Duh ebwana samahani.
Sijui kama umeshafanya maamuzi.
Tuconsider kila kitu kipo constant yaani bodaboda utafanya repair na ps controllers utazifanyia repair in a long run ps inakua better kwakua bodaboda itachoka ila siyo ps. Na bei ya bodaboda mpya inatosha kua na ps4, 3 na hata 2 kama unazipenda.
Isipokua kwa PS unatakiwa uwekeze kwenye location. Kama location utakaowekeza ni nzuri hata ps2 moja inatosha kukupa 10K mpaka 20K. Kuna mwaka nilipost kuuza ps2 humu kuna jamaa akanitafuta akaniambia tufanye exchange anipe simu nimpe game. Nikamkubalia, sikujua kumbe anatokea Moro mwaka huo nipo Dara, tukakutana tukamalizana.
Tukaja wasiliana akaniambia anatengeneza 40K to 60K per day. The reason ni kwakua hapo Moro alipo ni yeye tu alikua na game na mechi moja ni 500, wakati mimi (na Dar kwa ujumla) ps2 mechi moja ni 200.
So wekeza kwenye location na utaona bodaboda haina ishu.
Pia usiniaddress kama 'kaka'