Disruptor1
Senior Member
- Aug 9, 2022
- 139
- 388
Sio kwa ubaya na wala sipo hapa kusema anachokifanya ndugu mwalimu ni kitu kibaya lakini nataka niwakikishie hii sio njia sahihi ya kujifunza biashara ya nafaka.Hapa mtaishia kujifunza baishara na kilimo cha makaratasi.
Biashara ya nafaka na kilimo zinahitaji muhisika anaetaka kupata maarifa atoke alipo aingie field kwa vitendo na atajifunza siri zote za hii mambo.
Kuna umafia,ujanja ujanja,mbinu na vitu vingi sana kuanzia kijijini kwenye kubeba mazao,njiani kwenye kusafirisha hadi kwenye masoko unakouza hizi bidhaa ambapo huwezi kujifunza hivi vitu hotelini kijana.Itakuhitaji kwanza ujenge ukaribu na wazoefu wa hizi mambo wanaofanya kwa vitendo kila siku ndo utajua na kuelewa na itakuchukua muda fulani.
Hapo hotelini mtaishia kucalculate,mfano nimebeba gunia 100 za mahindi na kila gunia ina kilo 100 na kila kilo ina napata faida 200 aloo kwanza hizo hesabu zako zinaweza kupotea siku ya kwanza tu umebeba mzigo ukiwa pale mzani wa makambako.
Siku mkiwa tayari kujifunza kwa vitendo karibuni huku kusini mwa Tanzania kuna mkoa unasifika kwa kulima mahindi sana niwape hata geto la kufikia na kinglion ya kuwapeleka mashambani huko.