simulizi za kweli
Member
- May 7, 2021
- 29
- 64
Biashara ya mtandaoni ni biashara yoyote inayotumia mtandao wa intaneti kuuza, kununua na kutangaza bidhaa au huduma.Kutokana na ongezeko la matumizi ya intaneti sasa hivi Duniani kote bidhaa mbalimbali zinauzwa, zinanunuliwa na kutangazwa kupitia mitandao ya kijamii na tovuti.Hapa nchini Tanzania kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya intaneti hasa kupitia simu janja biashara ya mtandaoni nayo imeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Juni, 2021 ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inasema Tanzania ilikuwa na watumiaji milioni 29 wa huduma za intaneti kupitia simu za mikononi, huku idadi ya laini za simu ikifikia milioni 53.1,pia asilimia 26 ya Watanzania milioni 60 walikuwa wanamiliki simu janja.Taarifa hiyo ilisema kati ya laini milioni 53.1 zilizosajiliwa kwa alama za vidole milioni 32.7 ndizo zinazotumia huduma za fedha mtandaoni.
Idadi hii kubwa ya watumiaji wa intaneti,simu janja na huduma za fedha mtandaoni imechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa biashara ya mtandaoni na kadri siku zinavyoenda hii biashara inaendelea kukua.
Picha kwa hisani ya mtandao wa Google ikionesha vifaa mbalimbali vinavyotumika kwenye biashara ya mtandaoni.
Faida ya biashara ya mtandaoni
i) Gharama zake ni za chini ukilinganisha na biashara ya kawaida,hakuna haja ya kupanga nyumba/chumba cha kufanyia biashara.Hakuna kulipa fedha za mlinzi,maji umeme nk.
ii) Biashara ya mtandaoni haina mipaka,mtu anayeuza vitenge Sinza (Dar es salaam) anaweza kuuza Dodoma,Mpanda au Msumbiji.Tofauti na yule anayeuza kawaida ambaye anakuwa anauza tu kwa watu wa eneo lake.
iii) Inaweza kuwafikia wateja wengi zaidi, ikilinganishwa na biashara ya kawaida.
iv) Mitandao imerahisisha kufanya matangazo,gharama ya kufanya matangazo ni ndogo,kumbuka usipotangaza usisubiri mteja.
v)Hii ni biashara inayofanyika kwa masaa 24, unaweza ukaifanya muda wowote na sehemu yoyote hata ukiwa shambani,darasani,kitandani nk.
vi)Unaweza ukaifanya bila ya kuwa na mtaji,mfano unaenda kwa mwenye bidhaa unaomba kupiga picha bidhaa zake(kwa makubaliano ya ukimpata mteja utaenda kununua kwake) kisha unazitangaza,kwahiyo ukipata mteja unaenda kununua na kumpelekea/kumtumia mteja bidhaa yake.
Changamoto ya biashara ya mtandaoni
Pamoja na faida tulizoziona ya kufanya biashara ya mtandaoni lakini kumbuka kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.Biashara hii inakabiliwa na changamoto zifuatazo;
i) Utapeli
Kwenye hii biashara kuna matapeli,na hawa wapo pande zote mbili za wauzaji na wanunuzi,kwa mfanyabiashara kamwe usijihusishe na utapeli kwani unaweza kudhulumu laki moja ukakosa kufanya biashara ya milioni.
ii) Kukosa uaminifu kwa wauzaji na wanunuzi,kuna wauzaji wengine siyo waaminifu,wanaweza kuuza bidhaa mbovu,zilizokosa ubora,zilizoharibika,kutuma mzigo pungufu na hata kutuma bidhaa ambayo hajaagizwa.Pia kuna suala la kubadilisha bidhaa mfano umeagiza gauni lenye rangi ya dhambarau unatumiwa lenye rangi ya damu ya mzee.
iii) Ucheleweshaji wa bidhaa
Imekuwa kawaida unalipia halafu mzigo hauupati kwa wakati.
