Biashara ya salon za kiume na kike

Biashara ya salon za kiume na kike

Una mtaji wa kiasi gani ili tujuwe namna ya kukushauri.Mimi nilifungua saloon ya kiume mwaka 2015 kwa mtaji wa ml8.5

great thinker
 
71590ffc01cd4ab54baa20d1483c0b38.jpg
13aae2a91157918066ede4437927ea66.jpg

great thinker
 
Naombeni msaada wenu,

Kwa anayejua please ili nijifungulie japo hako ka biashara ili nianzishe niwe na sh ngapi na vifaa gani vinavyohitajika?

Please matusi sipendi kwa mwenye moyo wa kusaidia naomba msaada wako.
usiogope boi mm nasoma apa chuo cha duce chang'ombe km upo dsm, nilikua na milion moja nikafungua simple saloon ila bdae nikaongeza vitu kadri siku zinavyozid kwenda mana nilitarget mitaa flan ya keko na chumba ni elfu 40,kit km 100000 na mashine 90000 ambavyo ndo vya muhimu na vikolokolo vidogo vidogo,ILA inategemeana na sehemu uliyotarget iyo yangu ilikua na maeneo ya kawaida tu ila ukitarget uswaz hata lak 5 inatosha mana mtu unamnyorea kwenye benchi tu,for more nichek 0765321403

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.6m +..
Kiti cha kawaida kariakoo 450000
Front frame pamoja na mirror 400000
Resting chair vya wateja 200000
Machine mbili 220000
Vioo vya nyuma na pembeni 150000 pamoja na frame
Vitambaa vitano au sita 120000
Mengineyo 100000
Kodi ya frame inategemea na location ila sehem nyng ni 50000 per month

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habari.

Kama mwanzo nilivyoomba ushauri wa kushusha bei ktk banda langu la chipsi kwa kuuza buku kwa kavu na chipsi mayai 2000 kwa kweli mambo yamekaa vizuri sana japo upande wa chipsi kavu sipat faida nyingi ila mayai namaliza trei tano maana nauza 2000 wengine 2500 na faida apo ni 32000 na mishkak nachukua kilo mbili machinjilion ambapo ni 7000 kwa kilo na inatoa mishikaki ya 22000 na inakua mikubwa sana so kwa kilo mbili napata faida 30000 na kuku nauza nne kwa siku ambao faida ni 12, 000 yaani mpaka raha wajameni hapo viazi ndo vinarudisha ela ya mafuta, kuni na mkaa.

SASA BASI NINA KISALOON CHA KIUME kidogo kidogo hivi keko hapa DSM ambapo saloon za huku kunyoa wakubwa ni buku jero mpaka buku mbili sasa mimi nataka nifanye kunyoa kichwa iwe buku na ndevu jero tu inamaana kama mtu anataka kunyoa kichwa na ndevu atatoa buku jero badala ya buku mbili na ikiwezekana atatoa buku tu vyote mana saloon hazina ishu sasa hivi maana nahisi ningefunga tu bila kutumia hii mbinu na huyo mtu akinyoa kwa buku ataenda kumsimulia hata huko na ataleta wateja wengi kuliko kusubiri wateja watano kwa siku ambao wanatoa buku jero na kupata wateja 30 wa buku..na kodi hapa nalipa 40 kwa mwezi.

USHAURI WENU JAMANI(ubora na udhaifu) na anayeuza mayai ya kisasa aje PM nipo Temeke wailesi tuanze busness

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu habari.
kama mwanzo nilivyoomba ushauri wa kushusha bei ktk banda langu la chipsi kwa kuuza buku kwa kavu na chipsi mayai 2000 kwa kwel mambo yamekaa vizuri sana japo upande wa chipsi kavu sipat faida nyingi ila mayai namaliza trei tano mana nauza 2000 wengine 2500 na faida apo ni 32000 na mishkak nachukua kilo mbili machnjilion ambapo ni 7000 kwa kilo na inatoa mishkak ya 22000 na inakua mikubwa sana so kwa kilo mbili napata faida 30000 na kuku nauza nne kwa siku ambao faida ni 12000 yan mpaka raha wajamen hapo viaz ndo vinarudisha ela ya mafuta,kuni na mkaa.SASA BASI NINA KISALOON CHA KIUME kidogo kidogo ivi keko apa DSM ambapo saloon za uku kunyoa wakubwa ni buku jero mpaka buku mbili sasa m nataka nifanye kunyoa kichwa iwe buku na ndevu jero tu inamaana km mtu anataka kunyoa kichwa na ndevu atatoa buku jero badala ya buku mbili na ikiwezekana atatoa buku tu vyote mana saloon azina ishu saiv mana nahc ningefunga tu bila kutumia hii mbinu na uyo mtu akinyoa kwa buku ataenda kumsimulia hata uko na ataleta wateja wengi kuliko kusubir wateja watano kwa siku ambao wanatoa buku jero na kupata wateja 30 wa buku..na kodi apa nalipa 40 kwa mwezi.USHAURI WENU JAMANI(ubora na udhaifu)....na anauza mayai ya kisasa aje PM nipo temeke wailesi tuanze busness

