Biashara ya nguo za ndani za kike (underwears)

Biashara ya nguo za ndani za kike (underwears)

Moh04

Member
Joined
May 24, 2015
Posts
12
Reaction score
19
Kama kuna mtu ana uzoefu na biashara ya uuzaji wa nguo za kike za ndani kama vile chupi, sidiria, tight etc naomba anifungue natamani kuijua hii biashara imekua ni biashara nlokua naiwaza siku nyingi lakini sina mwongozo

Tafadhali kwa mtu mzoefu naomba mwongozo
 
Wakuu hii kitu inaonekana ni nzuri pia huku mitaani sijapata kuona maduka mengi ambayo yako special kwa ajili ya kuuza under wear.

Wajuvi wa biashara humu JF watuwekee mchanganuo wa hii. unahitaji mtaji kiasi gani, chupi zinanunuliwa wapi kwa bei gani na huku mitaani zinauzwa kwa bei gani
 
wakuu hii kitu inaonekana ni nzuri pia huku mitaani sijapata kuona maduka mengi ambayo yako special kwa ajili ya kuuza under wear
Wajuvi wa biashara humu JF watuwekee mchanganuo wa hii. unahitaji mtaji kiasi gani, chupi zinanunuliwa wapi kwa bei gani na huku mitaani zinauzwa kwa bei gani

Ingia hapo kuna mjadala unaendana na biashara hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii biashara ni nzuri sana kama eneo unapotaka kuweka kuna biashara pia ni biashara yenye faida ndogo sana lakn kama unaweza kuuza chupi kuanzia dozen tano na kuendelea unapiga ela mm nafanya biashara hii ni mwaka sasa lakn nilipo ni sehem ambyo haina mzunguko kivile lakn napambana sana, aliye na swali wapi pa kupata kwa jumla na biashara hii kwa ujumla karibu ntawaelekeza
 
neysima Aisee Hongera kwa kujua shida ilipo
Unaposena Dozen 5 ina maana ni Chupi 60 kwa siku Aisee mbona mtihani.
Au hapo unakuwa unauza Jumla??
Mtaji kiasi gani uliweka wakati unaanza?
Ukishauza hizo Dozen tano ndio unapiga Hela kama kiasi gani hivi

Kuhusu mtaji inafutana na mahli ulipo kuna watu wanaanza na mtaji ata wa laki lkn mtu anapiga ela unaweza kwenda kkoo na lak moja ukaja na chupi kibao au kidogo kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni lazma ujue unafungua biashara sehemu yenye watu wa aina gani maana kuna chupi za kila aina kuna zenye quality na za kawaida, inabidi kwanza usome watu wa mahali pale alaf ndo uanze biashara
 
neysima Aisee Hongera kwa kujua shida ilipo
Unaposena Dozen 5 ina maana ni Chupi 60 kwa siku Aisee mbona mtihani.
Au hapo unakuwa unauza Jumla??
Mtaji kiasi gani uliweka wakati unaanza?
Ukishauza hizo Dozen tano ndio unapiga Hela kama kiasi gani hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina uzoefu na hii biashara kwa kiasi fulani. Reja reja dzn 5 zisikutishe mkuu, kumbuka hakuna anayeenda dukani kununua chupi 1. Wengi ni 2, 3 na zaidi. Kama eneo lina mzunguko ukipata wateja 20 kwa siku basi dzn 5 unamaliza.

Chupi nzuri jumla dzn ni 34,000 hadi 36,000. Ukiuza @ kwa 4000 × 12=48000. Faida 14,000 hadi 12,000.

Chupi lonya dzn ni 9,000 hadi 13,000. Zote hizi faida ni 8,000 hadi 10,000.
 
Biashara hii inalipa Ni kupambana tu na ukiamua kufungua Jitahidi ukae mwenyewe hizo Biashara za kusema ukikaa mwanaume hawanunui ujue huyo hana shida ya kununua Chupi lakini mwenye Uhitaji ananunua na anakuomba ushauri kabisa hii nzuri?

