Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Mkuu nnaomba uzoefu wako kama hutojali
Nafanya hii biashara na dream yangu ni kuwa na center za kutosha sababu binafsi Napenda Sana games ni nzuri Ukifanya kwa hobby Usitegemee faida mara moja inachukua muda mara pad mbovu,mara flash imeibiwa nk but Ukiweka sehemu nzuri Unapiga hela.
 
Ina uharamu gani hii biashara mkuu, maana hizi game hazina ngono, ulevi, ni kama kuenda uwanjan tu kucheza mpira.
Hahhaha mkuu umenifurahisha. Hakuna huruma mbele ya pesa halali japo hii inanusu halali nusu haramu. Mm pia najipanga kufungua maeneo flan karibu na shule na sitajali kelele zozote kwakweli
 
Kama toto lako zwazwa ni zwazwa tu, watoto wa madon wanazo play station sebuleni na ndio wanaoongoza kila mahala, unadumaza mwenyewe kwa kipigo na mlo mbovu unasingizia game.
 
Siku hizi wachimba cryptocurrency wamepandisha sana bei za Gpu, ila pc unakuwa na choice nyingi sana ya games na quality inakuwa kubwa kushinda console.
Mkuu hizi cypto unaweza nielekeza namna ya kuzichimba?
 
Mkuu hizi cypto unaweza nielekeza namna ya kuzichimba?
Kwa njia rahisi zaidi hii tutorial nzuri ina involve mambo matatu tu.
1. Kuwa na wallet yako
2. Kuwa na hardware (computer) nzuri
3. Software rahisi ya kuchimbia.


Ila mkuu siku hizi kuwa na computer tu moja ya kawaida then uchimbe inakuwa kama unajidanganya tu mwisho wa siku unapata 2000 na umeme wa 3000 umeenda.
 
Yani ndo hivyo uzuri wake,sababu pc ni inashughuli nyingi.

Ukiwa na pc yenye uwezo mzuri unacheza any game na quality inayoeleweka
Siku hizi wachimba cryptocurrency wamepandisha sana bei za Gpu, ila pc unakuwa na choice nyingi sana ya games na quality inakuwa kubwa kushinda console.
 
Siku hizi wachimba cryptocurrency wamepandisha sana bei za Gpu, ila pc unakuwa na choice nyingi sana ya games na quality inakuwa kubwa kushinda console.
Naomba unisaidie taarifa updated ya wazo lako ulilochangia 2017 la kichezesha games kwa PC ambayo ulikadiria gharama inafika 650K, Kwa sasa hivi gharama kwa desktop yenye monitor kuchezesha FIFA 19 unaweza kutoka ngap mkuu.
 
Hio biashara uwe karibu na sehemu yenye wanafunzi, mfano jirani na shule utapiga hela.
Kuna jamaa mmoja alifungua hii biashara karibu na shule huko Arusha, kumbe wazazi walikuwa hawapendi kutokana na madogo wanatoroka shule kuja kwake. Ilifika mbali wakaanza hadi udokozi nyumbani, jamaa akaundiwa zengwe anaonyesha video za ngono hivyo anaharibu watoto. Huwezi amini polisi walimfukuzisha jamaa lile eneo na vitendea kazi akaviacha mle mle kwenye fremu ya biashara.
 
Naomba unisaidie taarifa updated ya wazo lako ulilochangia 2017 la kichezesha games kwa PC ambayo ulikadiria gharama inafika 650K, Kwa sasa hivi gharama kwa desktop yenye monitor kuchezesha FIFA 19 unaweza kutoka ngap mkuu.
400k mpaka 500k bila kutumia dedicated graphics, hii ni kutumia intel hd 530 am 630 zilizopo kwenye 6th/7th gen ya processor za intel. ila uhakika zaidi ni 600k mpaka 700k kwa kuongezea Nvidia 1030 hapo. ukiongeza budget kuna vr games siku hizi pia, sema gpu itabidi upande kidogo angalau 1650 na utahitaji miwani ya mixed reality.
 
Hii Miwani ikoje?
 
Hii Miwani ikoje?
Inakuwa kama hivi


Unavaa kichwani na inakuwa na controller zake. Hizo controller sasa ndio zinageuka kuwa chochote inaweza kuwa racket kwenye game la Tenis, ikawa upinde na mshale,bunduki, panga etc

Best Headset ni za Oculus rift na Htc Vive sema bei ndefu zinafika 1m na kupanda, hizi windows mixed reality bei zake ni nafuu around dola 200 na kukiwa na offer unazipata chini ya hapo. Na pia hazihitaji power kubwa sana kuanzia 940mx nvidia unaweza tumia baadhi ya vitu vya vr.
 
Dah hii itakuwa ya ukweli sana aisee.

Lazima niitafute hii nikitulia
 
Na mkononi au mtumba ps3 naweza pata kwa ngapi mkuu.
 
Dah! Hapa naona ni heri kuchezesha tu ps3 max settings, huko kwenye PC max settings bajeti iwe vizuri.
 
How about ps4 seems like ps3 is old for this new generation unless maybe kwahapo bongo Ndio wamezoea hizo
 
Habarini wanajamvi,

Ebu niende moja kwa moja kwenye mada Mimi ni graduate na kama mnavyo jua saivi hakuna tofauti kati aliyesoma na asiye soma cha muhimu ni kujiongeza tu.

Katika kufikiria kwangu nikaona ni vema nipate maelezo juu ya hiii biashara kabla sijaingia kichwa kichwa vitu ninavyo itaji kujua

- Vifaaa vinavyo hitajika
- Gharama ya vifaaa ambavyo vinaitajika
- Namna gani ya kuvitumia
- Na technic mbalimbali za kuongeza faida

Kiufupi sina uzoefu ata kidogo na hii biashara ninacho jua mm ni kucheza tuuu napo baadhi ya magemu.

Naombeni msaada ili niweze kuendana na kasi ya hii ya awamu ya tano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa ps4 ndio ina deal. Game pendwa ni fifa. (Unaweza kuwa pia na ps3 ukaweka pes)
Ps4 unaipata around laki 4.5 hadi 7 kwa mtu. Dukani fat au slim ni 800k hadi mil1+.
Tv inch 32 ni laki 350k unapata.

So jumla tuseme:-
Frame 300k
Ps4 1 jumla lak 7+
Ps3 2 jumla lak 70k
Tv 32" 3 jumla laki 9 hadi mil 1+
Cd za games jumla 400k (au kama console zimechipiwa utaweza kuwekewa games kwa gharama nafuu)
Viti na meza laki 150000

Mapato:-

Ps4 dkk 10 mpira tsh 1000 au 500 kutegemeana na location yako.
Ps3 mpira 500

Kwa nusu saa unaweza toza 1000 au 2000 kutegemeana na location yako.

Mapato waweza ingiza 20000+ per day kama mzunguko upo.

So kwa kuanza mtaji hapo utaitajika kama mil 3 - 3.5 unaweza kuanza biashara
(Ingekuwa mimi kwa mil 3.5 ningeanzisha biashara ya kuonyesha mpira kwanza ambapo kwa baadae ndani pia ningefanya hiyo biashara ya games)

Kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…