Mimi sifanyi biashara hii Japo ni mteja wa saloon nzuri na nazipenda kweli kweli. Kwa upande wangu yafuatayo ni muhimu
Saloon ya kiume:
1. Fanya survey na maongezi ya kutosha na vijana watakao kua vinyozi, wengi wao huwa hawajielewi na wanakua na pozi kwa Wateja(customer care ya mhudumu kwa mteja ni muhimu sana) wavalishe uniform
2. Upate nyumba yenye nafasi in which itakua na section kama tatu au nne hivi, iwe na shaving pool, customer waiting area,washing and scrabbing chamber na massage room.
3. Mkuu uwe na mabinti wazuri kama watatu hivi, kwa ajili ya scrabbling,pedicure na manicure plus body massage. Make sure wanakua na uniform kali, siku nyingine vitenge,vikaptula,skin jeans ,tyt n.k. Make sure wanavaa uniform na wafundishe kauli nzur kwa Wateja.
4. Uwe na kafriji kwa saloon yako, make sure ktk bei zako za kunyolea na Huduma nyingine una include na kaela ka soda kwa mteja ila mteja asijue kua ananunua soda. Mteja akiwa nasubiria zamu ya kunyolewa unampa kasoda au Maji na vikaranga fulani amazing,Basi atajiona mfalme na kamwe yaani.
5. Utakapofungua chukua week mbili au mwezi kusoma mazingira ya biashara,then cha kufanya kwa vijana vinyozi unawapa hesabu ya siku au week, kua ww kijana jilipe ila kwa week niletee elfu 70 mezani. Hao ni vinyozi haihusiani na Huduma nyingine.
6. Unapofungua jitahd ndani ya mwezi wa kwanza wa kuanza,Nenda kwenye hit radio station moja ya hapo dom Fanya tangazo ili wakazi wa wajue zawadi ulowaletea.
Kwa saloon ya kike.
Mkuu hii kwa upeo wangu kama mkeo siyo expert wa mambo haya utapata tabu kiasi, management ya wahudumu wa saloon za kike ni ngumu sana.
Tatizo wadada wanafanya ktk saloon hizi hawatulii,wanarukaruka kama nkiwa,Leo yupo hapa,kesho Singida,keshokutwa Utaikuta Mwanza.
Ila ukipata waliotulia utapiga hela. Labda uwachukue na uwafanyie treatment nzuri kuwajenga kisaikolojia watulie. Sasa hapo itabid upate wa sekta zote.
Kusuka, kushonea sijui ndiyo mawigi sijui mawiving, make up n.k. yaan kila sekta iwe na mtaalamu kias ya kwamba hakuna mteja wa kuchomoka.
Customer care ni muhimu pande zote ..
That's all in me sir