Kuhusu mtaji ni wewe unajishape kwenye quality ipi Ya chupi but kama utaki showoff changanya quality Mimi hiyo imenisogeza Sana kuna wakati anaingia Mtu anataka chupi Ya 3000 huna unakosa pesa

lakini ipo siku Chupi uliyoinunua 1200 ukaiuza 5000 na mtu akaridhika kabisa

Duh wengine Sio wazuri wa kuandika KILA LA KHERI 2020 Tuzisake pesa Jamani
 
@neysima,Hongera chief, kama hutojali tudadavulie kulingana na eneo lako ulipo unakumbana na changamoto zipi na pia sio vibaya ukatuelekeza kabisa huko uliposema kwenye maduka ya jumla ili mtu yeyeto anapoptia post hii anapata picha halisi kutona na uzoefu wako. Kumbuka haya ni maandishi, yanaweza kumsaidia mtu hata baadaye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehem ya kupata kwa jumla mkuu naomba kujua
Hii biashara ni nzuri sana kama eneo unapotaka kuweka kuna biashara pia ni biashara yenye faida ndogo sana lakn kama unaweza kuuza chupi kuanzia dozen tano na kuendelea unapiga ela mm nafanya biashara hii ni mwaka sasa lakn nilipo ni sehem ambyo haina mzunguko kivile lakn napambana sana, aliye na swali wapi pa kupata kwa jumla na biashara hii kwa ujumla karibu ntawaelekeza
[/QUOTE]
 
Hii biashara inahitaji mtaji kuanzia kiasi gani

yaani lifunguliwe duka la kawaida tu
 
Biashara hii inalipa Ni kupambana tu na ukiamua kufungua Jitahidi ukae mwenyewe hizo Biashara za kusema ukikaa mwanaume hawanunui ujue huyo hana shida ya kununua Chupi lakini mwenye Uhitaji ananunua na anakuomba ushauri kabisa hii nzuri?

Kuhusu mtaji ni wewe unajishape kwenye quality ipi Ya chupi but kama utaki showoff changanya quality Mimi hiyo imenisogeza Sana kuna wakati anaingia Mtu anataka chupi Ya 3000 huna unakosa pesa

lakini ipo siku Chupi uliyoinunua 1200 ukaiubiza 5000 na mtu akaridhika kabisa

Duh wengine Sio wazuri wa kuandika KILA LA KHERI 2020 Tuzisake pesa Jamani

Boss wangu..
Mimi navyofahamu kwa uzoefu wangu biashara ya nguo za ndani huwa inatoka sana akiuza mwanamke hakuna mteja atashindwa kuingia..
Mabinti wadogo wana aibu sana wakikuta anauza mwanaume
Pia wamama watu wazima nao huwa hawapendi kukuta anauza kijana wa kiume..

Ila biashara ya vipodozi ikimkuta kijana mchangamfu pia awe na muonekano asee utauza sana
 
Ngoja nieleze kwa uzoefu wangu mdogo kuhusu hii biashara.

Aina za chupi
Chupi zipo za ubora tofauti kulingana na material. Kuanzia za dozen (dzn) Tsh 8,000 hadi Tsh 45,000 na kuendelea.

Makundi ya chupi
Ninayatenga makundi kulingana na bei na ubora (quality) ya chupi.
1. Kundi la kila dzn Tsh. 8,000 hadi 14,000. Hili tunaliita lonya. Ni zile nyepesi (za wateja wa kipato cha chini).
2. Kundi la kila dzn Tsh 15,000 hadi 32,000. Hili ni la ubora wa kati (za wateja wa kipato cha kati).
3. Kundi la kila dzn Tsh 34,000 na kuendelea ni high quality (hizi za wa kipato cha juu).

Juwa aina ya wateja wako ujue kundi gani la ubora ulangue zaidi. Si mbaya kuchanganya ila isiwe nusu lonya na nusu high quality. Chagua kundi utakalojikita nalo. Mfano, kama wateja uliowalenga ni wa kipato cha chini basi jaza lonya na quality chache, na kinyume chake ni kweli (vice versa is true).
images (3).jpeg

Mtaji kiasi gani?
Inategemea na quality ya chupi uliyoamua kuuza. Mil 2 hadi 3 inaweza kukupa dzn 150 hadi dzn 200 za lonya, huku fedha hiyo hiyo ikakupa dzn 50 hadi 60 ya zile quality. Mtaji unaamuliwa na aina ya mzigo kulingana na kundi la wateja uliowalenga.

Size na aina ya wateja.
Wakati wa kulangua mzigo zingatia uchaguzi wa size kulingana na mahali unakokwenda kuuza. Kumbuka wanunua chupi zaidi ni wadada wa rika la kati, umri miaka 20 hadi 35. Sababu ni kuwa wengi hawana majukumu mengi ya kimaisha, wanajipenda na wako kwenye mahusiano ya mapenzi motomoto (wanatamani chupi nzuri na nyingi ili kuwavutia wenza wao). So, size za kundi hili ndizo ziwe nyingi.

Wapi utapata mzigo wa jumla?
1. Dsm, Kariakoo mtaa wa Msimbazi na muhonda zipo lonya nyingi sana.

