Biashara ya nguo kwa mtaji wa Tsh. milioni 1

Mkuu Asante kwa ushauri
 
Ok ushaur wang kwann kwa pesa io usingeitumia yote na ukafungua duka online lets say kachukue nguo za watoto na kina dada kwa 200000 then unafanya matangazo unalipia hii inakulipa zaid na mm ndio biashara yangu ...mtu akitaka nguo unampelekea alipo ...na io pesa nyingine unaiweka huku ukiangalia upepo unaendaje ...yan ukiwa na laki 3 ..mbili mzgo na moja matangazo inalipa sana
 
Hongera nimependa bosi ,naskia ukiamka mapema hapo ni kugombania vibaya au inakuaje
 
Mkuu wewe uko Dar pia?
 
Nilikuwa nauzia iringa mkuu tena kama machinga tu..... Nguo wamazopenda binti wa dar kuanzia crop top had vile viskin vyote vinapatikana ilala boma kwa bei ya 1500-2500 kwa crop top na visweta vya kike vizuri skin ndo hiyo elfu 3-4
Asante sana Mkuu kuna swali hapo mdau kauliza huko ilala boma mzigo ni wa kugombania au ipoje?
 
Hongera nimependa bosi ,naskia ukiamka mapema hapo ni kugombania vibaya au inakuaje
hapana eio kugombania kihivyo ni kawaida tu mnaweza kuwa watu 7 belo linakatwa ukiwahi ndio umewahi.....pia kwa uzoefu wangu wanafungua belo saa 11 hivi maana mimi nilifika saa 9 nikasubiri hadi saa 11......ila ukiwahi sana kwenye hiyo saa 11 au 11 kasoro unaweza kuuliza anaefungua nguo unazohitaji alafu unamwambia nguo zote kali unaomba akuwekee utanunua wewe ukiwa pembeni wenzio wanashangaa unaona tu anakurushia nguo.... kama ni skin, vipochi vibegi vyote niliona watu wanafanya hivyo ni njia nzuri zaidi akikuzoea mara 2 raha sana utapata nguo kali sana bila kugombania.....
 
Kugombania mgoja nielezee vizuri.....mimi mfano nilifika sehemu nikakuta tayari muuzaji mmoja amezichambua so anachukua nguo mojamoja alafu unaiwahi kwa kumwambia akurushie bei hizo koti na visweta ilikuwa ni 1500 na 2000 ila watu hatukuzidi 7......

Kwenye skin jeans nilienda muuzaji nikakuta kazungukwa na watu 5 basi akitoa suluari anainyosha juu ionekane basi mtu ukisema naomba hiyo anasitisha shughuli analurusjia usipoipenda unairudisha anatangaza kwa wengine au anaiweka pembeni.....

Kuna skin jeans zinauzwa nje kuanzia saa 3 zile zinauzwa elfu 4 na elfu 5 ni nzuri ila zile ndio mnakua watu hata 50 na wauzaji wanakaa juu pale wanakuwa kama 10 hivi kama wanavyofanya mnadani napo ukiona fasta ukisema nirushie basi wanakurushia na hakuna kugombania kihivyo ni kuwahi tu ndio maana inabidi uione nguo nzuri kwa jicho la kwanza tu ili uiombe uiangalie vizuri .....

Ukiwa unaangalia vizuri basi utapata nguo kali bila hata kugombania na kuna sehemu mzigo hawafanyi mnada wanavibanda vyao wanafungua wanazipanga huko utakuta magauni makali elfu 2000.....
Hongera nimependa bosi ,naskia ukiamka mapema hapo ni kugombania vibaya au inakuaje
 
Siku gani wanafungua au ni kila siku
 

Afu wew @Karucee wew[emoji23][emoji23]
 
Cha kuzingatia uendane na mahitaji ya eneo lako ma wahitaji.....wanachuo unajua wanavyovaa unaweza kuwaletea nguo zote kuanzia za kwendea out hadi za kuvaa lecture room...... watu wazima magauni mazuri pia wananunua....

kwamfano kipindi hiki cha baridi kali unaweza ingiza mzigo wako wa koti za korea, ukawa unazimwaga pembeni ya vituo vikubwa kuanzia saa 10 ukauza kwa bei ya elfu 5 yale mafupi na makubwa ukauza elfu 7 kama umenunua kwa belo haitaziri laki 4 (350) ukiuza kwa bei hizo unapata mchanganyiko utauza sana na faida yake ni kubwa pia....

Pia unaweza ingiza zile pullneck sokoni kwa bei ya elfu 5 zinauzika mbaya.....na uzuri wa hizi bidhaa unaweza kuta wabush huko amekuja town anajumua karibu koti 60 hapo unampunguzia kutoka elfu 5 hadi 4000 ila faida inakuwapo.....

Au kipindi cha baridi unaweza ingiza stock za visocks virefu kwa watoto na wadada watu wazima au ukauza mizura kwa bei ya elfu 3 mmoja kama mizuri utaifurahia biashara
 
sema hizo koti kuna watu wanauza hadu elfu 20 au 25 ila mimi kuna msela wamgu alifungua november akawa anauza elfu 5 na elfu 7 sasa watu wanavyojaa hapo ni hatari na belo la hizi koti sio rahisi kukuta mbovu au ronya ni kuombea ukute ndefu nyingi maana ndio zinapendwa sana.....
 
Ndio MKUU. naona wapo bize na kulijenga TAIFA.
Pia mkuu unaweza fungua frame karbu na town au ukatengeneza kwa kutumia mbao na zile nailon ndefu (nimesahau jina) ukawa unauza mtumba tu utajaza sana.....kuna jamaa angu amefungua frame karbu na town amejaza nguo za laki 7 tu na ameweka vizuri chumba cha kupimia huwa anaweza laza parefu sana maana pindi nikienda mtembelea kwa masaa 2 anapata wateja 7 hadi 10 hapo 6 wakinunua anakuwa na 30 tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…