine BRELA kama vile
  • 1.Kusajili jina la biashara atalipa kiasi cha shilingi 22,000
  • 2.Kusajili Kampuni malipo yatategemea na kiwango cha mtaji wa biashara ambayo yanaanzia shilingi 160,000 hadi 720,000
Jinsi ya kuchagua mbuzi bora anaefaa kwa biashara

Zingatia sifa hizi, mbuzi awe-
  • Mchangamfu wakati wote, macho mang’aavu huku mkia na masikio vikimsaidia kufukuza inzi.
  • Kula na kucheua, kunywa maji vizuri kila siku.
  • Kuonyesha ushirikiano na kutembea pamoja kwenye kundi.
  • Mwili wake una uwezo mkubwa wa kukibadili chakula anachokula kutoa mazao ya kutosha kama vile maziwa.
  • Anaonekana mwenye nguvu na kwa wale wanaoendelea kukua wanaongezeka uzito kwa muda mfupi.
  • Ngozi ya mnyama husisimka mara kwa mara wadudu wapomtambaa
  • Kwa madume, huwa wana hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto.
  • Pua na midomo huwa na unyevu unyevu wakati wote.
  • Ngozi kuwa na ulaini unaotakiwa na manyoya hung’aa.
  • Kwa kawaida unapo mkaribia mnyama endapo amekaa chini ni lazima atanyanyuka.
Soko la mbuzi

Biashara hii unaweza kuifanya kwa njia mbili, kuuza mbuzi hai au kununua na kuchinja mbuzi kisha kuuza nyama.

Katika mradi huu unatakiwa kuwa makini kwenye usimamiaji wa mradi huu wa mbuzi, hakika matunda yake utayaona ndani muda mfupi sana.

Soko la mbuzi ni kubwa na liko wazi. Kwa Dar es salaam soko la mbuzi liko kwenye mnada wa mbuzi wa Vingunguti na Pugu. Kwa Dodoma Soko la mbuzi liko kwenye minada ya Msalato, Kizota, Hombolo, Mpunguzi, Vikonje pamoja na machinjio ya kisasa ya TMC.

Kwa mikoani soko la Mbuzi liko minadani. Hata ukiwa na mbuzi wangapi ukiwapeleka tu mnadani utawauza wote na kwa bei ya ushindani. Lakini vilevile kama unaweza kuunda kampuni yako, unaweza kusafirisha nyama ya mbuzi mwenyewe kwenda kwenye nchi za Dubai, Iraq, Kuweit, Oman na Falme za kiarabu. Vilevile unaweza kuwapeleka Somalia.

Changamoto ya biashara
  • Kununua mbuzi wenye magonjwa na hivyo kusababisha kifo au kuingia gharama ya kumtibu.
  • Kukosabei ya uhakika maana biashara hii hutegemea mnadani bei ikoje
  • Kwa wale wanaouza nyama ikikosa wateja hulazimika kuweka kwenye majokofu na hivyo kupoteza uthamani wake na kulazimika kuuza kwa bei pungufu.
Wadau wanaotaka kufanya biashara ya mbuzi

----

Michango ya wadau

----
 
Habari zenu wadau, nataka nijitose kwenye uuzaji wa mbuzi , kwani nimeona soko lipo, kikubwa nitakua naenda kuwachukua vijijini na kuwauza mjini.

Kwa mdau yeyote anaefahamu changamoto ya hii biashara, au hata tahadhari kwa hii biashara, anifahamishe wadau.
 
Wakuu habari zenu,

Wakuu nina mil kumi nataka kiufanya hii biashara ya mbuzi naomba msaada wenu wa mawazo sina huzoefu, je natakiwa kuwa na leseni ya biashara au kibali cha kusafirisha mifugo tu kinatosha wakuu nakaribisha mawazo zaidi na upeo mkubwa zaidi.
 