2. Dsm, Kariakoo mtaa wa mchikichini na Manyema (kama sijakosea majina) jirani na ukumbi wa DDC. Hapo kuna quality nyingi. Pia yapo maduka machache kule mtaa wa Congo, mtaa wa Mchikichi na Nyamwezi, n.k
IMG_20200109_013518.JPG

3. Mwanza pembeni ya njia panda ya barabara ya Pamba na Miti mirefu. Upande wa stand ya zamani ya Tanganyika. Maduka yako bondeni kidogo (yamejificha).

4. Kampala, Uganda kuanzia makutano ya William street na Ben Kiwanuka Rd, na ukiteremka na hiyo Ben Kiwanuka hadi unakaribia njia panda ya stend ya zamani ya daladala (Kampala Old Tax park). Kabla ya hiyo njia panda kuna maduka yako ndani ndani.

Kumbuka; maduka mengi ya barabarani hapo William street na Kikuubo Rd (tamka Chikuubo) yenye wauzaji wengi ni ya rejareja, maduka ya jumla yako ndani. Kampala duka 1 wanaweza changia watu hata 6, kila mtu anauza upande wake. So, ukiona duka la nje limejaa na lina wauzaji wengi basi kuwa makini, wakijua ni mgeni nao wanajifanya wanauza jumla, then unapunguziwa kidogo kwenye bei yao ya rejareja so unakuwa umepigwa.

Zingatia;
  • Dsm unapata mzigo wa aina zote kwa bei nzuri
  • Mwanza mzigo mwingi ni ile quality ya kati na unatoka Kampala na Nairobi. Nairobi zinatoka Skin tight na brazia nzuri na baadhi hazipo Dar. Bei za Mwanza ni juu kidogo kuliko Dar japo baadhi ya tight na brazia Mwanza ni nafuu na nzuri kuliko za Dar.
  • Kampala chupi nyingi ni quality ya kati (si lonya wala high quality) na nafuu. Tatizo hawana brazia nzuri na tight nzuri.

Muuzaji
  • Kwa uzoefu wangu, wateja wengi hasa wadada (ambao ndio kundi kubwa) wanapenda wauzaji wa kiume hasa akiwa mchangamfu na mwenye kauli nzuri. Muuzaji asipitilize na kuleta utani na mitongozo.​
  • Mabinti wadogo wana aibu, wanapenda wauzaji wa kike, uzuri wao si wanunuzi sana maana bado wanafunzi wasio na kipato. Hili ni kundi dogo.
  • Wamama watu wazima sana wanapenda wauzaji wa kike, hawapendelei wauzaji wa kiume ila endapo akimpokea na kumsemesha kwa heshima, ananunua. Hili nalo ni kundi dogo.
  • Wanaume wanapenda wauzaji wa jinsi zote tu. Akimkuta muuzaji wa kike atatamani ajue yeye anapenda ipi, akiamini atakachopenda muuzaji basi na mwenza wake atakipenda pia. Akikuta muuzaji wa kiume anatamani ampe uzoefu wateja wengi wa kike wanachagua zipi. Hili nalo ni kundi dogo.

Ni chupi tu?
Hapana, lazima uuze na skin tight, brazia, lesso, sox, night dress,vest, boxer n.k wateja wapenda duka lenye bidhaa tofauti (one stop centre) ili amalize shida zake hapo.

Changamoto
  • Mzigo kupitwa na fashion. Usirudie mzigo mara nyingi hata kama ulipendwa. Mara zote uwe na vitu vipya. Design ukishaileta mara 3 au 4 iache hata kama bado wateja wachache wanaiulizia.
  • Wauzaji wa kiume kuingia kwenye mapenzi na wateja.
  • Biashara kuwa kijiwe cha story hadi kuziba wateja. Wadada wanaongea sana hasa ukiwachangamkia na wakikuzoea. Epuka hili.
  • Mteja kutaka kurudisha / kubadirisha nguo ya ndani baada ya kufika nayo nyumbani. Usikubali. Bora anune umpoteze coz hata ukimkubalia utampoteza pia coz atajua ndio mchezo wako.
  • Wateja wa kike kupenda mikopo mikopo. Usikubali.

Kumbuka kutoa zawadi kwa wale wateja wa siku zote na kwa wale wanaonunua mzigo mkubwa. Mf. Kanunua chupi 8 @ Tsh 3000 - Tsh 4000, mpe hata lesso ya 500. Haitokufilisi ila atafurahi sana na utamteka.

Karibuni kwa maswali.
 
Back
Top Bottom