Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,120
Wadau,
Niko katika utafiti awali wa biashara hii(huswa mbuzi) na hivyo naomba wenye mawazo nayo wanisaidie tafadhali hususani katika nyanja hizi:
=========
Ili kufanya biashara ya viembe hai ikiwemo mbuzi mfanyabiashara anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
Biashara ya mifugo ndani ya nchi
Mfanyabiashara anayefanya biashara ya mifugo ndani ya nchi yaani katika minada ya awali, upili na mipakani anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
Endapo atahitaji huduma nyingine BRELA kama vile
Mfanyabiashara anayefanya biashara ya mifugo nje ya nchi yaani kutoka minada ya mipakani kwenda nje ya nchi anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
Endapo atahitaji huduma nyingine BRELA kama vile
Zingatia sifa hizi, mbuzi awe-
Biashara hii unaweza kuifanya kwa njia mbili, kuuza mbuzi hai au kununua na kuchinja mbuzi kisha kuuza nyama.
Katika mradi huu unatakiwa kuwa makini kwenye usimamiaji wa mradi huu wa mbuzi, hakika matunda yake utayaona ndani muda mfupi sana.
Soko la mbuzi ni kubwa na liko wazi. Kwa Dar es salaam soko la mbuzi liko kwenye mnada wa mbuzi wa Vingunguti na Pugu. Kwa Dodoma Soko la mbuzi liko kwenye minada ya Msalato, Kizota, Hombolo, Mpunguzi, Vikonje pamoja na machinjio ya kisasa ya TMC.
Kwa mikoani soko la Mbuzi liko minadani. Hata ukiwa na mbuzi wangapi ukiwapeleka tu mnadani utawauza wote na kwa bei ya ushindani. Lakini vilevile kama unaweza kuunda kampuni yako, unaweza kusafirisha nyama ya mbuzi mwenyewe kwenda kwenye nchi za Dubai, Iraq, Kuweit, Oman na Falme za kiarabu. Vilevile unaweza kuwapeleka Somalia.
Changamoto ya biashara
Michango ya wadau
Niko katika utafiti awali wa biashara hii(huswa mbuzi) na hivyo naomba wenye mawazo nayo wanisaidie tafadhali hususani katika nyanja hizi:
- Aina za mbuzi wanaofaa
- Risks
- Ushindani na fitina za biashara hii
- Taratibu za kisheria
- Usafirishaji
- Masoko
=========
Ili kufanya biashara ya viembe hai ikiwemo mbuzi mfanyabiashara anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
- 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 62,000/-
- 2.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA kinatolewa bila malipo
- 3.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA
Biashara ya mifugo ndani ya nchi
Mfanyabiashara anayefanya biashara ya mifugo ndani ya nchi yaani katika minada ya awali, upili na mipakani anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
- 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 62,000/-
- 2.Mkataba wa kupanga ofisi
- 3.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA ambacho kinatolewa bila malipo
- 4.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA
Endapo atahitaji huduma nyingine BRELA kama vile
- 1.Kusajili jina la biashara atalipa kiasi cha shilingi 22,000
- 2.Kusajili Kampuni malipo yatategemea na kiwango cha mtaji wa biashara ambayo yanaanzia shilingi 160,000 hadi 720,000
Mfanyabiashara anayefanya biashara ya mifugo nje ya nchi yaani kutoka minada ya mipakani kwenda nje ya nchi anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:
- 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 152,000/-
- 2.Mkataba wa kupanga ofisi
- 3.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA kinachotolewa bila malipo
- 4.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA
Endapo atahitaji huduma nyingine BRELA kama vile
- 1.Kusajili jina la biashara atalipa kiasi cha shilingi 22,000
- 2.Kusajili Kampuni malipo yatategemea na kiwango cha mtaji wa biashara ambayo yanaanzia shilingi 160,000 hadi 720,000
Zingatia sifa hizi, mbuzi awe-
- Mchangamfu wakati wote, macho mang’aavu huku mkia na masikio vikimsaidia kufukuza inzi.
- Kula na kucheua, kunywa maji vizuri kila siku.
- Kuonyesha ushirikiano na kutembea pamoja kwenye kundi.
- Mwili wake una uwezo mkubwa wa kukibadili chakula anachokula kutoa mazao ya kutosha kama vile maziwa.
- Anaonekana mwenye nguvu na kwa wale wanaoendelea kukua wanaongezeka uzito kwa muda mfupi.
- Ngozi ya mnyama husisimka mara kwa mara wadudu wapomtambaa
- Kwa madume, huwa wana hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto.
- Pua na midomo huwa na unyevu unyevu wakati wote.
- Ngozi kuwa na ulaini unaotakiwa na manyoya hung’aa.
- Kwa kawaida unapo mkaribia mnyama endapo amekaa chini ni lazima atanyanyuka.
Biashara hii unaweza kuifanya kwa njia mbili, kuuza mbuzi hai au kununua na kuchinja mbuzi kisha kuuza nyama.
