Biashara ya namna hii inawezekana

Biashara ya namna hii inawezekana

Magwero

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
243
Reaction score
75
KUULIZA SI UJINGA WASWAHILI TUNASEMA
natamani kufanya biashara , na fedha nilizonazo jumla kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo ni tshs 2,000,000/= tu.
katika biashara hii, natamani kupata faida ya tshs 200,000/= baada ya kuondoa gharama zote za biashara usika kwa mwezi.

kama ipo, msaada tafadhali
naomba kuwasilisha, nategemea mengi toka kwenu GREAT THINKERS
 
KUULIZA SI UJINGA WASWAHILI TUNASEMA........

natamani kufanya biashara , na fedha nilizonazo jumla kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo ni tshs 2,000,000/= tu.
katika biashara hii, natamani kupata faida ya tshs 200,000/= baada ya kuondoa gharama zote za biashara usika kwa mwezi.

kama ipo, msaada tafadhari.....

naomba kuwasilisha, nategemea mengi toka kwenu GREAT THINKERS

mtafute Kakobe
 
Nunua boda boda, ukimpa dreva analeta 70,000 kwa wiki. Kwa mwezi inakuwa 280,000.
 
tafuta line ya M pesa ajiri kijana eneo zuri katikati ya mji utapata zaidi ya 200000 kwa mwezi baada ya kutoa gharama
 
hiyo ni biashara nzuri mkuu, ila risk yake iko juu sana.....
hela yenyewe ndo hii,hii....
wakikapora si ntaweza zimia.............
 
katikati ya mji fremu ntalipa pesa ngapi ndugu yangu, bado line na simu.....
niongezee ujanja
 
Tafuta fremu sehemu yenye watu wengi.fungua cafe ya chips inalipa sanaaaa...mtaji kama laki NNE hivi unaweka mazaga ya kutosha...saladi mishkak ya ukwel.mayonize....utafurahi mwenyewe;;;;;;;;
 
hiyo ni biashara nzuri mkuu, ila risk yake iko juu sana.....
hela yenyewe ndo hii,hii....
wakikapora si ntaweza zimia.............

iko hivi kaka
risky business ndo siku zote zinalipa
kama unaogopa risk then nenda kanunue hisa za UTT na usubirie gawio mwisho wa mwaka.
 
Uko mji upi? Kama una nafasi fanya ufugaji wa kuku wa kisasa.......kwa Moshi vifaranga@ 1400,gharama ya kutengeneza banda la vyumba viwili vya 12ft by 12ft ni pungufu ya laki tano, chakula cha pellets ni mifuko kumi@54000tshs average kwa kila mfuko kwa kuku 200 na utaanza kuwauza wiki la nne/tano wakati wa joto au wiki la sita wakati wa baridi,bei ni 6000tshs kwa kila kuku na utaweza kupata mpaka 350000 faida kwa batch.
 
kanunue hisa za ABG au Kenya Airways (KA) au hat Precision Air (PAL) pale dse. Onana na moja wa broker kama,Orbit Securities
 
Back
Top Bottom