iv) Kutopokea simu au kutopokea simu kwa wakati
Kwenye biashara ya mtandaoni mawasiliano ya simu ni muhimu sana lakini baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa na uzembe wa kutopokea simu au kutopokea kwa wakati,mteja hatakiwi kusumbuka kupiga simu.
v) Kutoweka bei ya bidhaa,kuna baadhi ya wafanyabiashara wakiweka matangazo ya bidhaa zao huwa hawaweki bei,mteja akiulizia bei anaambiwa njoo DM.
vi) Kubadilisha badilisha namba za simu na majina ya akaunti za mitandao ya kijamii.
vii) Kuweka bei kubwa ya bidhaa kuliko uhalisia
Bei ya bidhaa inayouzwa mtandaoni inatakiwa ifanane na ile ya mtaani.
viii) Kuweka gharama kubwa ya usafirishaji kuliko gharama halisi.Mtu anapanda dalala lakini anataka alipwe gharama ya bodaboda au bidhaa inatumwa mkoani lakini gharama za usafirishaji inaongezwa hii inasababisha bidhaa ipatikane kwa gharama kubwa na kukimbiza wateja.
ix) Wateja wasumbufu wasiotoa maelezo kamili sehemu walipo au wanahairisha kwa ghafla,wengine wanazima simu.
x) Picha za matangazo hazifanani na bidhaa utakayotumiwa yaani ubora unatofautiana.
Jinsi ya kutatua changamoto na mambo mengine muhimu ya kuzingatia:
i)Kila wakati na kwa kila jambo kuwa muaminifu, uaminifu ni nguzo kuu ya biashara ya mtandaoni.
ii)Omba radhi usipopokea simu ya mteja.
iii)Weka namba zako za simu wazi(zionekane kirahisi).
iv)Usibadilishe badilishe namba za simu au majina ya akaunti za mitandao yako ya kijamii.
v) Usibague mitandao ya kijamii,tumia yote,makampuni na mashirika makubwa Duniani kama Cocacola,Vodacom,CAF,FIFA,CNN, Walmart nk yana akaunti kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram nk.Baadhi ya wafanyabiashara utasikia wanasema kwa kujiamini kabisa kuwa "sina akaunti ya Facebook",ukibagua mitandao ya kijamii ni kubagua wateja,kila mtandao wa kijamii una aina yake ya wateja,itumie vizuri ili unase wateja wote.
vi)Weka bei zionekane wazi,siyo kusema njoo DM , baadhi ya wateja hawataki usumbufu wa kuanza kuulizia bei.
vii)Tumia pia tovuti kutangaza bidhaa zako,tovuti inarahisisha watu kukufahamua kirahisi,mtu akienda Google kutafuta bidhaa au maelezo ya bidhaa anakupata kirahisi.
viii)Sajili kampuni/jina la biashara ,ukishasajili fungua akaunti ya benki kwa jina la kampuni au jina la biashara na si jina lako mfano jina la akaunti ya benki isomeke Harid Hardware,vilevile sajili laini ya simu unayotumia kuwasiliana na wateja wako mfano anapokutumia fedha isomeke Harid Hardware na siyo Harid Juma,Hii itakufanya uaminike zaidi,mteja atajua kumbe anafanya biashara na mtu aliyesajiliwa na anayetambulika na serikali.
ix) Tafuta rangi nzuri zitakazopendezesha kurasa zako za mitandao ya kijamii.
x) Weka picha nzuri,kama huwezi kupiga picha zenye muonekano mzuri mtafute mpiga picha apige picha za matangazo ya biashara,picha ikiwa nzuri bidhaa itaonekana vizuri na watu wengi watavutika kuiangalia na kuifuatilia na vilevile picha ikiwa na muonekano mbaya mteja hatavutiwa na hiyo bidhaa.
