Biashara ya ndege haiwezi kuleta faida kabla pay back period haijafika

Kuna tofauti kati ya Cash flows na Profit & Loss Statement!
 

Mimi nadhani wewe hukumuelewa mwendazake. Alitwambia ndege tumenunua kwa cash! ndege tumenunua kwa hela zetu. Sasa hiyo payback period unayoisema ni ipi? Kama tungekuwa tulikopa na tunahitaji kurudisha mkopo ningekuelewa. Lakini kwa sasa hali ni tofauti.

In fact tuliambiwa kwamba tumepata faida ya billion 28 kwenye hizo ndege. CAG anatwambia tumepata hasara! Maybe mimi ndo kilaza sielewi.
 
Sasa hapo ndio unaonekana huna akili kumsema mnunuzi wa ndege kwamba kakosea. Umejaribu kufuatilia uongozi wa ATCL unavyofanya kazi? Don't conclude without formal analysis
 
Mimi sijakataa sijui mambo ya pay back,ishu ni kwamba tuliambiwa shirika linajiendesha kwa faida inayopatikana sasa iweje leo iwe hasara ,?
 

Hiyo return of investment kwa nani?
Alio kuambia ndege hizi tumekopa ni nani?
mapaka udai return of investment? Hizi ndege tumelipa cash kwa kauli ya Magufuli au ulikua humsikii akisema?
Kwa hiyo unapo iona ndege hapo akili yako itambue kua hiyo ndege ndio mtaji(capital) unapo izunguusha hewani akili yako itambue sasa mtaji una zunguuka. Inapo tua akili yako itambue sasa mtaji umetua unahesabu jumla ya ulichoingiza asila(actual) unalinganisha ulicho tarajia kuingiza kama kilicho ingia asilia ni kidogo kulinganisha na ulicho tarajia basi biashara yako hiyo umelamba hasara.
Na kama pato ulilo ingiza asilia litalingana na pato ulilo tarajia kuingiza umelamba faida

Beare in your mind there is no return of investment on your own capital.
 
Kulikuwa na mkataba wa atcl kulipa serikali kwa manunuzi ya ndege? Serikali imenunua, atcl ndio aendeshe biashara.
 
Una maanisha ku break even,
Anyway sikuelewi hata robo maana kama inaleta hasara means inatumia hela ambazo hazitokani na kujiendesha kuzirusha.

Sasa kama wewe ni mtaalamu sana basi nenda ATCL kwa mkurugenzi msaidie hayo unayofikiri ili atapoitwa mbele ya pilato aweze kujieleza
 
Longterm investment ina pay back period yake lakini kama haiperfom ni hasara.
Mfano jengo la bilioni 20 kuna kitu kinaitwa RRI inarange from 1-3%
Sasa kama estimation ya payback ya hyo 20b ni 10yrs halafu kwa mwezi hamkusanyi hala milioni moja na bado unafanya service jua ni hasara hata kama miaka hyo kumi ikiisha .
Ndicho wanaeleza CAG kuhusu ndege zetu
Weanzako wataka kuona faida tangia siku ya kwanza ndege kununuliwa wala hawataki kureason kisa ati hawakumpenda Magufuli.
 
CAG walifanya hesabu zote ndo wakaja na hyo hasara.
Usidhani wamekurupuka.
Ndege kama haileti kiasi kilichopangwa(return from investment) wangekujaje na hyo hesabu ya hasara
Hapo ndipo wanapokosea hata biashara za kawaida hazipo hivyo. Sasa yeye hiyo hasara anaipataje ndani ya hii miaka minne. ilitakiwa tupewe hesabu zinazoeleweka. Tueleze return of investiment imefika kiasi gani
 

Thobias Marandu youtube alieleza kwa kina kwamba ndege ni hasara tu hazina faida,ndege mpaka irudishe fedha inabidi urun kwa miaka zaidi ya 30 na uwe unafanya route daily kwenda na kurudi halafu ziwe full......Kwa taifa kufanya biashara ya ndege kwa kutegemea faida ni upuuzi....wawe na ndege chache kwa ajili ya kuleta heshima tu na si kibiashara yaani ni kama May weather anavyonunua ndege tu kwa matumizi yake.
 
Nadhani watu wanachanganya kati ya payback period na profit japo zinategemeana kiasi fulani...
Payback period is time it will take for an investment/project to recover its initial costs. Ambapo unachukua present values of projected cashflow(free cash flow after excluding operational costs in that period/year) less investment costs

Profit from accounting perspective is simply revenue less costs. Cost ya kununua hizo ndege haitokuwa sehemu ya operational costs except depreciation charge ya mwaka mzima kulingana na estimated useful life of hizo ndege...

Kama CAG anasema shirika linapata loss its obvious kwamba expenses are higher than profit.

The only relationship kati ya payback na profit ni kwamba zipo inversely related, the higher the profit the shorter payback period and vice versa is true
 
Kwamba hao walioposti hasara hawajui haya maswali yako??
 
Investment kama hii ya ndege kwa nchi kama Tanzania developing country faida inarud Pole Pole,watanzania wengi wanataka faida ionekane haraka ,in real term haiwezekan.napia kumbuken ndege zilinunuliwa kipind corona imeanza duniani ,kwaiyo kama ni hasara ni dunian kote.sio Tanzania tu..
 
Hayo maelezo aliyoyatoa ndio ambayo yalitakiwa sasa yaelezwe ili mtanzania aelewe, kwa mantiki hiyo tatizo halipo kwenye ndege tatizo lipo kwenye uongozi wa shirika, hapo ndio kwenye tatizo.
Acha kulaumu shirika na usimamizi wake. Tatizo lipo kwa aliyenunua ndege kwa mbwembwe bila kufanya analysis, wenzake wananunua ndege kwa mahitaji na malengo yeye alinunua kwa sifa. Hata umlete CEO wa Fly Emirates hapa ATCL haitokaa itengeneze faida hata miaka mitano ijayo.
 
Mleta mada una uwezo hafifu wa masuala madogo kabisa ya uchumi
Wewe ndio una uwezo hafifu wa maswala ya kiuchumi na ndio maana hata ukiambiwa utoe ushauri ATCL ifanyeje ili ipate faida utashauri ndege ziuzwe. Mtu mwenye akili ndogo hawezi endeleza asset bali huwaza ziuzwe. Na ndio maana afrika hawana viwanda, afrika hawana makampuni ni kwasababu ya kuwa na waafrika wenye uwezo mdogo kama wewe hapo. Mliuza viwanda vyetu vyote vilivyo jengwa na Nyerere, mliua shirika la ndege lilianzishwa na Nyerere, mliua shirika la reli likawa halifanyi kazi vizuri, mliua kila kitu, ili kila biashara mzishirikirie nyinyi tena hata kodi mkawa hamlipi, mtaka mfanye free business matokeo yake serikali ikakosa hata fedha za Kujenga madaraja na Kujenga na barabara nzuri, huduma za afya zilikua mbaya, kwasababu tu mlijibinafsishia kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…