Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

.....JE NILIENDELEA AMA?...
Kwa kweli sijarud tena kuchukua huko mzigo nikaamua kubadili upepo, nikaenda maduka ya hapa dsm kwa wahindi wapumbavu watupu, wezi wale, matusi yao mizigo mibaya kama roho zao, just hasara juu ya hasara...
Kwa sasa nachukua nguo ilala na zinanilipa, kuna jamaa pale wana vijana wao wanapoint nguo kali kali wenyewe wanaita sumu, then inapofika mchana wanazitundika kwa pamoja, wamenizoe nikifika mfano mtu ana nguo kama elf 5000 katundika anakuruhusu uchague zile utakazo na wanafanyaje
1.tops nachukuaga kwa 3000 unauza elf 8000
2. Gauni ndef nachukuwa kwa 8000 nauza mwisho 15,000
3.gauni fupi 5000 nauza elf 10 mwisho
4.skin jeans nachukulia elf 5, nauza 10,000 mwisho,
5.sketi fupi 5000 na kuuza 10elf,
hvyo naona bora hii ya bongo kuliko uganda, sikutaka kuwa mchoyo kwan jf imenisaidia mengi ktk maisha yangu, pia kama kuna m2 ana ushauri kuhusu the way ninavyofanya hii biashara namkaribisha, kama kuna sehemu nyngne pana soko zuri la mtumba namkaribisha pia, nimeandika mara nyngi nyingi coz natumia 4n kuandika, karibuni wadau tusaidiane hasa vijana maisha yasonge mbele.
Mkuu umesaidia sana,binafsi umenifungua macho....ubarikiwe na nitakutafuta nijifunze mengi toka kwako
 
Safi sana ulichokiandika kimeeleweka kimenifanya nami nijiune kuwa naweza kufanya biashara vipi lakini upande wa ushuhuru ukitoa mzigo uganda na ukaleta Tanzania ,mfano mzigo ni wa thamani ya TSH LAKI TANO naomba kufahamishwa🙂🙂🙂
 
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

mkiwa na swali ulizeni
Safi sana mkuu naweza kwenda kwa ndege

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni poa sana ila ogopa kukopesha,hautalipwa chalii angu,nshauza sana viatu na nguo za kike za dukani,now nimehamia mitumba,ni nzuri ila changamoto ni haoo wateja wa kike!

sent from my land lover 109 using Jamii forums app
 
Habari zenu wandugu

Nina shilingi 200,000 nahitaji kufanya biashara ya nguo za mitumba na viatu

KWANINI NIMEAMUA KUFANYA BIASHARA HII?

Kwasababu eneo naloishi kuna chuo ambacho kina wanafunzi 2000+,na chuo kinafunguliwa wiki lijalo

SWALI LANGU
-Ni wapi naweza kupata maroba ya nguo na viatu? (Bello) sina hakika kama ndo yanaitwa hvyo kwa bei ambayo inaendana na mtaji wangu?

NAPATIKANA DODOMA
 
Mkuu ww ni mwanachuo pia???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,Kama unataka kufanya biashara karibu na hicho chuo na umelenga zaidi wanafunzi biashara italipa Lakini kwa nguo za wanachuo nadhani unajua wengi wanavaa nguo zenye grade ya juu kiasi(bei za juu kidogo) haswa kwa wanawake.
Kwa dodoma sijui ni wapi utapata nguo za jumla kwa bei rahisi,Kama utataka kuchukua mkoa wa dar basi ukifika kariakoo hata kwa kuuliza watakuelekeza Au unaweza ukauliza kwa wafanyabiashara wadogo mahali wanapochukulia nguo kwa jumla na bei zake.
Sifahamu sana ila kwa nguo za mtumba kunakuwa na grade inaweza ikawa grade1,2au3 Jitahidi uchukue grade ya kati/juu kutokana na aina ya wateja wako kisha pakia either kwenye basi la kuja dodoma au lori.
Kuhusu mtaji sidhani,ila ungekuwa na angalau laki3 ingekuwa vizur yaani laki2 ununulie mzigo na nyingine laki1 ya matumizi ya hapa na pale.
 
Nashukuru mkuu kwa ushauri wako,ngoja niufanyie kazi
 
Back
Top Bottom