Nina mchele wa kulima mwenyewe nategemea kuvuna gunia 250 ambazo ni zaidi ya Kilo 15,000 elfu ambazo kimsingi nataka kuzifanya kama mtaji wa kuanzia biashara mjini Dar es salaam. Nimeshazoea kulima na kuuzia shambani kule kule sasa nataka frem niuze mwenyewe, pia wapo majirani zangu ambao wamekubali kunipa gunia zao zinazofikia 400 ili nizilete mjini kwa makubaliano ya kuwauzia na kuwapa fedha yao na mimi nibaki na cha juu.Jifunze mkuu niwe mteja wako dar huwa nahitaji walau mchele tani moja kwa wiki kwaaajili ya duka la rejareja
Nimeamua hivyo nikidhani kuwa nitapata faida kubwa na pia nitaifanya kazi kuwa endelevu badala ya kulima na kuvuna kisha unakaa miezi 6 kusubiri mvua tena.
Naomba ushauri na kama kuna mbinu nyingine.
Ahsanteni