Katika mradi huu unatakiwa kuwa makini kwenye usimamiaji wa mradi huu wa mbuzi, hakika matunda yake utayaona ndani muda mfupi sana.
Soko la mbuzi ni kubwa na liko wazi. Kwa Dar es salaam soko la mbuzi liko kwenye mnada wa mbuzi wa Vingunguti na Pugu. Kwa Dodoma Soko la mbuzi liko kwenye minada ya Msalato, Kizota, Hombolo, Mpunguzi, Vikonje pamoja na machinjio ya kisasa ya TMC.
Kwa mikoani soko la Mbuzi liko minadani. Hata ukiwa na mbuzi wangapi ukiwapeleka tu mnadani utawauza wote na kwa bei ya ushindani. Lakini vilevile kama unaweza kuunda kampuni yako, unaweza kusafirisha nyama ya mbuzi mwenyewe kwenda kwenye nchi za Dubai, Iraq, Kuweit, Oman na Falme za kiarabu. Vilevile unaweza kuwapeleka Somalia.
Changamoto ya biashara
- Kununua mbuzi wenye magonjwa na hivyo kusababisha kifo au kuingia gharama ya kumtibu.
- Kukosabei ya uhakika maana biashara hii hutegemea mnadani bei ikoje
- Kwa wale wanaouza nyama ikikosa wateja hulazimika kuweka kwenye majokofu na hivyo kupoteza uthamani wake na kulazimika kuuza kwa bei pungufu.
----Habari zenu wadau, nataka nijitose kwenye uuzaji wa mbuzi , kwani nimeona soko lipo, kikubwa nitakua naenda kuwachukua vijijini na kuwauza mjini.
Kwa mdau yeyote anaefahamu changamoto ya hii biashara, au hata tahadhari kwa hii biashara, anifahamishe wadau.
Wakuu habari zenu,
Wakuu nina mil kumi nataka kiufanya hii biashara ya mbuzi naomba msaada wenu wa mawazo sina huzoefu, je natakiwa kuwa na leseni ya biashara au kibali cha kusafirisha mifugo tu kinatosha wakuu nakaribisha mawazo zaidi na upeo mkubwa zaidi.
Michango ya wadau
----Ndugu zanguni nashukuru kwa ushirikiano naomba tushirikane zaidi naomba niulize tena maswali na hii ni baada ya kufanya utafiti Leo nakukutana na mchoma nyama ya mbuzi naomba kusaidiwa yafuatayo
-Mbuzi dume mkubwa kwa mliiofika mnadani anauzwaje?
-Je kuna tofauti kati ya mbuzi wa nyama ya kuchoma na yule wa supu?
-Kwa kawaida mbuzi mkubwa huwa na kilo ngapi kiwango cha juu?
-Ukubwa wa mbuzi hutofautiana kati ya sehemu na sehemu namaanisha nasikia mbuzi wa handen ni wadogo wadogo sana je maeneo gani ni wakubwa na hupendwa kwa Biashara
-Usafirishaji wa mbuzi kutoka mkoa HADI DSM ni kias gani kwa mmoja na je magar ya kusafirisha hao mbuzi yapo ya kutosha
Naombeni wadau mnisaidie kiukwel taarifa kwa mnaojua na kiukwel natambua changamoto za baadhi ya wenzetu ambao huchangia kwa kuponda naheshimu mawazo ya kila mdau na kwangu na wengine ni darasa tosha tujenge MOYO wa kusaidiana hasa tunapohitaji mbinu za kujikomboa kibiashara nawakaribisha pia inbox kwa mawazo ya kujenga
Habar za muda wadau wa jamii forum heri ya mapumziko ya jumapili na Siku ya ibada pia
Nimejitokeza kwa mara nyingne tena kuuliza kwenu wadau ambao mshewahi kufanya Biashara hii ya mbuzi kwa DSM na hii inafuatia kufanya utafiti maeneo niliyopo na kukutana na maswali ambayo naomba msaada kwenu na nipo tayar kupokea changamoto zozote kutoka kwenu kwa kuwa naamin uwepo wenu humu unatusaidia kuweza kufikisha mawazo na mitazamo yetu sehemu ambayo hatuwez kufika kwa miguu yetu nakuomba unachokifahamu share ili tusaidiane
Naomba kuuliza yafuatayo
- ni maeneo gani kunapatikana mbuzi wakubwa wanaofaa kwa Biashara na bei zake zikoje ingawaje zinatofautiana na msimu
-usafirishaji kutoka huko kwa mbuzi mmojamoja ni kiasi gani na upokewaji wake hufanyikaje
-Bei ya kuuza mbuzi mmoja au jinsi anavyonunuliwa haswa na wadau wenye majiko ya nyama choma na bei hii nikimaanisha anavyouzwa mnadani na kwa MTU wa jiko
-kuna utofauti kati ya mbuzi wa supu na mbuzi wa nyama na tofauti ikoje
Karibuni wadau tupeane faida na tukomboane na hali ya maisha ya sasa