xi) Maelezo ya bidhaa yawe mafupi,yenye lugha sanifu na yanayoeleweka kirahisi.Kamwe usikosee kuandika au usichanganye herufi mfano sehemu ya R unaweka L.
xii) Usichoke kutangaza bidhaa zako ni lazima uwe mvumilivu ,huwezi kutangaza leo na siku hiyohiyo uanze kupata Wateja. Pia unapotangaza bidhaa kuna watu watakuja kuponda bidhaa au bei ikitokea hivyo kuwa mvumilivu,usiwajibu vibaya.Puuzia kauli zozote za kukatisha tamaa.
xiii) Kuwa mwepesi kuomba msamaha hasa iwapo mteja hajaridhika na huduma au kachelewa kuipata.
xiv)Kama bidhaa imeisha,muombe mteja msamaha na mwambie itafika lini.
xv) Usichanganye akaunti ya mtandao wa kijamii ya biashara na mambo binafsi.
xvi) Lipa kodi kama biashara yako ina sifa ya kulipa kodi,sifa hizi ni zile zilizoainishwa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). Wafanyabiashara wengi wa mtandaoni wanaona hawastahili kulipa Kodi.Kulipa kodi ni ishara ya kukua kwa biashara.Kwa uataratibu wa TRA biashara yoyote yenye mtaji unaoanzia 4,000,000 inatakiwa kulipa kodi.Ukilipa Kodi na ukitambulika nchi inafaidika na wewe mfanyabiashara utaaminika zaidi.
xvii) Kuwa na lugha nzuri, mfanyabiashara wa mtandaoni ni lazima awe na lugha nzuri hata kama mteja ana lugha mbaya ,lugha za dharau na matusi,ni lazima uwe na kauli nzuri na uwe mnyenyekevu,mteja ni mfalme , mteja hakosei,huyo ni bosi wako kwa sababu anakufanya uishi. kwahiyo kamwe usijibu matusi,usimjibu vibaya mteja, vumilia kauli mbaya kwa sababu anayekutukana leo ndiyo mteja wa kesho.
xviii) Chukua fedha kabla ya kutuma bidhaa,hii itaepusha kutapeliwa na kusumbuliwa kulipwa.
xix) Fuatilia kama mzigo kaupata.
xx) Fuatilia maendeleo ya bidhaa uliyomtumia,hii inatengeneza urafiki/mteja wa kudumu na vilevile anaweza kukuunganisha na wateja wengine.
xxi) Muombe ruhusa ili uwe unamtumia picha za bidhaa mpya(kwa lengo la kumshawishi anunue)kamwe usimtumie bila ruhusa yake.
xxii)Toa ushauri wa bidhaa uliyoiuza au unayotaka kuiuza,mfano unaweza kumwambia mteja "hilo gauni linafaa livaliwe na viatu rangi nyeusi".
xxiii) Kuwa na tabia njema, muonekano mzuri kwenye mitandao na watu watakuamini lakini ukiwa una'post' mambo ya ajabu ajabu au umevaa vitu visivyoeleweka,wateja watalinganisha maisha yako binafsi na biashara yako.
xxiv) Karne hii ya 21 biashara ya mtandaoni inakua kwa kasi kwahiyo ni lazima ujifunze njia mbalimbali za kutangaza biashara yako, vilevile unaweza ukatafuta wataalam wa matangazo ya mtandaoni ili waweze kusaidia jinsi ya kupata wateja zaidi.
xxv) Mwisho tumia unachouza mfano unauza simu za Nokia lakini wewe unaonekana kwenye picha mtandaoni unatumia Samsung. Hii italeta picha kuwa bidhaa unazoziuza hazina ubora ndiyo maana wewe unayeuza huzitumii.
Nimetoa mchango wangu karibuni wengine kwa mjadala,wenye hoja na mawazo mbalimbali.Naomba pia mnipigie kura kwa wingi.

Upvote
2