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana umejitahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saloon itakulipa pia, shusha bei iyo itavutia wengi
Kikubwa uwe na kinyoz mzuri

D.A"mwanaume mashine"
 
Wakuu habari.

Kama mwanzo nilivyoomba ushauri wa kushusha bei ktk banda langu la chipsi kwa kuuza buku kwa kavu na chipsi mayai 2000 kwa kweli mambo yamekaa vizuri sana japo upande wa chipsi kavu sipat faida nyingi ila mayai namaliza trei tano maana nauza 2000 wengine 2500 na faida apo ni 32000 na mishkak nachukua kilo mbili machinjilion ambapo ni 7000 kwa kilo na inatoa mishikaki ya 22000 na inakua mikubwa sana so kwa kilo mbili napata faida 30000 na kuku nauza nne kwa siku ambao faida ni 12, 000 yaani mpaka raha wajameni hapo viazi ndo vinarudisha ela ya mafuta, kuni na mkaa.

SASA BASI NINA KISALOON CHA KIUME kidogo kidogo hivi keko hapa DSM ambapo saloon za huku kunyoa wakubwa ni buku jero mpaka buku mbili sasa mimi nataka nifanye kunyoa kichwa iwe buku na ndevu jero tu inamaana kama mtu anataka kunyoa kichwa na ndevu atatoa buku jero badala ya buku mbili na ikiwezekana atatoa buku tu vyote mana saloon hazina ishu sasa hivi maana nahisi ningefunga tu bila kutumia hii mbinu na huyo mtu akinyoa kwa buku ataenda kumsimulia hata huko na ataleta wateja wengi kuliko kusubiri wateja watano kwa siku ambao wanatoa buku jero na kupata wateja 30 wa buku..na kodi hapa nalipa 40 kwa mwezi.

USHAURI WENU JAMANI(ubora na udhaifu) na anayeuza mayai ya kisasa aje PM nipo Temeke wailesi tuanze busness

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye chips ulifanyaje hadi watu wakajua bei umeshusha nisaidie marketing strategies
 
BIASHARA YA SALON YA KIUME.

Habari za majukumu wanaMwanza, nina salon yangu ya kiume iliyopo Mwanza mjini, eneo la Mabatini, Mtaa wa Kleruu, Nyumba namba 263/09. Ni salon ya kiume, imekuwepo tokea mwaka 2012 na ina viti 2 (viwili) vya kunyolea. Ni salon ya hadhi ya kati. Ina vitu vyote vya muhimu katika salon ya kiume ikiwemo na sehemu maalum ya kuoshea baada ya mteja kunyolewa.
Salon hii nina nia ya kutokuendelea kuiendesha na ninahitaji mtu ambaye atakuwa tayari KUINUNUA/KUIKODISHA ama akanunua vifaa vyote vya salon vilivyomo humo nami nikamalizana nae.

Bei ya KUINUNUA/KUIKODISHA ni maelewano endapo mtu ataonesha nia ya kweli.
Kwa aliyetayari kuwekeza katiaka salon ya kiume tafadahali sana tuwasialiane kwa mawasialiano yafuatayo:

NAMBA ZA SIMU: 0768 111 123 AU 0787 111 123 (PIGA, SMS AU WHATSAPP KWA 0787 111 123)

BARUA PEPE: mkisusi@gmail.com

SKYPE: Kisusi.Mohammed

FACEBOOK MESSENGER: Kisusi Mohammed

Ntashukuru sana kwa kuwasiliana nami kwa ajili ya biashara hii.
Weka picha.
 
Helo wakuu na wadau wa biashara mbalimbali mwenzenu nilihitaji msaada wa mchanganuo wa biashara ya saloon ya kike na vipi kuhusu uendeshaji wake pamoja na jinsi navoweza kujua faida yangu na jinsi ya kumlipa msusi

Kumbuka mm ni mwanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau naombeni wenye uzoefu na hii biashara je nikiwa na milioni 15 naweza fungua BERBAR SHOP ya maana na pesa zangu zikarudi haraka.Aksanteni
 
Back
Top Bottom