Cha kuzingatia uendane na mahitaji ya eneo lako ma wahitaji.....wanachuo unajua wanavyovaa unaweza kuwaletea nguo zote kuanzia za kwendea out hadi za kuvaa lecture room...... watu wazima magauni mazuri pia wananunua....
kwamfano kipindi hiki cha baridi kali unaweza ingiza mzigo wako wa koti za korea, ukawa unazimwaga pembeni ya vituo vikubwa kuanzia saa 10 ukauza kwa bei ya elfu 5 yale mafupi na makubwa ukauza elfu 7 kama umenunua kwa belo haitaziri laki 4 (350) ukiuza kwa bei hizo unapata mchanganyiko utauza sana na faida yake ni kubwa pia....
Pia unaweza ingiza zile pullneck sokoni kwa bei ya elfu 5 zinauzika mbaya.....na uzuri wa hizi bidhaa unaweza kuta wabush huko amekuja town anajumua karibu koti 60 hapo unampunguzia kutoka elfu 5 hadi 4000 ila faida inakuwapo.....
Au kipindi cha baridi unaweza ingiza stock za visocks virefu kwa watoto na wadada watu wazima au ukauza mizura kwa bei ya elfu 3 mmoja kama mizuri utaifurahia biashara
View attachment 1816153View attachment 1816154View attachment 1816156