Da mimi mwenyewe niko na hela, nilikuwa nafikiria biashara kama hio, sema ndo sina uzoefu, kama una uzoefu call me on 0767328063 man, nitasaidia kupata habari zaidi.
 
Nenda Pugu mnadani utapata taarifa kamili pale.
 
Wakuu njooni uku mawazo yenu muhimu sana mbona kimya au wengi hamna uzoefu na hii kitu.
 
Unategemea kununua kwa bei gani na kuuza kwa bei gani?
 
Habari za muda huu samahani wadau naomba kwa anayefahamu anisaidie taarifa zifuatazo ili kupambana na hali ya maisha badala ya kulalamika

Napenda kujua
-upatikanaji wa mbuzi hasa mikoani yaani mkoa gani una mbuzi wengi na bei za huko
-usafirishaji wake
-masoko yake kwa Dar es salam
Mimi Niko Dar es salaam tusaidiane wadau mawazo ya Biashara
 
Yaani kaktika watu wavivu wewe ni namba moja. Uko Dar hujui hata masoko ya mbuzi yako wapi! Itakuwa ngumu sana kusaidia mtu kama wewe.

Ili kukusaidia, fanya utafiti ujue kwa Dar soko olikoje ukisha pata jibu, njoo nitakuelekeza maeneo ambayo unaweza kununua mbuzi hadi kwa elf 15
 
Soko kwa Dar lipo Vingunguti
Vingunguti hapawezi pale...lugha ya wauza mbuzi pale hadi anaambiwa mnunuzi huyo mbuzi hana maini au anae kuuzia ana ukimwi [emoji4] akiwa fyatu atapaweza! Na wizi upo kidigitali ukitangaza nimeibiwa unajitangaza wanakuona wa analogia ndipo utaibiwa zaidi [emoji38]
 
Kwa hiyo soko zuri ni wapi?
 
Sinumesema ni wezi sana hapo
Na wewe ukifuzu mila na desturi soko utaiba tu hakuna laini laini kama unauza kahawa [emoji38]mwanzo wowote sio lele mama lazima uwe fyatu [emoji38]
 
na wewe ukifuzu mila na desturi soko utaiba tu hakuna laini laini kama unauza kahawa [emoji38]mwanzo wowote sio lele mama lazima uwe fyatu [emoji38]
Vipi bei zimekaa je?
 
Sasa mimi soko la Dar nitakusaidiaje? Tuma pesa huku kwetu MEATU nikununulie mbuzi mmoja unaweza kumpata kwa bei ya kati ya 30-50 elfu! Commission yangu itakuwa bei gani? usafiri ni fuso na bei ni mawelewano!
 
Ndugu zanguni nashukuru kwa ushirikiano naomba tushirikane zaidi naomba niulize tena maswali na hii ni baada ya kufanya utafiti Leo nakukutana na mchoma nyama ya mbuzi naomba kusaidiwa yafuatayo

-Mbuzi dume mkubwa kwa mliiofika mnadani anauzwaje?
-Je kuna tofauti kati ya mbuzi wa nyama ya kuchoma na yule wa supu?
-Kwa kawaida mbuzi mkubwa huwa na kilo ngapi kiwango cha juu?
-Ukubwa wa mbuzi hutofautiana kati ya sehemu na sehemu namaanisha nasikia mbuzi wa handen ni wadogo wadogo sana je maeneo gani ni wakubwa na hupendwa kwa Biashara

-Usafirishaji wa mbuzi kutoka mkoa HADI DSM ni kias gani kwa mmoja na je magar ya kusafirisha hao mbuzi yapo ya kutosha

Naombeni wadau mnisaidie kiukwel taarifa kwa mnaojua na kiukwel natambua changamoto za baadhi ya wenzetu ambao huchangia kwa kuponda naheshimu mawazo ya kila mdau na kwangu na wengine ni darasa tosha tujenge MOYO wa kusaidiana hasa tunapohitaji mbinu za kujikomboa kibiashara nawakaribisha pia inbox kwa mawazo ya kujenga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…