Biashara ya "PHOTO STUDIO"

Biashara ya "PHOTO STUDIO"

Fedora

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
238
Reaction score
172
Wadau nampango wa kufungua kastudio kadogo kwaajili ya kusafisha picha za digital na film, je ni vifaa gani natakiwa kuwa navya na wapi ntavipata. Asanteni
 
Wadau nampango wa kufungua kastudio kadogo kwaajili ya kusafisha picha za digital na film, je ni vifaa gani natakiwa kuwa navya na wapi ntavipata. Asanteni
Kwenye Film no one does that anymore imepitwa na wakati kwahio achana nayo..., cha maana ni kuangalia wewe upo wapi kwenye location yako na kama kuna any big studios karibu yako, kama hakuna basi unaweza tu ukawa na a good inkjet photo printer ukaanza nayo wakati bado unakuza mtaji na ukipata kazi kubwa unapeleka kwenye studios kubwa mjini na wewe unakula commission (unaongeza kidogo kafaida)

What am trying to say is Big Studios wanazo mashine kubwa na expensive ambazo mwisho wa siku huwezi uka-compete nao kwa bei na kupata faida kama unayo a normal inkjet photoprinter.

Ila kama unataka kuanzisha photolab kubwa unahitaji mtaji mkubwa (google minilab) nadhani agfa na fuji is among few brands.., ukiwa na hii mitambo ndio utaweza kutoa picha kwa bei ndogo sana na bado ukapata faida.
 
Asante keysersoze kwa mchango wako
 
Printer aina ya Frontier DL 600 fuji inauzwa bei gani
Binafsi sijui ila nadhani unaweza kupata used kwa bei nafuu ingawa nayo itakuwa bado kubwa.., nimegoogle nimeona hapa ipo around 17,000 usd The Spectrum Minilab Store - Fuji Dry Labs

Anyway kitambo nilishafanya research nikaona kuna kampuni zilikuwa zinatoa franchise kwa fee fulani (ambayo bado ni kubwa) wanakuwa wanakupa mashine na kukusaidia ku-set up business yako. Ila cheki hio site niliyokuwekea hapo juu huenda ikakusaidia zaidi
 
Yeah kweli nimeona inakwenda around USD 17000 excluding shipping nafikiri, sasa hizo kampuni zilizokua zinatoa kwa fee flani hapa bongo zipo? Pia niliiangalia hiyo frontier DL 600 eBay used ipo chini kidogo je niiagizie
 
Nyongeza; usifanye biashara ambayo wewe binafsi huna utaalam nayo. Unajua software zipi za kudevelop / edit picha?
 
Nyongeza; usifanye biashara ambayo wewe binafsi huna utaalam nayo. Unajua software zipi za kudevelop / edit picha?
Mkuu sio kweli kama unajua faida ya kitu (mfano kuku akiwa hai bei ni x) na unajua akipikwa anakuwa 2x hauitaji kujua jinsi ya kumpika au anapikwa vipi, iwapo unatatufa wapishi wa kumpika kwa bei nafuu ambayo bado utapata faida.

You don't have to be an expert on something to profit from it..., so long as you have experts doing that something...

Kwahio jamaa kama kweli amefanya research ameona soko lipo basi haitaji yeye mwenyewe kukaa kwenye hio shop sababu editing kwanza mara nyingi anafanya mteja na developing (ni enzi zile sasa hivi digital mambo ya developing sio kama enzi za mikanda)
 
Hata hivyo mambo ya picture editing siko nyuma sana. Swali langu, hivi nikiagiza hiyo printer Ebay kunamalipo yoyote TRA
 
Hata hivyo mambo ya picture editing siko nyuma sana. Swali langu, hivi nikiagiza hiyo printer Ebay kunamalipo yoyote TRA
Kitu ambacho hakina malipo TRA ni Computer System kwahio hata ukileta vifaa vya computer unalipia ushuru au ukileta printer peke yake unalipia ushuru ila ukileta computer na printer pamoja unaweza ukasema hii ni system nzima kwahio usilipe ushuru...

Anyway mashine / printer kama hii lazima utalipa ushuru.., tena hata kama utanunua used kwa bei ndogo sana ebay usishangae jamaa wa TRA waka-uplift ushuru kulingana na bei ambao wenyewe ndio wanadhani ni muafaka, Anyway kwa estimation hapo fahamu kwamba kuna 18% VAT, Customs (Importy Duty %age kulingana na unachoagiza) pamoja na other charges zote hizo hasitazidi 50%.

Kama utatumia DHL watakufanyia clearing wenyewe ila kama mzigo utakuja kwa freight (cargo) au meli hapo itabidi utafute mtu wa clearing and forwading na umpe agency fee ya consignment (anywhere from laki moja mpaka laki mbili)
 
Mkuu sio kweli kama unajua faida ya kitu (mfano kuku akiwa hai bei ni x) na unajua akipikwa anakuwa 2x hauitaji kujua jinsi ya kumpika au anapikwa vipi, iwapo unatatufa wapishi wa kumpika kwa bei nafuu ambayo bado utapata faida.

You don't have to be an expert on something to profit from it..., so long as you have experts doing that something...

Kwahio jamaa kama kweli amefanya research ameona soko lipo basi haitaji yeye mwenyewe kukaa kwenye hio shop sababu editing kwanza mara nyingi anafanya mteja na developing (ni enzi zile sasa hivi digital mambo ya developing sio kama enzi za mikanda)

Nafikiri hujasoma masomo ya ujasiliamali ndo maana unasema sio kweli.
 
Nafikiri hujasoma masomo ya ujasiliamali ndo maana unasema sio kweli.
Mkuu kusoma na kufanya au kuelewa jinsi ya kufanya wapi na wapi..., kwahio bila kusoma masomo ya ujasiliamali huwezi kuwa mjasiliamali ?

Kwahio wewe unataka kuniambia kufungua garage lazima uwe engineer au kufungua biashara ya ndege lazima uwe pilot. Mkuu ndio maana kuna outsourcing na experts ambao unaweza kuwalipa wakaendesha biashara yako, kuna kitu kinaitwa power of leverage kwenye biashara (Profiting from efforts of others...) ni bora wewe ukatumia 5% ya muda wako na kupata faida kidogo (50%) kuliko 100% ya muda wako na kupata faida yote...

Kwahio kuliko kusema sijasoma hicho unachokijua wewe ndio maana nimesema hivi ni bora kwa faida ya kufundishana unionyeshe kwanini nimekosea kwa kusema nilichosema
 
Nazidi kupata point kwenye hayo malumbano yenu. Asanteni

Lakini kuna mtu amenishauli ninunue printer aina ya Epson L 400 amesema inafaa sana kwa mradi wangu. Naomba uhakika juu ya printa hii kwa anae fahamu utendaji kazi wake.
 
Back
Top Bottom